Unajisikiaje mwenzi wako akihusudu usivyonavyo?

Unajisikiaje mwenzi wako akihusudu usivyonavyo?

Hornet

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Posts
26,892
Reaction score
52,491
Nimewaza tu.

Muda mwingine unakuta mwanaume anahusudu vitu usivyokuwa navyo kwa mfano hips, Makalio makubwa ya kubinuka, Maziwa na vinginevyo.

Yaani gallery yake inajaa picha na videos za warembo halafu ukijiangalia hauna walivyonavyo. Muda mwingine mkitembea macho hayakauki kwenye migongo ya wadada.

Na kwa upande wa wanawake Mara amsifie Fulani ana six pack ilhal wewe una four pack's! Yaani Mtu anasifia vitu ambavyo hauna na si rahisi kuwa navyo, unamchukuliaje!?
 
Huyo anakua anatafuta sababu ya kuachana. Kwani mpaka anakutongoza au unamtongoza alikua haoni kama wewe huna makalio makubwa ya kubinuka? Wakati anakubali uwe mpenzi wake hakuyaona hayo?
 
Wakati mwingine kwa wanaume wengi wao ile huwa kama burudani kumuangalia mtu kama huyo, haina maana akimsifia anamtaka,
Hata mwanamke aweza msifia mwanaume kua hivi na vile lakini hata itokee akitongozwa na huyo mwanamme hamkubali hata kwa dawa.
 
Back
Top Bottom