Kukataliwa kunatokana na sababu nyingi; mtu anaweza kuwa anakupenda lakini hakuamini kuwa unampenda kweli sababu ameshaumizwa sana, anaweza kuwa hakupendi na haoni sababu ya kuremba and so anakupa makavu, anaweza kuwa na mpenzi, anaweza kuwa anaumwa HIV anaogopa kukuambukiza, Na mengine mengi anayojua yeye tu.
Kwa kifupi kukubali au kukataa ni hiyari yake mtongozwaji, huwezi kucontrol maamuzi yake unapomtongoza. Kuumia unapokataliwa ni swala la kawaida, labda umezee/ ujidanganye au uvunge ila kuumia kiasi cha kuanza kufanya mambo ya ovyo bila kujicontrol, ni dalili ya tatizo na unapaswa kutafuta msaada.