Unajua kwanini watu wanahama upinzani saa hii?

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,813
18,549
1. Wana njaa kali wanatafuta pa kujishibisha

2. Wamekosa ukomavu wa kisiasa, wanafikiri upinzani ni lele mama

3. Wanafikiri upinzani hauna cha kusema angali hata Marekani/Uingereza/Ufaransa upinzani una mambo kibao ya kukosoa serikali

4. Ndoto zao za kunyakua madaraka na vyeo zimefifia

5. Hawana uvumilivu wala mipango ya kisiasa ya muda mrefu

6. Wamezoea shamra shamra, zikikosekana watazitafuta popote kwingineko

7. Wamezoea kusimama penye umati mkubwa na kushangiliwa

8. Wana ufinyu mkubwa wa mawazo

9. Hawana mrengo/itikadi imara ya kisiasa, kila siasa inayovuma inawapeperusha

10. Wanatafuta nafasi za uongozi ndani ya chama tawala wakikosa watakwenda kwingine

11. Ni wabinafsi wakubwa, hawasimami kwa ajili ya manufaa ya wananchi bali matumbo yao

12. Wamefanya siasa kuwa ajira binafsi kama kulima mpunga, shamba hili likichoka wanahamia shamba jingine na kutelekeza la kwanza

13. Ni matapeli wa kisiasa

14. Hawapo tayari kuwatumikia wananchi katika wakati mgumu

15. Wanategemea siasa pekee kupata fedha, watu hawa ni hatari kwa nchi
 
Hata aibu hawana. Wanadhani sisi wananchi ni mazezeta. Ubinafsi umewajaa nyoyoni mwao.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Sasa mtu anaacha ubunge huyo ananjaaa?
hayo yote uliyoorodhesha ni kama umekuwa upande mmoja.

1. Wanahamia ccm kwakuwa kuna kitu wanataka kule na sio kwa mapenzi ya wao kuwa ccm, ila Mh rais anaelewa zaidi kuliko wao wanavyoelewa. watajifanya wanamsifia rais ila rais keshaelewa kila kitu.
Mfano sisi tulimpigia Rais Magufuli kura kwa moyo wetu wote, nilikuwa siipendi ccm ila nilikuwa nampenda Mh Magufuli. nikampa kura yangu. na akasema tusibomolewe maana tulimpa kura. sasa hawa wanaojidai kumsifia sasaivi ili wapewe nini?
Au kuna malali walivinja sharia ( walijenga kwa mianya ????? ) wanaogopa kubomolewa? sikuzote walikuwa wapi wasimkubali Mh Magufuli?

2. unajua ukiingia ccm sema kilichokupeleka huko mfano mm nilikuwa naichukia ccm kipindi cha utawala wa Fulani ila kwa utawala wako ccm imekuwa na sifa nzuri na ninaipenda. na sio kusema oooh niemrudi ccm kwakuwa huku nilipokuwa kazi yao ni kukuponda na mm nakusifia sasa nakosa pa kukusifia naamua kuja huku. mmmmmh
 
Wengine wanatishwa au wana biashara zao sio halali au hawajalipa kodi muda kama huyo anayejiita wakili msomi aliyekuwa act wazalendo ametishiwa kulipuliwa
 
Back
Top Bottom