Unakwama wapi katika biashara yako?

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,480
5,502
Habari za wakati huu wajasiriapesa wenzetu;

Kwanza kabisa niwashukuru sana wale ambao hunitafuta na kutumia huduma zangu za ushauri na uelekezi ni niwaambie kwamba wanachangia katika kunipa elimu na maarifa mengi huku nikitengeneza kipato kidogo cha pembeni. Nawashukuru pia kwa sababu kila mara kunapokuwa na changamoto huwa wananirudia na kunieleza na hiyo huwa nafasi ya mimi kujifunza na kuendelea kutoa huduma nyingi. Kwa kweli mimi sifahamu kila kitu na mara nyingi mimi na timu yangu huwa tunatumia huduma za wataalamu wengine ambao ni wafanyakazi,washauri waelekezi na wanataaluma na mara zote huwa najitahidia kuelewa yale ninayoelezwa ili niweze kuyaweka kwa usahihi kwa wateja wangu.

Jambo linaloendelea kunitia moyo kila mara ni ukweli kwamba kila aina ya mteja ninayekutana naye huwa anakuwa na changamoto tofauti na mahitaji tofauti na mara zote huwa ninajikuta inanipasa kujifunza kitu kipya kabisa ndani ya muda mfupi tena huwa ninajifunza kwa makosa. Hata hivyo jambo jambo moja ambalo nimejifunza ni kwamba mfumo wetu wa elimu haumuandai mtu kuweza hata kuelewa zile basic abc za biashara na mbaya zaidi hata wale watumishi wa serikali ambao huhusika na usimamizi wa sheria na utumishi wa umma hutumia vitisho,uchanganyaji na upotoshaji wa kimakusudi ili kumfanya mwananchi aone jambo rahisi kuwa gumu.Kwa mfano.LEO hii ukiwa unataka huduma ya aina moja na ukatembelea ofisi tatu tofauti za TRA usishangae ukapewa majibu matatu tofauti na usishangae zaidi iwapo utaenda katika ofisi hiyo hiyo ukakutana na watu wawili tofauti na wakakupa majibu tofauti kwa swala lile lile.

Kwa mfano TANGU TRA waanze kamtindo kakuwa wanatoa TIN ya BIASHARA na isiyokuwa ya BIASHARA ukienda kuhitaji TIN ya biashara unaweza kuondoka na kukimbia kwa sababu ya mlolongo wa mahitaji kwa mfano watataka mkataba wa pango la ofisi as if kila biashara lazima iwe na ofisi tena mbaya zaidi huo mktaba wantaka ili wakutoze withholding TAX ambayo hawajali hata TIN number ya mwenye Nyumba wako yaani unaona kabisa kwamba wanakuchosha.Ukitoka hapo utshangaa wanataka barua ya mjumbe wa serikali ya mtaa wakati unaweza kuhama mtaa anytime na mbaya zaidi hizo barua hazina standards.Sasa mimi sipingi taratibu zao lakini huwa nawauliza ni kwa nini hizi taratibu ni tofauti kwa kila ofisi ya TRA? Ukifuatilia sanaunagundua sana hawa maofisa wa TRA wanafidia UZEMBE na udhaifu wao kwa kuweka vigezo lukuki ambavyo kimsingi havina maslahi.Huwa nawaambia kwamba make it easy cheap and friend for people to pay their TAXES and YOUR COST for collecting Taxes will be minimal.Ule muda mnatumia kukimbizana na walipa kodi na kuwafungia biashara mngeutumia kwa mambo productive.Naelewa TRA huwa wanapita huku na ushauri wangu kwenu ni HUU.Kuweni ni standards na procedures zinazofanana katika nswala la TAX administration na ondoeni ulazima wa watu kupanga fulani katika ofisi zenu waje tu kwa maswala ya lazima.mnaelekea kuzuri ila bado mnahitajika kuboresha.

Sasa nirudi kwenye mada ya msingi ambayo inahusu sswali je UNAKWAMA WAPI NA BIASHARA YAKO. Hili swali ni swali ambalo wafanyabiashara huwa wanajua jibu hawathubutu kusema na wale wanaothubutu kusema huwa hawajui jibu sahihi.Ukipita mijini kwenye baadhi ya maeneo utaona kila siku kunaibuka biashara mpya na nyingine zinafungwa.Ukizingumza na wafanya biashara wakongwe wote utakuwa wana issues nyingi na wengi unakuta wamebaki katika biashara moja kwa muda mrefu kwa sababu tu hawajapata fursa nyingine na wengine wanaitumia kama cover tu na wana njia zao nyingine za kupata kipato.Hii ina maana kwamba BIASHARA sio rahisi.

Biashara ziko za aina nyingi. Zipo za kuzalisha, zipo za kuuza na kununua na zipo za kutoa huduma mbalimbali.Biashara yoyote ina changamoto.Changamoto inaweza kuwa wateja, usimamizi, uendeshaji, teknolojia. Kila aina ya changamoto inahitaji suluhu tofauti.Ni lazima uwe na uwezo wa kuitazama biashara yako kwa jicho tofauti ili uweze kuelewa kwa kina tatizo husika. Hakuna hatari mbaya kama pale mmiliki wa biashara anapo misdiagnose tatizo la biashara yake. Unaweza sema wafanyakazi wako hawafai kumbe ni kiwango chako cha mtaji ni kidogo. Unaweza kusema bidhaa ya ko ni hafifu kumbe hakuna wateja kwa sababu ya location.Ili uweze kutambua tatizo kwa uhakika ni lazima uwe tayari kujitazama kwenye kioo na kujiambia ukweli

Kama mmili wa biashara lazima utambue tofauti kati ya changamoto na visingizio. Wengi huwatunapenda kutafuta visingizio vya kushindwa kwetu ili tukwepe uwajibikaji.Visingizo madhara yake ni kwamba vinatunyima ujasiri wa kutaza tatizo katika uhalisia wake.Unaposjindwa kulitazama tatizo katika uhalisia wake fahamu kwamba uwezo wako wa kuweza kulitatua unapungua.Ukitafuta visingizio utafanya maamuzi ambayo haya ushahidi wa kitakwimu wala kitaalamu na matokeo yako ni kujiingiza katika shida zaidi.

Leo nimeleta mjadala huuambapo nitajitahidi kujibu maswali serious ya wale ambao wako kwenye biashara seriou kwa kunijibu swali liloko kwenye mda hapo juu ambalo ni JE UNAKWAMA WAPI KWENYE BIASHARA YAKO? Zingatie kwamba mtu yeyote hata wewe unaweza kutoa majibu kulingana na uelewa na uzoefu wako hivyo ni mjadala huru. Hata hivyo iwapo una maswali ambayo ni binafsi sana kulingana na aina ya biashara zako au aina ya taarifa unazotaka kuweka basi unaweza kutuma kwa njia ya email kwenda masokotz@yahoo.com.Usiogope kurudia swali au changamoto kwani naamini huu uzi unaweza kuwa darasa kwa wengine.

Kuhusu SISI

Masoko Consulting ni Strategic Consulting Firm (Washauri waelekezi wa Kimkakati) ambao tunatumia mbinu za kisasa na utaalam wa kisasa katika kuwasaidia wateja wetu kutambua fursa na kuzitumia kwa ajili ya kukuza biashara zao na kukuza faida.Lengo letu ni kuwasaidi wafanyabiasha wadogo na wakati kubadilisha na kuboresha mfumo wa uendeshaji na usimamizi wa biashara zao ili ziendane na dunia ya kisasa kwa kuwawezesha kufikia zana za kisasa,utaalamu wa kisasa na teknolojia katika kuendesha biashara zao.

Sisi tunatoa huduma ya usajili wa Majina ya biashara,kampuni,leseni,TIN number NGOs, Taasisi za Kijamii, SACCOS, Taasisi za KIDINI,Taasisi za ELIMU,Viwanda,UWEKEZAJI na pia tunatoa ushauri juu ya namna bora ya kuendesha biashara yako.Unaweza kupata huduma hizo kwa gharama nafuu.Baadhi ya huduma hizo ni pamoja na:
  1. Kwanza tutakushauri kuhusu muundo wa biashara yako faida na hasara pamoja fursa mbalimbali
  2. Pili tutakufanyia utafiti na ushauri wa Jina la Biashara yako kwa kuzingatia vigezo vya SOKO
  3. Tutakufanyia Taratibu zote za usajili kuanzia Uandaaji wa Nyaraka Mpaka Kukamilika kwa Usajili Kampuni, TRA, Mashine za EFD, Vibali vya TBS pamoja na leseni
  4. Tutakuandikia Company Profile ya Kisasa kwa Lugha ya Kiingereza na Kiswahili
  5. Kama unahitaji mkopo kutoka katika taasisi za fedha tutakusaidia kufanya mchakato kwa kuzingatia mahitaji yako na vigezo vya taasisi husika.
  6. Tutakutengenezea Website ya kisasa kwa ajili ya Biashara na huduma zako.
  7. Tutakutengenezea, Logo, Business Card, Letter Head pamoja na Nyaraka nyingine za Kibiashara
  8. Tutakupatia Mfumo wa Kutunza kumbukumbu kwa njia ya Mtandao au kwenye Computer yako kwa ajili ya kusimamia Biashara yako
  9. Tutakufanyia Initial Marketing kwa Wateja wako (Inategemea aina ya biashara) wa Mwanzo ili kuwa na customer base ya kuanzia
  10. Pia tutakusaidia Mchakato wa Kufungua Bank Account kwa kutumia jina la Biashara yako (Deposit Ya Kwako)
  11. Tutakuwa nawe katika mchakato mzima wa kuendesha biashara yako mpaka itakapokuwa stable na wewe kupata uzoefu wa kutosha katika biashara yako.
 
Back
Top Bottom