Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,201
- 233
Kwa sasa hivi sio ajabu kabisa kwenda katika kampuni yenye watu zaidi ya 60 mfano ukakuta wanatumia programu ambazo hazina leseni , ambazo zina crack na vitu kama hivyo .
Wakurugenzi wa kampuni hizi sijui kama wanajua madhara yake kwa kuruhusu hizo programu kutumika pale , hata sijui walimu wa vyuo wanafundisha nini wanafunzi wao haswa wale technician na administrator wa baadaye kuhusu vitu hivi .
Ni kawaida kabisa kukuta administrator ameacha system yake iwekwe programu hizi na zitumike bila wasi wasi na tatizo lolote , shida ikitokea si anaformat tu ? kwanza hata installation cd anazotumia sio licenced yeye anashida gani ??
Wakati Fulani rafiki yangu mmoja aliwahi kuniomba programu Fulani kwa ajili ya kazi zake , nikamwambia ninayo lakini yangu ina leseni ambayo ni kwa ajili ya mtu mmoja au computer moja tu .
Akaniuliza siwezi kumkopia au siwezi kumtafutia programu kama hiyo hiyo ya bure ambayo ni cracked ( iliyofanyiwa usanii ili ifanye kazi ) nikamwambia huo ni uhalifu siwezi kufanya hivyo , akaniuliza kama kuna tovuti yoyote wanazotoa serial number au crack au keygen zake .
Unaweza kuchanganyikiwa kidogo ninavyotaja crack , keygen na serial number na licence key hivi ni vitu tofauti .
Crack Ni aina ya njia haramu ya kuifanya programu Fulani ifanye kazi , lakini programu hiyo inakuwa haina baadhi ya vitu na ni ngumu sana kujua labda likitokea tatizo Fulani , ila mara nyingi crack huwa na virus ndani yake na spyware .
Keygen Hii ni programu inayotumika kutengeneza serial number katika programu husika , mfano programu nyingi za adobe zina keygen au nero 7 ina keygen au Autocad , maana yake ukisha install inabidi kufungua keygen ili ugenerate serial number kwa ajili ya programu yako .
Serial Number Hizi ni namba maalumu unazotakiwa uingize katika programu yako ili ihalalishwe katika matumizi yako ya kawaida , sasa Keygen inaweza kugenerate hiyo serial number .
Licence Key hizi nazo ni namba pia lakini mara nyingi hizi licence key unatakiwa uimport katika programu yako ili iweze kufanya kazi na hizi zinatumika zaidi katika programu kama za Autocad 2008 na kuendelea .
Hayo ni maelezo mafupi kuhusu baadhi ya mambo muhimu ambayo ni muhimu kujua unapokutana na vitu kama hivi .
1 Programu nyingi ambazo ni cracked zinakuwa na virus katika baadhi ya file zake kwahiyo haitafanya kazi ipasavyo ingawa sio zote .
2 zingine zinakulazimisha usijiunga na internet ukifanya hivyo wenye programu ni rahisi kuifunga au kukutambua kwamba unatumia kitu haramu na kuzifungia mfano wake ni Microsoft Windows Xp na Windows Vista .
3 Ni rahisi kushambuliwa kwa njia ya mtandao kama unatumia Antivirus au Firewall ambazo ni cracked kwa sababu baadhi ya vitenda kazi vinaweza kuwa havifanyi kazi au vimezimwa ingawa sio zote .
4 Kama unatumia programu za uhasibu , au mahesabu ni rahisi kupoteza data , au kuchanganya baadhi ya mahesabu kutokana na hivi yaani programu kutokufanya kile inachotakiwa kutokana na mapungufu wakati wa cracking .
5 Kwa programu kama Adobe Acrobat Profesianal 6 na kuendelea , ukitumia crack hizi , unapojaribu kugeuza Kitu toka Word kwenda Pdf au PDF kwenda Word , baadhi ya maandishi yanaweza kupotea au kutokea madhara mengine yoyote katika Document husika .
6 Ni rahisi kuforge vitu vilivyotengenezwa kwa kutumia programu hizi kwa sababu zinakuwa hazina protection ya kutosha au protection hizi hazifanyi kazi zikiwekwa.
Hayo ni baadhi ya madhara tu ingawa kuna madhara mengi na mambo mengi unayoweza kukumbana nayo unapotumia programu ambazo sio halali .
Nakushauri usitependee sana kutumia programu ambazo sio halali kwa sababu madhara yake ni ya muda mrefu , unaweza kuharibu data za watu huko makazini , au unaweza kusababisha madhara yoyote yale yatakayoleta hasara katika jamii yako unayofanya nayo kazi .
Kama unanunua programu ambazo si halali na ukafurahia wakati unajua sio halali na ni makosa , basi hata mafisadi usiwalalamikie , unasababisha hasara kwa watu waliowekeza katika kutengeneza programu husika ,utambue na wao wanatakiwa kuishi na kudhaminiwa kutokana na ujuzi wao wa kukuletea programu hiyo husika .
Mwisho kabisa programu nyingi zinakuwa na kitu kinaitwa Terms Of Use , Disclaimer na Fair Use , kwahiyo unatakiwa uwe makini sana unavyojaribu ku install hizi programu , soma ujue kampuni husika inasema nini kuhusu bidhaa yake hiyo .
Ingawa sheria nyingi zinazotumika ni za marekani na nchi zingine za ulaya sio kwamba Huwezi kushitakiwa unavyotumia kinyume chake , kwa sababu kuna sheria za kimataifa zinazoweza kutumika kuku hukumu .