Unajua kwamba Dr Slaa ameongoza kwa kura nyingi Iringa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unajua kwamba Dr Slaa ameongoza kwa kura nyingi Iringa?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Abraham Lincon, Nov 4, 2010.

 1. A

  Abraham Lincon Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unapomsikia mpendwa wetu mheshimiwa Dr Slaa akilalamika juu ya wizi (uchakachuaji) wa kura ambao CCM imefanya dhidi ya chama chetu kitukufu unaweza ukadhani ni mtu anayetapatapa baada ya kufanya vibaya katika uchaguzi mkuu wa Tanzania 2010.

  Kusema ukweli hali haiko hivyo na **** pekee yake anayeweza amini kwamba mheshimiwa Dr. Slaa ameshindwa! Hii inatokana na jinsi Mheshimiwa Dr. Slaa anavyopendwa na watanzania hasa kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa kwa nchi yetu ndani na nje ya Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania. Leo hii nikiwa Internet Cafe moja hapa Iringa, waliingia vijana wa kiume wawili (wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma).

  Binafsi siwafahamu watu hawa na wala sikuwa na mawazo yoyote ya kuwafahamu kwani nilikuwa bize na shughuli zangu. Baada ya kupewa muda wa kutumia Internet katika Cafe hiyo, wanafunzi wale wali "play" video ya Mheshimiwa Dr. Slaa akitoa hotuba katikak moja ya mikutano yake ya campaign" kisha maongezi yakaanza. Katika maongezi yao walikuwa wakim"discuss" mheshimiwa Dr Slaa na uchakachuaji wa matokeo ya kura ambazo watanzania wenye mtazamo wa mabadiliko chanya walimpigia Dr. Slaa ili awe rais wetu.

  Katika maongezi yao, nilikuja gundua kuwa vijana wale walikuwa moja kati ya wasimamizi wengi wa vituo vya kupigia kura katika uchaguzi mkuu 2010 wa hapa nchini. Walisimulia waziwazi kwamba katika mkoa wa Iringa Dr. Slaa pamoja na wagombea wa nafasi ya Ubunge na udiwani walikuwa wakiongoza lakini jambo la kushangaza matokeo yaliyotangazwa na tume yamekuwa tofauti. Binafsi ninaona uchumgu mkubwa sana juu ya wizi wa kura unaofanywa na CCM. Watanzania lazima tujiulize, ni kitu gani kinachowafanya CCM kung'ang'ania Ikulu kiasi kile wakati uwezo wa kutuletea mabadiliko hawana? kuna biashara gani pale?

  Ninasikitika sana na wala sitaki kuamini kwamba baada ya Nyerere kufariki hakuna viongozi wengine wenye uchungu na nchi hii isipokuwa wachache kama Dr Slaa. Viongozi wa tume wameonesha mapungufu makubwa sana kiasi cha kunifanya niwadharau kwani wameonesha kukosa hekima na busara kabisa. Wamejaa uchu wa madaraka na ubinafsi wa kutupwa kiasi cha kushindwa kujali wananchi walio wengi kwa kuwapendelea wachache.

  Laana ya wananchi wanyonge hakika na iwe juu yao. Ninamuomba Dr Slaa asikate tamaa kwani watanzania wapenda mabadiliko tupo pamoja naye.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mkuu, habari yako yaweza kuwa nzuri, lakini jinsi ulivyoiweka haiko 'reader-friendly!...no paragraphs and other panctuational errors!
  Rekebisha broda!
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Tutatafuta haki yetu tu hata kwa ncha ya upanga.
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,906
  Trophy Points: 280
  hali kama hii nina uhakika imetokea kwenye majombo mengi tu
   
 5. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  "Leo hii nikiwa Internet Cafe moja hapa Iringa, waliingia vijana wa kiume wawili (wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma). Binafsi siwafahamu watu hawa na wala sikuwa na mawazo yoyote ya kuwafahamu kwani nilikuwa bize na shughuli zangu." Sasa hapo mkuu uliwajuaje kama ni wanafunzi wa chuo kikuu cha dodoma? Uliongea nao wakadhibitisha kwa wao ni wanafunzi? Clarify please
   
 6. M

  MSAUZI JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 228
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tetetehhh...Majombo?..Majombo ni viatu wanavaa kule makaa ya mawe
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,906
  Trophy Points: 280
  i mean majimbo!!! typing error bro!!
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  ukitukana kidogo hasira zinapungua puuuuuuu$$#%#% zenu!
   
 9. A

  Abraham Lincon Member

  #9
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sikuwa na haja ya kuwauliza kwani walikuja kwa aja ya kuangalia matokeo yao kupitia website ya chuo chao. Kwa bahati nzuri walikuwa wakiongea kwa sauti ya juu iliyonifanya niwasikie na kutambua uanafunzi wao ktk chuo hicho. Sitegemei utaniuliza wanafunzi wa UDOM walikuwa wakifanya nini Iringa!
   
 10. A

  Abraham Lincon Member

  #10
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante! Nitafanya hivyo. I was in a hurry.
   
 11. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Ina maana tovuti ya chuo kikuu cha dodoma inaripoti matokeo ya uchaguzi? Au ulikuwa una maana matokeo yao ya mitihani?
   
 12. A

  Abraham Lincon Member

  #12
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maana yangu ilikuwa ni matokeo ya mitihani yao waliyofanya kabla ya kufunga chuo.
   
 13. Chizi Fureshi

  Chizi Fureshi JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,710
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Unge-report kwa sura ya jimbo la Geita na Nyang'wale ingenoga sana! Sasa hiiiiiiiiiiii, aaah. :nono:
   
 14. Chizi Fureshi

  Chizi Fureshi JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,710
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Uzi huu ungeuleta kama yalivyo-reportiwa matatizo ya jimbo la Geita na Nyang'wale ingenoga sana. Lakini kwa sura hiiiii, aaah.:nono:
   
 15. A

  Abraham Lincon Member

  #15
  Nov 5, 2010
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli, lakini lengo langu ni kufikisha taarifa ya tukio kama nilivyoshuhudia na si kunogesha story. Ahsante kwa ushauri hata hivyo.
   
Loading...