Unajua faida ya juisi ya ndimu

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,219
6,650
Umesikia mara nyingi kuwa kunywa maji kwa wingi hasa asubuhi kuna faida kubwa sana za kiafya mwilini,lakini kunywa maji yenye ndimu na vuguvugu kuna faida maradufu na ni rahisi kufanya kila siku. Vitamin C nyingi iliyomo katika ndimu (au limao) ni siri ya faida za tunda hili,ukiachia vitamini C ndimu ina vitamini B-complex, madini ya Kalsiamu, chuma, magnesiamu na potasiumu, na fiba (Ndimu ina potasiumu kwa wingi kuliko tofaa (apple au Zabibu).

Tunajua kwa watu wengi Kunywa maji peke yake (yasiyo na kitu) wakati wa asubuhi hupata tabu na baadhi ya wengine hupata kichefuchefu . Lakini maji yaliyotiwa ndimu kidogo huwa na radha nzuri zaidi na watu wote wanaweza kunywa bila shida.

Faida kubwa ya juisi ya ndimu ni kinga dhidi ya malaria. Kamau glasi moja ya ndimu asubuhi na mapema kabla ya kupiga mswaki na kuinywa. Hakika utakuwa umejijengea kinga dhidi ya malaria.

Kisha kila siku asubuhi, kabla ya mswaki uwe na tabia ya kunywa angalau glasi moja ya maji ya uvuguvugu yenye ndimu. Kuna faida nyingi ambazo utazipata kwa kunywa maji yenye ndimu au limao. Baadhi ya faida hizo ni kama ifuatavyo:

1) Huchochea Mmeng’enyo Wa Chakula Tumboni: Maji yenye ndimu husaidia chakula kusagika vizuri na haraka katika mfumo wa chakula. Japo limao lina asidi(acid) lakini likiwa tumboni huwa alkali (alkaline) na kufanya mazingira mazuri kwa usagaji wa chakula. Kumbuka kwamba maji ya uvuguvugu husaidia kusawazisha utumbo uliojikunja na kutoa mawimbi tumboni na kufanya chakula kusukumwa vizuri.

2) Huboresha Kinga Za Mwili: Vitamini C na potasiumu iliyomo kwa wingi katika limao inasaidia katika utengenezaji wa seli za kinga katika mwili.

3) Husaidia Unyonywaji Wa Madini Mwilini: Vitamini C iliyomo katika limao husaidia kunyonywa kwa madini mwilini hasa madini ya chuma ambayo ni muhimu kwa utengenezaji wa damu. Hata kama maji ya ndimu yakiwa baridi.

4) Husaidia Kinga Dhidi Ya Saratani: Vitamini C ni 'antioxidant' ambayo inasaidia kuondoa uchafu na sumu za madawa mwilini ambazo zimebainika kusababisha saratani (cancer).

5) Husaidia Kupunguza Hatari Ya Kiharusi: Kutokana na matokeo ya kitafiti ulaji wa matunda jamii ya ndimu/limao (citrus fruits) unasaidia kupunguza hatari ya kupatwa na shambulio la kiharusi aina ya 'ischemic stroke' hasa kwa wanawake na wale wanaokula kula chumvi nyingi.

6) Usafishaji Wa Mwili Na Damu: Ndimu/Limao husaidia kusafisha damu kwa kuondoa uchafu. Limao pia husafisha figo, ini na mfumo wa chakula.

7) Kurekebisha Sukari Katika Mwili: Ndimu hasa Limao husaidia kuweka kiasi cha sukari tumboni na katika mwili kuwa katika kiasi stahili. Hii inawasaidia sana wagonjwa wa kisukari katika ulaji wao.

8) Dawa Ya Kikohozi Na Mafua: Ndimu/limao likitiwa katika maji ya uvuguvugu na asali husaidia sana katika kutibu mafua na kikohozi kwa njia ya asili.

9) Inasaidia Urekebishaji Wa Ngozi Na Kupona Makovu: Ndimu/Limao inasaidia kufanya ngozi isizeeke. Kama unataka kubaki kijana basi ndimu/limao litakusaidia. Hii ni kwa sababu Tabia za vitamin C za kusafisha uchafu zinasababisha kufanya ngozi kuwa na afya na kutozeeka haraka.

10) Husaidia Kupungua Uzito: hupunguza hamu ya kula. Na inajulikana kuwa sababu kubwa ya watu kuwa na uzito mkubwa ni kula chakula kingi au kula mara kwa mara. Limao litakufanya ujisikie kushiba muda mrefu hivyo kusaidia wale amabao wanataka kupungua uzito.

11) Kuondoa Harufu Ya Mdomo: Ndimu/Limao husaidia kuua bakteria wabaya mdomoni ambao husababisha harufu mbaya.

Anza Siku Kwa Kunywa Maji Ya Uvuguvugu Yenye Ndimu Kila Siku. Ni zoezi rahisi na haraka kabisa, weka maji yenye joto kidogo (vuguvugu) katika glasi au kikombe, kata ndimu/limao vipande viwili na kamua kipande kimoja tu ndani ya glasi yenye maji.

Kunywa na uanze siku mpya. Ni vizuri ukafanya hivi dakika 30 kabla ya kula chochote kingine kwa faida zaidi.

Anza leo kwa kunywa maji yenye ndimu kila siku asubuhi na uone mabadiliko ndani ya mwili wako. Mshirikishe mwenzio ili naye afaidike.

KUPANGA NI KUCHAGUA

Imetolewa kwa hisani ya mitandao
 
sasa kwa ss vimbaumbau hatuhusu maan hailet hamu ya kula sasa hilo nalo c tatizo aisee
 
sasa kwa ss vimbaumbau hatuhusu maan hailet hamu ya kula sasa hilo nalo c tatizo aisee
Matumizi hayahusu umbile la mtu ila afya bora. Unene siyo kigezo cha afya bora yaweza ikawa ugonjwa pia
 
Back
Top Bottom