Unakumbuka wapi mdudu huyu?

Dahhh, yaani nimekumbuka sana LIZABONI, SONGEA PALE PALE KWENYE MSUFI ULIOKATWA, tulikuwa tunmwita LIMBALA AU LIMBALANGULI... Tena kuna yale yenye mabawa mekundu ndani tulikuwa tunayaita mambalanguli rangi ya simba.... Wakati mwingine tulikuwa tunamwita MDEDE...
 
Kweli mkuu humchezo ni noma, inafika kipindi mpaka madaftari yana kuanguka lakini huna habari, sasa ngoja urudi nyumani upambane na kibano. Kwanza ume chulewa kurudi skonga, pili madaftari yame pungua ndani ya bag basi balaa tupu

............lakini leo hii ngoja umkute akiwa Ofisini kwake anavyojifanya bosi, wakati utotoni kala sana Balanguru.....na kakamata sana balale.
 
Weeh koma kabisa! Alikuwa ananikuna dada saa ananisugua mgongo na miguu.
Hahhaa. Mie sikuwahi ona wakiliwa. Kubaka na mikono ilikuwa mtindo mmoja!
 
Balale wanaliwa? Najuuuta, manake tulikuwa tunawabaka kwenye majani. Ukitoka kubaka balale ukienda kuga unawashwa ile mbaya.
Enzi hizo kubaka was not a crime
King'asti hujakula balale wewe?? mwenzio hawa tulikuwa tunawachoma ama kuwakaanga kwenye kigae pasi mafuta.

kasheshe ilikuwa kwamba unakwenda kumkamata balale kwenye nyasi ndefu sana sasa kama kuna mabua ya mahindi yanakukata kama kisu ukienda kuoga unawashwa kama vile umemwagiwa ----- halafu una mikwaruzo kama vile njia ya gari mweeh!

sasa ukiwa mdada huwez kuwabaka vizuri lol! unajikuta unalipishwa na vibonde kulipa kwenyewe inabidi iwe ..................... dah! hapa nafkiri wale wazee wenzangu Asprin SnowBall DARKCITY watakumbuka vyema malipizi yake.
 
Last edited by a moderator:
kikwetu tuliimita GUGWA

There you are; nilikuwa najiuliza tulikuwa tunamuitaje, jina likakataa kuja kbs. Na majina mengine didn't sound familiar, umenikumbusha mbali, niliambiwa na mama nilinde nyumba (nisitoke); tukaenda kubada/kubaka Gugwa, kurudi tumeibiwa. Sikuchapwa lakini! Lol
 

LI NG'AGA lyabugi. GALIHO NA MA BUNGU, GENE GA MANANA GA BULULU, GAKUBIZA ULU LIZA LYAMUA KULALA KWINGILA SOKONI KARIAKOO MPAGA LYUSHIKA I KIBAHA AHA MIZANI.

Huyu panzi anaitwa Ng'aga, walikuwepo na wengiine wakubwa zaidi ya huyu wanaitwa Bungu. Bungu anaweza kuruka trip moja kutoka sokoni kariakoo hata akafika Kibaha kwenye Mizani, mkwala wake ni matatizo!
 
Watoto wanajipanga kwenye msitu wa majani kama wapo vitani. Kumbe wapo busy kukamata panzi.
 
I wish ningekuwepo nikakukamatia.......!Damn!
 
Zamani maana ya kubaka ilikuwa ni kumkamata panzi au balanguru, siku hizi kubaka ni noma.

Umenikumbusha. Watoto wamenyang'anywa msamiati. Hata neno uroda lilikuwa linatumiwa sana na watoto lakini sasa hawana uhuru nalo tena. Natamani kuitisha maandamano ya watoto nchi nzima kudai msamiati wao ambao umeporwa na wakubwa. Haki za watoto hapa "zimebakwa".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…