Unakabiliana vipi na mmomonyoko wa maadili dhidi ya mwanao?

mr vata

JF-Expert Member
Jan 30, 2017
465
616
Jamani...
Pamoja nami, poleni sana kwa mvua zinazoendelea kutiririka kwa fujo hapa nchni. Pia niwape pole za pekee wale wote wanaoishi mabondeni.

HUSIKA NA KICHWA CHA HABARI HAPO JUU...
Suala hili linatuhusu sana sisi tunaoishi uswahilini...
Jamani uswahilini kuna mmomonyoko mkubwa sana wa maadili, lugha chafu, suala la wazazi kuwatukana watoto wao matusi makubwa makubwa na mengine mengi tu kama hayo.
Binafsi bado sijawa na familia. Nakuuliza mwenzangu ambae una familia (watoto) na unaishi uswahilini.
Unakabilina vipi na mmomonyoko wa maadili dhidi ya watoto/mtoto wako?
 
Mimi binafsi namuongoza mtoto katika maadili mema na bora...Namfundisha katika njia zilizo bora na zinazoipendeza jamii. Akikosea namkanya kwa kumpa adhabu zinazoendana na kosa na kumshauri asirudie tena kwa kumpa njia zilizo sahihi..Namfundisha utu, uadilifu, heshima,uaminifu na mambo mengine ili asipotee katika malezi.

Kusema ukweli kuishi mtaani na kulea watoto inahitaji moyo sana kwa maana ukizubaa tu mtoto anakengeuka na kuanza tabia zisizoipendeza jamii.. Ni jukumu la Baba, Mama na jamii nzima kwa ujumla kuwapa malezi bora na kuwafundisha katika mienendo ifaayo na kuepuka njia mbaya.
 
Namtanguliza Mungu ili anifanye kuwa mfano bora kwa njia atakayopita mwanangu. Malezi yahitaji msaada wa Mungu ili mtoto apokee tabia njema yenye kufaa kwenye jamii!
 
Namtanguliza Mungu ili anifanye kuwa mfano bora kwa njia atakayopita mwanangu. Malezi yahitaji msaada wa Mungu ili mtoto apokee tabia njema yenye kufaa kwenye jamii!
 
Back
Top Bottom