Unajivunia nini kuwa Mtanzania?

Nilifedheheshwa na CNN kuelezea swala la ushirikina wa waTz. Swala la wenye ulemavu wa ngozi kuuwawa nalo linatia aibu sana.
 
Ndiyo hvyo sasa.......tunavyo tu kama mapambano ila wananufaika navyo wengine.
Ni kweli kuna vitu vimegunduliwa mfano Uranium na Helium lakini hakuna anayejua vinaenda wapi, vimekuwa ni mapambo tu.
 
Naona aibu barabara kujaa mchanga.......naona aibu posta tunapishana na vinyesi vikielea.
 
Naona Aibu

- Madini ya Almas, Tanzanite na Dhahabu kutaja chache kwamba yanapatikana Tanzania lkn kuyanufaishi nchi wala hakuna taarifa za kutosha kuhusu uvunaji wa madini hayo.

- Kwamba Tanzania ina rasimali nyingi lakini ndio nchi yenye umaskini wa kukudhiri.

NAJIVUNIA

- Wananchi kupanga mipango kwa mdomo hawajambo ila utekelezaji hakuna.

- najivunia kila jambo tunakichukulia kisiasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…