1987 braza angu alileta kanda ya alpha blondy enzi hizo nyimbo km idjidja, afrique, intepranetary revolution, brigadier sabare kwa kweli mimi kwangu alpha blondy ni zaidi ya lucky dube! Nyimbo zake zinanipa raha mno! Ile afrique bd inaleta burudani. Mbili miaka ya mwanzo ya tisini yaani kuanzia 1989 nikuwa Iringa nilipenda sana kusikiliza idhaa ya kingereza ya kenya, walikuwa wana vipindi vizuri sana na miziki ya kizungu waliipiga sana. Namkumbuka mtangazaji wa reggae time kbc nairobi akiitwa jeff mwangeni aka crucial jeff jamaa alinifanya nisikikose hicho kipindi kila alhamis saa mbili kamili asubuhi mpaka saa tatu. Tatu miaka hiyo family yetu hatukuwa vizuri sana mzee wangu alipenda sana kusikiliza redio kenya ya kiswahili siku za jmosi na jpili akiwa home, wakati huo tulikuwa tunakamua ndondoz daily, kenya ni wataalam sana wa kutangaza bidhaa zao, lile tangazo la roiko mchuzi mix lilituokoa ndondoz zetu zikatafutiwa mchuzi mix sasa tukawa tunatafuna ndondoz kwa flavor tofauti. Nne ilikuwa ikifika saa tatu kasorobo mzee anazima radio yake anaichuku room kwakee utasikia tu tatu kamili kale ka mziki ka majira enzi hizo radio Tanzania.