Unakijua chuo kikuu cha Dar es Salaam?

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,743
25,535
Uuuuuwiiiiiiii!!!!!!!!!!!! Yarabiiiiii!!!! Mwaka 2009 nilipatwa na furaha isiyokuwa na kifani baada ya kuchaguliwa kujiunga na masomo ya juu katika ngazi ya uhasibu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Nilimshukuru maulana kwani ndoto yangu imetimia kwani sio tu kwamba nimefanikiwa kujiunga na masomo ya juu bali ni kwa kufanikisha ndoto zangu za kusoma Chuo Kikuu barani Afrika na duniani kwa ujumla. Toka utotoni nalikua na fikara za kuitwa mwanazuoni wa “Mlimani”…..

Taswira niliyokuwa nayo awali juu ya kisima hiki cha fikra na kituo kikuu kilichozalisha nguli wa kila aina barani Afrika na ulimwenguni ni tofauti kabisa na hali halisi niliyoikuta ndani ya mdumange wa Mlimani. Ama kweli wahenga wanasema urembo wa mwanamke si muonekano wa sura bali kilichopo ndani ya kijuba cha moyo wake.
Chuo kikuu cha Dar es Salaam, ndicho kilichokuwa kitovu cha harakati za ukombozi wa bara la Afrika. Kina Robert Mugabe, Samora Machela, Senghor, Madiba, Kenyata na wengine lukuki wakiongozwa na Mwalimu J.K. Nyerere waliendesha harakati za ukombozi na kudai uhuru wa nchi zao na bara la Afrika kwa ujumla chini ya “Rev Square” ya chuo cha Mlimani.

Maraisi kama kina Salvar kiir, Yoweri Museveni, mwanaharakati Garang’ wote ni mazao ya chuo kikuu cha mlimani. Usisahau kina Walter Rodney (how Europe underdeveloped Africa) naye ni mjeshi wa kitalu hiki cha Mlimani.

Hapa Tanzania viongozi wa sekta mbalimbali na hasasi tofauti tofauti ni mazao ya UDSM. “Prof” Kikwete, PROF. Lipumba, Zito Kabwe, Mbatia, Mnyika, Shivji, Kabudi, Bana na wengine kedekede ni tanzu za kitalu cha Mlimani.

Daaah!!!! Ama kweli kwa UDSM kuwa chuo bora Afrika ya mashariki na kati inastahili kutokana na mazao yake kuonekana kote duniani na mbegu zake kuota na kutoa vivuli kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Nikiendelea kulumbana juu ya umahiri na umaarufu wa kijiwe hiki cha wasomi nitamaliza kurasa nyingi bila kufika tamati.

Pamoja na mbwembwe na sifa lukuki za mrembo huyu “Mlimani”, kuna baadhi ya mambo nikiyaanika hadharani hutaniamini ama utaniona nina kinyongo na mzee wa posta, Prof Mkandala. Wengine watasema ni msukumo wa msimamo na mrengo wangu kisiasa na wengine watadiriki hata kusema natukana wakunga baada ya kumwona mwana. Lakini ukweli niwahubirie hadhira yangu, sina hila yoyote na kitalu hiki na mtizamo wangu huu utasaidia wadau mbalimbali warejee nyuma na kusaidia kukabiliana na changamoto hizi ambazo zinaelekea kuzaa hadi vilembwekeza.

1.MAZINGIRA YA KULALA

Kwa mtu asiyejua unaweza kupiga picha na kudhani mazingira ya kuishi kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Afika yanalandana na hadhi ya chuo chenyewe. Mazingira ya hostel za Mwalimu Nyerere Campus ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, hayafanani hata na mazingira ya Shule ya Sekondari Arusha (Sekii).
Nianze na majengo. Kila mwaka ripoti mbalimbali za wataalamu wa majengo, zinaonyesha kuwa jengo la Hall V na Hall II of resident ya Mlimani Campus hayafai tena kuishi binadamu. Wataalamu hawa ambao nao pia ni sehemu ya waadhiri ya UDSM wamekua wakitoa tahadhari hizo kwa utawala wa Chuo na serikali kwa ujumla lakini wote hawa wameonekana kukalia masikio na kutosikia lolote linalonenwa na wasomi hao. Kwasasa imekuwa ni desturi ya kila mwaka kubomoka kwa sehemu ya ukuta wa maghorofa haya yanayotumiwa kwa malazi tena wanafunzi wakiwa wamejipumzisha na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na wahusika. Lakini labda wanasubiri siku moja watu wafe halafu baadaye iundwe tume ya kuchunguza na kikundi Fulani kujitengenezea fedha kupitia dili hilo.
Vuta picha majengo ya ghorofa kumi na moja kila moja (11 Floors) yaliyojengwa zaidi ya miaka 50 iliyopita na hadi sasa yanatumiwa na watu na mbaya zaidi idadi ya wananchi wanaoishi humo wameongeza ijapokuwa hakuna urekebishwa wala uboreshwaji wa miundombinu zilizopo. Vyoo vinavyotumika kwa kila floor ni kama matundu 3 na mbaya zaidi ni ya kukalia. Idadi ya watu wanaokaa kwa kila floor ni zaidi ya 35 na wote wanapata huduma kwenye matundu haya matatu tu ya kukalia.
Je, Hapa kupata maradhi ya fangasi sehemu za siri kutakwepeka kweli?? Je, Serikali na wadau mbalimbali hawalioni hili??
Mbali na miundombinu ya kupatia huduma binafsi kuwa hafifu, vitanda vilivyopo kwenye kila chumba ni viwili vya double deka. Vitanda hivi ni size ya mita 2 kwa sita (2x6) lakini hulaliwa na watu wawili kwa kulala mzungu wanne. Nikisema mzungu wanne namaanisha kunyonyana vidole kwa mmoja kuelekeza kichwa mashariki na mwingine magharibi.
Hali ya malazi haijaisha hapo, bado kuna vigodoro vinavyojulikana kwa jina maarufu kama “ulimi”. Vigodoro hivi hutumiwa na wanafunzi ambao wamekosa malazi kama sehemu ya kuweka mbavu zao unapoingia usiku. Ifikapo kipindi cha mitihani wengine hulala kwa kupokezana na wengine hufikia hatua ya kulala juu ya meza za kusomea kama sabufa na hata wengine kulala uvunguni kama mende. Dah!!! Ebwana hiyo ndiyo Mlimani ambayo wengi walio nje ya karandinga hili hawajui yaliyomo ndani yake.

2.MIUNDOMBINU YA MAJI MACHAFU.

Chuo Kikuu na cha kuheshimika barani Afrika na chenye wanataaluma na wataalamu nguli Afrika, kila kona kuna mifereji yaliyojitengeza ya vinyesi na mikojo. Ukiwa eneo la Academic bridge kwa wale waliopata bahati ya kufika eneo hili, kuna matiririko ya mchanganyiko wa mavi na mkojo ambao hutirirka ovyo tena imekua jambo la kawaida sana na lililozoeleka kwa wanazuoni wa jamvi hili kwani wanafunzi na waalimu wanaotoka Economics department kuhudhuria lecture za Theater one na two wamekuwa wakisaidia kuchanganya mchanganyiko huu wa vinyesi kwa kutumia miguu yao bila kupenda.
Miundombinu hii ya maji machafu kila kona ya kitalu hiki cha fikra hayaridhishi kwani kila kona ukipita utakutana na mtirirko wa mavi na mikojo kitu ambacho kinaharbu na kushusha hadhi ya kiota hiki cha enzi cha kitaaluma.

3.MIJADALA, KONGAMANO NA MIDAHALO YA KITAIFA/NA KIMATAIFA KWA WANAFUNZI.

Ili kukuza uwezo wa vijana wetu kuhoji na kuyafahamu mambo mbalimbali yanayotokea duniani na yanayoikumba nchi, wazee wa zamani waliweka eneo maarufu kwa jina la Revolution Square kama sehemu ambayo vijana wasomi wa kiota hiki cha fikra wataweza kukutana na kujadili masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kwa manufaa ya nchi yetu na bara letu kwa ujumla. Hali ilivyosasa, lile eneo limegeuzwa ni haramu na mtu yeyote atakayesimama pale mara moja hufukuzwa chuo na kufungiwa udahili katika vyuo vyote vya umma na kupata mikopo ndani na nje ya nchi. Shughuli mbadala inayoendeshwa ndani ya eneo hili ni ukataji wa majani ya kulishia ng’ombe. Kama Mwalimu Nyerere angekua mbinafsi na kuzuia vijana kujitengenezea uwezo wa kuhoji na kujenga hoja, leo tungekua na kina Kikwete tungewapata? Kwanini mnakuwa waoga kwa kuwafunga vijana midomo ili wasikemee uozo na utumbo mnaoufanya? Eti kisa cha kufunga eneo hili ni kwasababu Ndugu Mkandala amepewa onyo na Ndugu mmoja wa Posta kuwa eneo hilo linazalisha vijana wenye uwezo kwa vyama vya upinzani. Shame up on you!!!!!!!!! Yaani unatanguliza mrengo wako na msimamo wako kisiasa kuliko maslahi ya nchi na vizazi vijavyo? Kweli akili ndogo siku hizi imetawala akili kubwa na akili hiyo kubwa imekubali kufyata na kuuza dhamani ya maarifa na ujuzi wake kwa digrii za kichina…….

ITAENDELEA.............
 
kuhusu hall 2 nikweli kabisa mwaka jana ukuta ulidondoka asubuh nikasema kifo chaja

kuhusu miundombinu ya maji ndo usiseme ivyo vyoo mkuu havifai kbsa
 
Sitaki kukumbuka vyoo vya hall three au vile vya pale seminar rooms. Nikiwa chuo Mlimani nilipata UTI hadi kufikia stage ya kukojoa damu sitakaa nisahau!!! Usafi wa pale ni zero kabisa. Nakumbuka tulikua na trip nyingi za Mlimani city kila jioni maana vyoo vyao atleast vilikua visafi... kwa hiyo mtu unajikaza simu nzima ukimaliza vipindi unaenda kushusha mzigo Mlimani City!!! That was 6 years ago.....
 
Kwahiyo huoni kama mwenzetu ulifaidika na angalau uliweza kuondoka UDSM na Degree mbili moja ya Kitaaluma kabisa na nyingine ya Uchafu uliotukuka?
 
Sitaki kukumbuka vyoo vya hall three au vile vya pale seminar rooms. Nikiwa chuo Mlimani nilipata UTI hadi kufikia stage ya kukojoa damu sitakaa nisahau!!! Usafi wa pale ni zero kabisa. Nakumbuka tulikua na trip nyingi za Mlimani city kila jioni maana vyoo vyao atleast vilikua visafi... kwa hiyo mtu unajikaza simu nzima ukimaliza vipindi unaenda kushusha mzigo Mlimani City!!! That was 6 years ago.....
 
Sitaki kukumbuka vyoo vya hall three au vile vya pale seminar rooms. Nikiwa chuo Mlimani nilipata UTI hadi kufikia stage ya kukojoa damu sitakaa nisahau!!! Usafi wa pale ni zero kabisa. Nakumbuka tulikua na trip nyingi za Mlimani city kila jioni maana vyoo vyao atleast vilikua visafi... kwa hiyo mtu unajikaza simu nzima ukimaliza vipindi unaenda kushusha mzigo Mlimani City!!! That was 6 years ago.....
pole sana
 
M City kote kule si ungekuwa unakuja kunya CoET mkuu.. hawakatazi
 
Hii ulichosema ni ukweli, ila mentality ya walimu na wanafunzi hapo ni DESA TUU ukianza mambo sijui mazingira yamefanyaje yaani woote wanakushangaa.
Mambo yanayopigiwa kelele toka kwa wanafunzi ni BOOM, ADA, UCHAGUZI WA RAIS WA CHUO etc
 
Dah! niko mwaka wa kwanza miaka kama 10 iliyopita niko hall 2 alfajiri tukasikia vitu vinaanguka niko floor ya sita tulitoka mbio sitasahau kumbe yalikuwa yale yanayojengwa kwa ajili ya kukinga jua kutoka floor ya nane yalikuwa yamekatika sasa katika kudondoka yakawa yanapiga yale yote yaliyokuwa usawa wake ilikuwa balaa, kwa upande wa vyoo dah ilikuwa ni hatari sana ama ujisaidie ukiwa umechuchumaa au uweke toilet paper kuzunguka sink la kukalia maana ukicheza tu ukakalia hivi hivi lazima utoke na maradhi.
 
Back
Top Bottom