Wadau wa jukwaa, wasalaaam.
Hiki ni kipindi cha lala salama kwa utawala wa JK na sio vibaya tukiangalia moja ya mbinu aliyoanza nayo, kulifanyika semina elekezi kwa ngazi nyingi za juu pale Ngurdoto hotel.Katika kujadili hili tuangalie ufanisi na changamoto zilizojitokeza katika utawala wake na mchango wa zile semina na nyingine nyingi, pia ikumbukwe huu ndio utawala uliopatwa na misukosuko mingi. Tujue kama walienda kutafuna kodi zetu au kuna kitu wametuengezea .
Karibuni,
Mashamba.
Mkuu umesahau kidogo.
Kabla ya semina elekezi alizunguka kila wizara, akasikiliza matatizo yao na kutoa maelekezo, lakini sidhani kama alifuatilila tena utekelezaji wa maagizo yake....!!
vasco da gama hakuwa na uwezo wa uraisi
Itakua alikuja kuyasahau kutokana na haraka ya kwenda kujitambulisha nchi za ulaya na amerika mkuu