MoroGent
Senior Member
- Jan 10, 2018
- 146
- 460
Salaam sana Wanajukwaa,
Unakumbuka hadithi ya kitabu cha "A Wreath for Father Mayer:😀😀
Kitabu hiki ni hadithi fupi iliyoandikwa na S. N. Ndunguru (aliandika Stori maarufu ya SAFARI YA GARI MOSHI 😀 na kutafsiri Rosa Mistika cha Shabaan Robert).
Kiujumla kitabu hiki cha hadithi fupi Kinaelezea maisha ya Padre Mayer, mmisionari wa Kijerumani aliyehudumu Tanzania kwa miaka mingi, hasa kipindi cha ukoloni na baada ya uhuru. Padre Mayer alikuwa mtu mnyenyekevu, mwenye kujitolea sana kwa watu wa kijijini – aliwasaidia kielimu, kiafya, na kiroho.
Wakati wa maisha yake, alipendwa na kuheshimiwa sana na wanakijiji, lakini pia alikumbana na changamoto za kikoloni, mabadiliko ya kisiasa, na mgongano wa tamaduni. Alijitahidi kuishi kwa haki, upendo na huruma licha ya mazingira magumu.
Baada ya kufariki kwake, wanakijiji walikusanyika kumpa heshima ya mwisho, wakitambua mchango wake mkubwa. “Wreath” (taji la maua) linawakilisha heshima, kumbukumbu, na shukrani kwa maisha yake ya kujitolea.
Ni hadithi ya maadili, upendo kwa binadamu, na urithi wa wema unaoishi hata baada ya mtu kuondoka.
Nawasilisha,
Je na wew huwa unakumbuka kusoma vitabu vya zamani ukajikumbushia?