Unakaribia kuoa au kuolewa moyo unakuwa mzito

Unakaribia kuoa au kuolewa moyo unakuwa mzito

Papa Mopao

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2009
Posts
4,166
Reaction score
2,670
Hii ni nini?

Ni wasiwasi ama wrong choice ama matarajio yamekuwa tofauti, ama vita vya kiroho?

Hii nimeisikia sana watu wakilizungumzia huwa inawatokea watarajiwa kwa vipindi tofauti

Wazoefu mnasemaje, kuna ukweli wowote hapo?
 
Ndoa sio jambo la mchezo.....kuishi na mtu mwenye tabia, maoni na mtazamo tofauti sio jambo jepesi............

Yapaswa kuwa makini kwenye uchaguzi na upendo ili kumpata aliye sahihi, hata kama ametoka kijiji au mjini
 
Ukweli ni kuwa, moyo huona mbali kuliko macho. Moyo hutoa ishara kuwa jambo hili halina mwisho mwema, macho hutazama nje na kuupinga moyo, akili huchambua na kupuuza. Hivyo wale wachache wanaojua kucheza na miili yao wamefanikiwa kuwa na mahusiano mazuri yenye changamoto zinazohimilika.
^^
 
hii ni ngumu aiseee.......binafsi ningesali kujua ukweli......ningemwambia Mungu kama huyu ndie ubavu wangu na ndoa ifungwe.....na kama sie....basi tutengane.....kila mtu aendelee na maisha yake......
 
Kila hisia hasi au chanya huwa na sababu nyuma yake...

Yote uliyotaja yanaweza kuleta uzito wa moyo...
 
ni kweli, wakati wa karibu na harusi yangu ilikua hivyo. Nilisali sana. Naamini ni vita ya kiroho coz shetani hapendi jambo jema.
 
Kila hisia hasi au chanya huwa na sababu nyuma yake...

Yote uliyotaja yanaweza kuleta uzito wa moyo...

Kwamba huna uhakika kama huyu ndiye Mungu aliyekupa au la? mara nyingi maswali ya kujiuliza yanatawala sana kipindi hiki
 
Ukweli ni kuwa, moyo huona mbali kuliko macho. Moyo hutoa ishara kuwa jambo hili halina mwisho mwema, macho hutazama nje na kuupinga moyo, akili huchambua na kupuuza. Hivyo wale wachache wanaojua kucheza na miili yao wamefanikiwa kuwa na mahusiano mazuri yenye changamoto zinazohimilika.
^^

Kwa uzoefu wako kwanini akili inachukua nafasi zaidi kuliko moyo??
 
Kwamba huna uhakika kama huyu ndiye Mungu aliyekupa au la? mara nyingi maswali ya kujiuliza yanatawala sana kipindi hiki

Mkuu sio kila mtu huweka sala na dua zake kwa Mungu kwa habari ya ndoa...

Wapo watu wengine hutamani kuoa/kuolewa kwa matamanio ya fikra zao pekee, na wana vigezo vyao ambavyo huvitizama...

Ndio maana nikaandika kuwa kuna sababu tofauti tofauti ziletazo uzito kulingana na watu tofauti...
 
Mwenza sahihi utamjuaje?AMANI YA MOYO HUSEMA KILA KITU.Utapata amani ya ajabu juu ya hilo.Sio tu ktk kuoa au kuolewa ni ktk mambo yoote.Ukiona mashaka hofu ujue jambo lako halitakua jema mbeleni.
 
Back
Top Bottom