Unajua Computer inafayaje kazi?

Msamiati

R I P
Joined
Mar 6, 2011
Posts
1,063
Reaction score
700
Hoja yako inaonesha kuwa unatakakufahamu jinsi ambavyo mifumo ya computer inafanya kazi. Sitakupamaelezo ya kitaalamu sana lakini nitajitahidi angalau ufahamu hivi vitu vinafanyaje kazi.

Mfumo wa mawasiliano wa Kidigitali(Digital Communication).

Jambo kubwa na La kuzingatia tunapozungumzia mfumo wa mawasiliano wa kidigitali, nikwamba mafanikio ya mfumo huu yamekuwa yakifocus kwenye mawasiliano baina yacomputa na vifaa vingine na si computer na binadamu..

Mafanikio ya mfumo wa mawasiliano wakidigitali yalichagizwa zaidi na madhumuni makubwa mawili.

Usafirishaji wa taarifa(Data Transimition).

Lengo la kuwa na njia rahisi zaidi yakusafirisha taarifa ni moja kati ya vyanzo vikubwa kabisa vilivyochukua nafasi kubwa sana kwenye mafanikio ya mfumo wamawasiliano wa kidigitali.

Historia zinaonesha kuwa kwa karne nakarne sasa watu mbali mbali walikuwa wakiwekeza kwenye utafiti nauvumbuzi wa technolojia itakayokuwa bora zaidi kwenye usafirishaji wa taarifa kutoka chanzo kimoja mpaka sehemu nyingine. Mfano rahisi kabisa wa pointi hii ni jinsi unavyoweza kusafirisha nyimbo kutoka kwenye simu moja kwenda simu nyingine au simu za mkononi zinavyo safirisha sauti kutoka simu moja hadi nyingine.

Kurahisisha Matumizi ya vifaa vingi kutoka kwenye chanzo kimoja(Nodes Usability).

Kabla ya mafanikio makubwa kwenye teknolojia hii, zoezi la kutumia vifaa zaidi ya kimoja kutoka mahali pale pale alipokuwa mtumiaji lilikuwa mtihani mkubwa na pengine lisilowezekana kabisa. Ili kuongeza urahisi wa matumizi(Usability) na mapinduzi kwenye soko viwanda mbali mbali vinavyohusika na uzalishaji wa mashine za ofisini na majumbani vililazimika kuwekeza zaidi kwenye mfumo wa mawasiliano wakidigitali.

Hii ni kwa dhumuni la kumuwezesha mtu mfano abadilishe stesheni ya television bila kusimama mahali alipo,apige alam ya gari akiwa ofisini kwake, atumie printa ya ofisini bila kunyanyuka kwenye kiti chake au akiwa nyumbani kwake kabisa namatumizi mengine mengi makubwa zaidi.

Kufikia Hapa Nataka utambue kuwa vifaavinawasiliana, wakati mwingine binadamu hutumia kifaa kimojakuwasiliana na kifaa kingine (Nodes Communications). Hii ndio elimuya kawaida kabisa ambayo sio vibaya kila mtu akawa nayo juuya Mfumo wa mawasiliano wa Kidigitali.


Sasa leo nimalizie kwa swali moja tu! Vifaa hivyo vinawasiliana vipi!?


Katika kusafirishataarifa kutoka kifaa kimoja kwenda kifaa kingine, kanuni ni ileile inayotumika kusafirisha mpunga kutoka kyela kwenda Dar es Salaam. Lazima kuwe na basi, Barabara mahari mzigo unapotoka na kule unakokwenda. Bila kusahau uwepo wa taarifa kwa pande zote mbili kuwa ni mzigo gani ambao unasafirishwa, uzito wa mzigo na vigezo vyausalama.

Aina ya Taarifa (Mzigo) . Data Type

Gari linaweza kusafirisha aina mbalimbali za mizigo, leo mchele kesho mahindi na safari nyingine kitu chatofauti zaidi. Lakini kwenye mifumo ya komputer hii ni tofauti kidogo. Mzigo unaosafirishwa umelazimika kuwa na sifa na vigezo vya aina moja (standard) ili kuwezesha vifaa vyote vinavyotumia mfumo wakomputer viweze kuwasiliana na kubadilishana taarifa bila shida. Hii ndiyo sifa inayowezesha komputer iweze kuwasiliana na computer nyingine lakini pia iwe na uwezo wa kuwasiliana na simu, printa nakifaa kingine chochote kinachotunia mfumo wa komputer.


Unataka kujua Standad hiyo Ni Ipi ?

nb: Hii sio technical review nimezungumza kutokana na uzoefu wa ufatiliaji na usomaji wa vitabu mbali mbali. nakaribisha maswali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ