KWA muda mrefu nimekuwa nikipata maswali kutoka wadau na wengine wakieleza matatizo waliyonayo katika uhusiano na wapenzi wao. Kati yao, wapo ambao wanateswa na jambo dogo sana; ni dogo lakini linawashinda kiasi sasa limekuwa kubwa!
Msamaha. Katika uhusiano ni vyema kukubali kwamba, mwenzako si mkamilifu na anaweza kukosea, hivyo ana wajibu wa kuomba msamaha lakini pia nawe unapaswa kupokea msamaha wa mwenzako hasa kama ameomba kwa dhati. Ukiacha kusamehe na kubaki na kinyongo, utabaki na maumivu makali moyoni mwako.
Ni maumivu hayo ndiyo yatakayoweza kusababisha matatizo mengine katika uhusiano wako. Kubali kusamehe, omba msamaha kwa mwenzako, mara nyingi inavyowezekana ili uhusiano wenu uendelee kuwa wenye amani. Acha kuweka vinyongo moyoni mwako.
Ahsanteni sana. Naamini dondoo imeeleweka vizuri.
- Joseph Shaluwa.