Unakumbuka wapi mdudu huyu?


Nakumbuka tukiwa darasa la kwanza na la pili tulikuwa tunawabaka hasa wale wakubwa zaidi kisha tunachimba vishimo vidogo chini tunawaweka na kuwafunika na vioo. Basi wakianza kutembea tembea humo ndani ya vishimo tunafurahi ile mbaya kuwa tunaangalia sinema. Duh! Jamani zamani ilikuwa raha sana! Leo hii mwanangu akiona panzi mkubwa anaweza kupiga mayowe kwa woga!
 

Ni kweli kabisa watoto wamenyang'anywa msamiati. Tulikuwa tukibembea tunasema 'nasikia uroda' na haikuwa na shida yoyote kusema hivyo.
 
huyu tulikuwa tunamwita panzi akiruka juani utasikia anatoa mlio parrrrr parrrrrr
ukimkamata vibaya anakuchoma na miba ya kwenye mikono yake.. ni watamu sana hasa ukikuta alikuwa anakaribia kutaga, wanapatikana sana sehemu wanazolima mahindi

Jiwe Linaloishi we unatokea Kilimanjaro eeh?
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli kabisa watoto wamenyang'anywa msamiati. Tulikuwa tukibembea tunasema 'nasikia uroda' na haikuwa na shida yoyote kusema hivyo.

siku hizi je uroda uko pande gani...?? tataaa
 
ha ha ha nakumbuka mbali mtoto wa kiume ukiwa uchi utasikia mama anakuambie "shikia nzie yoo"
 
ukikamata wa kijani tunaita umekamata barare mzungu,halafu kuna wale wa nyakati za mvua hawana mbawa wana vistari stari tuliwaita barare komba mavi duh mbali sanaa big up mkuu.
 
Chuo cha Ushirikaaaaa..Moshi those days!!! tulibaka panzi mpaka mwereni kule..old moshi sekondari...daaah..neshno housing...kuzurura tu..!!!

Good Old days...😛layball:
 
nme mwinda sana uyu mdudu...enz hizo nachunga mbuzi
 
............lakini leo hii ngoja umkute akiwa Ofisini kwake anavyojifanya bosi, wakati utotoni kala sana Balanguru.....na kakamata sana balale.
Ahaaaa! Binamu yangu vipi tena mbona unaniaibisha mbele ya vijana?
 
Mkuu we nomaa nimekumbuka enzi hizoooooooooo na marafiki zangu wa kipindi hichoooooooooo na mavazi yangu ya kipindi hichooooooooooo kikwetu tunamwita ''NGALAGA'' na wale wa rangi ya blue ni "KALIMBO".
 
mi nkae kimya, hawa huwaga nawaona kwenye picha, kutokana na maisha niliyo kulia nimemiss vingi.
 
Kizazi cha sasa hakibaki baranguru bali mouse play station .hizi ndizo play station za enzi hizo
 
Ina maana kila siku wee ulikuwa unabakiwa hayo mabalale/mabalangulu!
 
huku masasi tulikua tunawaita NANTEETE. nakumbuka sana nikiwa chiungutwa miaka ya 1995-1996
 
paradeee....ndio tulikuwa tunalitumia mtaani kwetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…