Unakumbuka hii mwanawane

Yes, this was really nice...Enzi hizo MCHINA iko juu sana, maeneo ya kwetu ilikuwa ni walimu tu wanayo majiko hayo, tulikuwa tunawaona wako juu kimaisha ile mbaya!
 
them good old days...machozi yamenilenga aisee kwa kuiona hiyo picha. Nashukuru i lived during those times za sayansi kimu na sayansi kilimo na sanaa... I am a better person because of such classes.

Ni jana usiku tu nime-repair sarawili yangu iliyotatuka kabla sijaipasi. Watoto wa siku hizi hizi kazi ndogondogo za nyumbani hawajui..inasikitisha sana.

Kizazi cha twitter na facebook!
 
Dah, nilikuwa anfundisha hili somo shule ya msingi Shamaliwa.
Afu wakati wa umitashumita, raha kama nini
Ni mwendo wa kula miwa na mihogo tu.
 
Enzi hizo kulikuwa na Mitaala, na mambo yote ya Elimu yalisimamiwa na Wizara husika. Cheki hata hicho Kitabu hapo chini kimeandikwa "Kimetolewa na Wizara ya Elimu ya Taifa". Sikuhizi Wizara imeacha wachapaji binafsi waingize mawazo yao binafsi mashuleni ingawa mitihani inaletwa na Wizara. Utakuta kitabu kimeandikwa "Kimetolewa na Kuchapwa na Nyambari Nyangwine". Watoto wakifeli tunastandardize halafu tunatoa Matokeo Remix! Ee Mungu utusaidie.
 
Kiukweli haya masomo yalitufanya tuwe wasaidizi wa wazazi/ walezi wetu. Kwa kuona picha kam hiyo tu kulitosha kuona kuwa jioni ukitoka shule atleast uchote maji, unyweshee maua, ufungie kuku (kwa wale walio fuga kuku wa kienyeji) ufagie, umsaidie mama jikoni lakini siku hizi wakitoka shule tv na wao, wao na tv.. Mengine yote anafanya dada (Mschana wa Kazi). Mtoto wa kike alijua majukumu yake na wakiume vivyo hivyo... Haya mabadiliko hewa ya sasa hivi yametupelekea watoto wenye vitambi maana hawajishughulishi wala hawataki shuruba
 
hujakosea ndugu, yaan siku hizi wakitoka shule ni tv na playstation, hata mpira wa madaso siku hizi hamna. sis home ukitoka shule kama ni zamu yako kuosha vyombo au kuchota maji unafanya fasta ukacheze mpira, dada wa kazi alikuwepo lakin kama kiranja wetu kutusimamia kufanya kazi.
 
Dah! Tumetoka mbali sana! Na huyo binti ktk cover hapo juu sasa ni mtu muhimu sana serikalini! dah! utaniliza aisee!
Mkuu naomba -unijuze, huyu binti ni nani vile? Ila nimekumbuka mbali sana!
 
Tulipotoka ni pazuri mno! Watoto tulikua tunagawiwa hivi vitabu bure, halafu tunakunywa Uji wenye maziwa Duh ilikua safi sana! Lakini sasa hivi watoto wetu wameletewa vitabu vingine vya ajabu sana, eti Kitabu cha hesabu kinasema 7 x 2 = 15:A S-frusty:
 
kumbe na wewe ulikuwepo enzi hizo nikafikiri wewe ni wa dot.com pole kwa hayo machozi ndo nilikuwa nakuuliza kulikoni mwenzangu pale kwenye kochi kumbe umeona hiyo kitu kwa laptop hapo hata usinshtue mwenzio nami nione
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…