Elections 2010 Unajua kwamba Dr Slaa ameongoza kwa kura nyingi Iringa?

Oct 22, 2010
78
0
Unapomsikia mpendwa wetu mheshimiwa Dr Slaa akilalamika juu ya wizi (uchakachuaji) wa kura ambao CCM imefanya dhidi ya chama chetu kitukufu unaweza ukadhani ni mtu anayetapatapa baada ya kufanya vibaya katika uchaguzi mkuu wa Tanzania 2010.

Kusema ukweli hali haiko hivyo na juha pekee yake anayeweza amini kwamba mheshimiwa Dr. Slaa ameshindwa! Hii inatokana na jinsi Mheshimiwa Dr. Slaa anavyopendwa na watanzania hasa kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa kwa nchi yetu ndani na nje ya Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania. Leo hii nikiwa Internet Cafe moja hapa Iringa, waliingia vijana wa kiume wawili (wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma).

Binafsi siwafahamu watu hawa na wala sikuwa na mawazo yoyote ya kuwafahamu kwani nilikuwa bize na shughuli zangu. Baada ya kupewa muda wa kutumia Internet katika Cafe hiyo, wanafunzi wale wali "play" video ya Mheshimiwa Dr. Slaa akitoa hotuba katikak moja ya mikutano yake ya campaign" kisha maongezi yakaanza. Katika maongezi yao walikuwa wakim"discuss" mheshimiwa Dr Slaa na uchakachuaji wa matokeo ya kura ambazo watanzania wenye mtazamo wa mabadiliko chanya walimpigia Dr. Slaa ili awe rais wetu.

Katika maongezi yao, nilikuja gundua kuwa vijana wale walikuwa moja kati ya wasimamizi wengi wa vituo vya kupigia kura katika uchaguzi mkuu 2010 wa hapa nchini. Walisimulia waziwazi kwamba katika mkoa wa Iringa Dr. Slaa pamoja na wagombea wa nafasi ya Ubunge na udiwani walikuwa wakiongoza lakini jambo la kushangaza matokeo yaliyotangazwa na tume yamekuwa tofauti. Binafsi ninaona uchumgu mkubwa sana juu ya wizi wa kura unaofanywa na CCM. Watanzania lazima tujiulize, ni kitu gani kinachowafanya CCM kung'ang'ania Ikulu kiasi kile wakati uwezo wa kutuletea mabadiliko hawana? kuna biashara gani pale?

Ninasikitika sana na wala sitaki kuamini kwamba baada ya Nyerere kufariki hakuna viongozi wengine wenye uchungu na nchi hii isipokuwa wachache kama Dr Slaa. Viongozi wa tume wameonesha mapungufu makubwa sana kiasi cha kunifanya niwadharau kwani wameonesha kukosa hekima na busara kabisa. Wamejaa uchu wa madaraka na ubinafsi wa kutupwa kiasi cha kushindwa kujali wananchi walio wengi kwa kuwapendelea wachache.

Laana ya wananchi wanyonge hakika na iwe juu yao. Ninamuomba Dr Slaa asikate tamaa kwani watanzania wapenda mabadiliko tupo pamoja naye.
 
Mkuu, habari yako yaweza kuwa nzuri, lakini jinsi ulivyoiweka haiko 'reader-friendly!...no paragraphs and other panctuational errors!
Rekebisha broda!
 
Unapomsikia mpendwa wetu mheshimiwa Dr Slaa akilalamika juu ya wizi (uchakachuaji) wa kura ambao CCM imefanya dhidi ya chama chetu kitukufu unaweza ukadhani ni mtu anayetapatapa baada ya kufanya vibaya katika uchaguzi mkuu wa Tanzania 2010. Kusema ukweli hali haiko hivyo na juha pekee yake anayeweza amini kwamba mheshimiwa Dr. Slaa ameshindwa! Hii inatokana na jinsi Mheshimiwa Dr. Slaa anavyopendwa na watanzania hasa kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa kwa nchi yetu ndani na nje ya Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania. Leo hii nikiwa Internet Cafe moja hapa Iringa, waliingia vijana wa kiume wawili (wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma). Binafsi siwafahamu watu hawa na wala sikuwa na mawazo yoyote ya kuwafahamu kwani nilikuwa bize na shughuli zangu. Baada ya kupewa muda wa kutumia Internet katika Cafe hiyo, wanafunzi wale wali "play" video ya Mheshimiwa Dr. Slaa akitoa hotuba katikak moja ya mikutano yake ya campaign" kisha maongezi yakaanza. Katika maongezi yao walikuwa wakim"discuss" mheshimiwa Dr Slaa na uchakachuaji wa matokeo ya kura ambazo watanzania wenye mtazamo wa mabadiliko chanya walimpigia Dr. Slaa ili awe rais wetu. Katika maongezi yao, nilikuja gundua kuwa vijana wale walikuwa moja kati ya wasimamizi wengi wa vituo vya kupigia kura katika uchaguzi mkuu 2010 wa hapa nchini. Walisimulia waziwazi kwamba katika mkoa wa Iringa Dr. Slaa pamoja na wagombea wa nafasi ya Ubunge na udiwani walikuwa wakiongoza lakini jambo la kushangaza matokeo yaliyotangazwa na tume yamekuwa tofauti. Binafsi ninaona uchumgu mkubwa sana juu ya wizi wa kura unaofanywa na CCM. Watanzania lazima tujiulize, ni kitu gani kinachowafanya CCM kung'ang'ania Ikulu kiasi kile wakati uwezo wa kutuletea mabadiliko hawana? kuna biashara gani pale? Ninasikitika sana na wala sitaki kuamini kwamba baada ya Nyerere kufariki hakuna viongozi wengine wenye uchungu na nchi hii isipokuwa wachache kama Dr Slaa. Viongozi wa tume wameonesha mapungufu makubwa sana kiasi cha kunifanya niwadharau kwani wameonesha kukosa hekima na busara kabisa. Wamejaa uchu wa madaraka na ubinafsi wa kutupwa kiasi cha kushindwa kujali wananchi walio wengi kwa kuwapendelea wachache. Laana ya wananchi wanyonge hakika na iwe juu yao. Ninamuomba Dr Slaa asikate tamaa kwani watanzania wapenda mabadiliko tupo pamoja naye.

"Leo hii nikiwa Internet Cafe moja hapa Iringa, waliingia vijana wa kiume wawili (wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma). Binafsi siwafahamu watu hawa na wala sikuwa na mawazo yoyote ya kuwafahamu kwani nilikuwa bize na shughuli zangu." Sasa hapo mkuu uliwajuaje kama ni wanafunzi wa chuo kikuu cha dodoma? Uliongea nao wakadhibitisha kwa wao ni wanafunzi? Clarify please
 
"Leo hii nikiwa Internet Cafe moja hapa Iringa, waliingia vijana wa kiume wawili (wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma). Binafsi siwafahamu watu hawa na wala sikuwa na mawazo yoyote ya kuwafahamu kwani nilikuwa bize na shughuli zangu." Sasa hapo mkuu uliwajuaje kama ni wanafunzi wa chuo kikuu cha dodoma? Uliongea nao wakadhibitisha kwa wao ni wanafunzi? Clarify please

Sikuwa na haja ya kuwauliza kwani walikuja kwa aja ya kuangalia matokeo yao kupitia website ya chuo chao. Kwa bahati nzuri walikuwa wakiongea kwa sauti ya juu iliyonifanya niwasikie na kutambua uanafunzi wao ktk chuo hicho. Sitegemei utaniuliza wanafunzi wa UDOM walikuwa wakifanya nini Iringa!
 
Sikuwa na haja ya kuwauliza kwani walikuja kwa aja ya kuangalia matokeo yao kupitia website ya chuo chao. Kwa bahati nzuri walikuwa wakiongea kwa sauti ya juu iliyonifanya niwasikie na kutambua uanafunzi wao ktk chuo hicho. Sitegemei utaniuliza wanafunzi wa UDOM walikuwa wakifanya nini Iringa!

Ina maana tovuti ya chuo kikuu cha dodoma inaripoti matokeo ya uchaguzi? Au ulikuwa una maana matokeo yao ya mitihani?
 
Unge-report kwa sura ya jimbo la Geita na Nyang'wale ingenoga sana! Sasa hiiiiiiiiiiii, aaah. :nono:
 
Uzi huu ungeuleta kama yalivyo-reportiwa matatizo ya jimbo la Geita na Nyang'wale ingenoga sana. Lakini kwa sura hiiiii, aaah.:nono:
 
Uzi huu ungeuleta kama yalivyo-reportiwa matatizo ya jimbo la Geita na Nyang'wale ingenoga sana. Lakini kwa sura hiiiii, aaah.:nono:

Ni kweli, lakini lengo langu ni kufikisha taarifa ya tukio kama nilivyoshuhudia na si kunogesha story. Ahsante kwa ushauri hata hivyo.
 
Back
Top Bottom