Unaifahamu imani ya rastafarian?

MTOTO WA KUKU

JF-Expert Member
May 3, 2012
2,510
2,000
Maana halisi ya neno RASTAFARIAN: ni imani ya mtu mweusi au mweupe inayotetea UTU wa MTU MWEUSI. MPIGANIA HAKI YA MTU MWEUSI huitwa RASTAMAN au RASTAWOMAN na kwa WATOTO wao huitwa RASTABABY.

Imani "kamili" ya Rasta ilianzishwa zaidi ya miaka 100 iliyopita huku kundi kubwa la waafrika waliokuwa mikononi mwa wakoloni walipoweza kuingia kwenye imani hiyo huku nchi ya JAMAICA ikiwa na wafuasi wengi. Dredy locks ni moja kati ya kitambulisho kikubwa cha Rastafarian,,lakini si kila mwenye dredy locks basi akawa Rastafarian kwani asilimia 25 ya Rastafarian hawana Dredy locks na ndipo tunapoona kwamba kufuga dredy si kuwa na imani ya Rasta bali matendo humpeleka mtu kwenye imani ya Rasta. Rastaman hupenda kujiajiri na mara nyingi hufanya shuhguli zake kwa kutumia mikono na si vifaa vya kazi na kati ya kazi za Rasta ni SANAA, wao hufanya aina zote za sanaa lakini kazi zote hizi Rasta hujiajiri na si kuajiriwa.

Moja kati ya nguzo kuu za Rastafari ni UPENDO na AMANI, Rasta hujaribu kutafuta amani popote ipatikanapo, tabia hiyo ya Rasta imewafanya Rasta kuheshimiwa popote pale waingiapo lakini baadhi ya jamii huwa tofauti na imani hii.

Imani ya Rasta chimbuko la asili ni Nimrodi binadamu wa kwanza mweusi na mtawala wa Babeli ya kale, na kutukia kwake kumechipuza kamili nyakati ambapo haki ya mtu mweusi ilipo potea na hatimaye jamii kubwa ya watu weusi kutafuta njia ya kutetea utu huo wa mtu mweusi.

GABRIEL HAIRE SELASIE aliyekuwa kiongozi wa nchi ya Ethiopia ni moja kati ya watu waliochangia kukuza imani ya Rasta ulimwenguni na ndipo jumuiya ya Rastafariani ilipoamua kumteua kuwa kiongozi wa Rastafarian ulimwenguni.

Rasta hutumia muda wa mapumziko kwa kusikiliza burudani ya nyimbo za rege walizo zitunga ambazo nyingi ya nyimbo hizo huwa za kuwapa moyo na kuwafariji watu wanyonge na wanaopuuzwa.

Rege kwangu nisehemu ya Ibada ya kweli ambapo hutumia mziki huo siku za jumamosi kama sehemu ya kuwasiliana na Mungu wangu, Hakika Mungu hunijibu tena LIVE.

Labda nipende kusema kuwa watu wengi wanafikiri kuwa Rastafari ni kuvuta Bangi na kuwa na dreads (Dreads ni muhimu).

Kuwa Rastafari nilazima uishi nakufuata yafuatayo:

1.Fuata sheria za Nazareti katika Bible(Rastafarian Bible).
2.Epuka vyakula najisi kama nguruwe, kambale n.k
3.Epuka intoxicants kama pombe, sigara, kahawa, coca cola na vyakula ambavyo sio natural na vyenye madhara mwilini.
4.Heshimu utamaduni wa Africa na kubali kuwa wanadamu wote asili yetu ni Africa na ndio Zion Yetu
5.MHESHIMU KING OF KINGS, THE LION OF JUDAH, ELECT OF GOD, RAS TAFARI MAKONEN, HAILE SELASSIE, THE POWER OF THE TRINITY, KING MESIAH FROM THE ROOT OF KING DAVID IN A SOLOMONIC LINEAGE.
6.Kuwa msafi, usimuudhi mtu, Heshimu imani za watu, usibague mtu kwa kuangalia imani, kabila wala rangi.
7.Jali Elimu kwa kuwa ndio msingi wa Haile kujikomboa.
8.Heshimu mother nature na usiharibu mazingira.
9.Usiue mnyama wala kumpiga bila sababu.
10.Heshimu dini/imani za watu wengine,
11.Tambua uwepo wa Yesu Kristu na Mtume Mohamed SAW (japo mafundisho yao usiyafue)
12.Epuka kugusa damu wala kunywa damu.
13.Heshimu Bendera ya Empire ya Ethipia na Rasta colour, usivae ovyo kama urembo,
14.Jali equality, kuwa natural na epuka vitu vya kemikali n.k
15.Tafari Makomein (Gabriel Haile Selassie) ni God incarnate.

Pengine hili swala la kumwabudu Haile Selassie limebaki kwa " Root Rastafarians" yaani mimi na wale walio devote maisha yao yote katika namna ya asili ya Rastafari.

Maisha yanabadilika halikadhalika mawazo na mitazamo pia.

Rastafari sasa inaonekana kuwa kama lifestyle na pengine ni jambo jema. Kuwa Rastafari kama Kebra(Rastafari Holy Book) inavyosema ni kuwa na namna ya maisha yaliyo nyofu.

Hii inatia ndani; upendo, heshima, na amani. Kwa Rastas tunasema " don't haffi dreadlocks to be rasta, a Rastaman is a conception of the heart"

Kaya ni "sakramenti" kwa maana ya kwamba inatumiwa wakati wa worshipping kwa dhumuni la ku "calm yourself" na kutafuta oneness na muumba "Jah".

Ikumbukwe kwamba, Rastafari sio organized religion lakini ni imani yenye tumaini tofauti na inabeba mafundisho mengi ya bible hasa old testament.

Hauitaji kuacha kazi, dini yako, mke wako/mume au umkane mtu fulani ili uwe rasta. Kuwa rasta ni kuishi maisha bora kama nilivyo taja hapo huu.

Mpende mzazi wako, jali utu wa mwanadamu na viumbe vingine hapo utakuwa Rastafari kwa matendo. Kuhusu ku "smoke Kaya" ni uamuzi japo wengi tunatumia.

Kuwa rastafari ni very hard, inabidi uwe makini na ukubali kupata chalenges nyingi za maisha na watu kukuhukumu kwa kukuangalia na wengine kukuona mjinga. Ila ni raha sana kwa kuwa utaishi maisha ya furaha bila kujali what they think.

BLESSINGS! Over!
 
Attachments

  • 1400923716818.jpg
    File size
    72.6 KB
    Views
    213

lumanyisa

JF-Expert Member
Oct 2, 2012
884
500
rastafarians the followers of ras tafari makonen.napenda utamaduni huu kwa sababu ya amani na heshima waliyonayo.hata wasiokuwa rastafarians ila wana dreadlocks wana aina flani ya utu ambao jamii nyingi huikosa.wanaamini juu ya elimu mno na kuendelea.nasikia haile Selassie kabla hajafa alimwambia mengistu juu ya ukame na njaa kubwa na ikatokea kweli 10 years later.tafari alikuwa mtu poa sana
 
G'taxi

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,387
2,000
Maana halisi ya neno RASTAFARIAN: ni imani ya mtu mweusi au mweupe inayotetea UTU wa MTU MWEUSI. MPIGANIA HAKI YA MTU MWEUSI huitwa RASTAMAN au RASTAWOMAN na kwa WATOTO wao huitwa RASTABABY.

Imani "kamili" ya Rasta ilianzishwa zaidi ya miaka 100 iliyopita huku kundi kubwa la waafrika waliokuwa mikononi mwa wakoloni walipoweza kuingia kwenye imani hiyo huku nchi ya JAMAICA ikiwa na wafuasi wengi. Dredy locks ni moja kati ya kitambulisho kikubwa cha Rastafarian,,lakini si kila mwenye dredy locks basi akawa Rastafarian kwani asilimia 25 ya Rastafarian hawana Dredy locks na ndipo tunapoona kwamba kufuga dredy si kuwa na imani ya Rasta bali matendo humpeleka mtu kwenye imani ya Rasta. Rastaman hupenda kujiajiri na mara nyingi hufanya shuhguli zake kwa kutumia mikono na si vifaa vya kazi na kati ya kazi za Rasta ni SANAA, wao hufanya aina zote za sanaa lakini kazi zote hizi Rasta hujiajiri na si kuajiriwa.

Moja kati ya nguzo kuu za Rastafari ni UPENDO na AMANI, Rasta hujaribu kutafuta amani popote ipatikanapo, tabia hiyo ya Rasta imewafanya Rasta kuheshimiwa popote pale waingiapo lakini baadhi ya jamii huwa tofauti na imani hii.

Imani ya Rasta chimbuko la asili ni Nimrodi binadamu wa kwanza mweusi na mtawala wa Babeli ya kale, na kutukia kwake kumechipuza kamili nyakati ambapo haki ya mtu mweusi ilipo potea na hatimaye jamii kubwa ya watu weusi kutafuta njia ya kutetea utu huo wa mtu mweusi.

GABRIEL HAIRE SELASIE aliyekuwa kiongozi wa nchi ya Ethiopia ni moja kati ya watu waliochangia kukuza imani ya Rasta ulimwenguni na ndipo jumuiya ya Rastafariani ilipoamua kumteua kuwa kiongozi wa Rastafarian ulimwenguni.

Rasta hutumia muda wa mapumziko kwa kusikiliza burudani ya nyimbo za rege walizo zitunga ambazo nyingi ya nyimbo hizo huwa za kuwapa moyo na kuwafariji watu wanyonge na wanaopuuzwa.

Rege kwangu nisehemu ya Ibada ya kweli ambapo hutumia mziki huo siku za jumamosi kama sehemu ya kuwasiliana na Mungu wangu, Hakika Mungu hunijibu tena LIVE.

Labda nipende kusema kuwa watu wengi wanafikiri kuwa Rastafari ni kuvuta Bangi na kuwa na dreads (Dreads ni muhimu).

Kuwa Rastafari nilazima uishi nakufuata yafuatayo:

1.Fuata sheria za Nazareti katika Bible(Rastafarian Bible).
2.Epuka vyakula najisi kama nguruwe, kambale n.k
3.Epuka intoxicants kama pombe, sigara, kahawa, coca cola na vyakula ambavyo sio natural na vyenye madhara mwilini.
4.Heshimu utamaduni wa Africa na kubali kuwa wanadamu wote asili yetu ni Africa na ndio Zion Yetu
5.MHESHIMU KING OF KINGS, THE LION OF JUDAH, ELECT OF GOD, RAS TAFARI MAKONEN, HAILE SELASSIE, THE POWER OF THE TRINITY, KING MESIAH FROM THE ROOT OF KING DAVID IN A SOLOMONIC LINEAGE.
6.Kuwa msafi, usimuudhi mtu, Heshimu imani za watu, usibague mtu kwa kuangalia imani, kabila wala rangi.
7.Jali Elimu kwa kuwa ndio msingi wa Haile kujikomboa.
8.Heshimu mother nature na usiharibu mazingira.
9.Usiue mnyama wala kumpiga bila sababu.
10.Heshimu dini/imani za watu wengine,
11.Tambua uwepo wa Yesu Kristu na Mtume Mohamed SAW (japo mafundisho yao usiyafue)
12.Epuka kugusa damu wala kunywa damu.
13.Heshimu Bendera ya Empire ya Ethipia na Rasta colour, usivae ovyo kama urembo,
14.Jali equality, kuwa natural na epuka vitu vya kemikali n.k
15.Tafari Makomein (Gabriel Haile Selassie) ni God incarnate.

Pengine hili swala la kumwabudu Haile Selassie limebaki kwa " Root Rastafarians" yaani mimi na wale walio devote maisha yao yote katika namna ya asili ya Rastafari.

Maisha yanabadilika halikadhalika mawazo na mitazamo pia.

Rastafari sasa inaonekana kuwa kama lifestyle na pengine ni jambo jema. Kuwa Rastafari kama Kebra(Rastafari Holy Book) inavyosema ni kuwa na namna ya maisha yaliyo nyofu.

Hii inatia ndani; upendo, heshima, na amani. Kwa Rastas tunasema " don't haffi dreadlocks to be rasta, a Rastaman is a conception of the heart"

Kaya ni "sakramenti" kwa maana ya kwamba inatumiwa wakati wa worshipping kwa dhumuni la ku "calm yourself" na kutafuta oneness na muumba "Jah".

Ikumbukwe kwamba, Rastafari sio organized religion lakini ni imani yenye tumaini tofauti na inabeba mafundisho mengi ya bible hasa old testament.

Hauitaji kuacha kazi, dini yako, mke wako/mume au umkane mtu fulani ili uwe rasta. Kuwa rasta ni kuishi maisha bora kama nilivyo taja hapo huu.

Mpende mzazi wako, jali utu wa mwanadamu na viumbe vingine hapo utakuwa Rastafari kwa matendo. Kuhusu ku "smoke Kaya" ni uamuzi japo wengi tunatumia.

Kuwa rastafari ni very hard, inabidi uwe makini na ukubali kupata chalenges nyingi za maisha na watu kukuhukumu kwa kukuangalia na wengine kukuona mjinga. Ila ni raha sana kwa kuwa utaishi maisha ya furaha bila kujali what they think.

BLESSINGS! Over!
HIS IMPERIAL MAJESTY EMPEROL HAILE SELASSIE I
 
kethika

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
632
500
EE MUNGU WETU KATIKA JINA LA YESU NAKUOMBA UMFUNGUE HUYU NDUGU NA WEBGINE WA AINA YA IMANI YAKE. KWANI ULISEMA YESU KRISTO NDIYE NJIA KWELI NA UZIMA HAKUNA MTU ATAKAYEFIKA ULIKO WEWE ISIPOKUWA KWA KUPITIA KWA YESU KRISTO.
JAMBO MOJA
HATUMOANGII MUNGU CHA KUFANYA ILA YEYE NDIYE ANAYETUPANGIA CHA KUFANYA.
NA KUWA NA IMANI POTOVU JUU YA MUNGU HAKUBADILISHI IMANI YA KWELI JUU YA MUNGU.
SO NI MUHIMU KWA UNYENYEKEVU MKUBWA KUOMBA REHEMA NA NEENA YA MUNGU ILI ATUFUNULIE ILE IMANI SAHIHI NA HALISI JUU YAKE.
 
Rastafarian inaamini uwepo ya YESU kristo.haipingi,usidhani kuifikili nje ya box la ukristo ni dhambi,dhambi ni kutenda yanayomchukiza MUNGU hasa kutokutii zile amri zake 10 alizotupa,na hasa UPENDO,usijidanganye mtu mwenye imani ya rasta ni mdhambi,ila kama atatenda maovu ndo atakua mdhambi,ni sawa na mkristo au muislam,mchungaji,kasisi,muumini,lakini wakawa wafitini,wazinzi,walevi n.k.hao wote ni watenda dhambi,ukimhukumu mtu Rastafarian ni umejidanganya mwenyewe.hata MUNGU asingewahi kuikubali sadaka ya Kornelio maana hakua na dini wala mahala pa kuabudu ila alikua na imani ya kua MUNGU yupo na anaweza kumjibu maombi yake kupitia sadaka zake alizokua anazitoa mtaani kwa masikini na wahitaji kama wafanyavyo Rastafarian.fikili nje ya box na usiache imani yako
 
Kama nilielewa vizuri katika moja ya masharti ya hawa rasta ni kukubali kuwa Yesu yupo ila kutofuata mafundisho yake. Hapa ndio kuna tatizo. Hata mimi nakubali kuwa shetani yupo ila kitendo cha mimi kukataa mafundisho yake kunaoondoa any credibility yake kwangu haijalishi ninakubali kiasi gani kuwa yupo.

Si ukiwaza nje ya box hata kama sio sahihi ni sawa?

Mimi siwahukumu raster ila nimewapa maelekezo hayo ninayoamini mimi kuwa ni sahihi.

Ukweli kuwa Mungu anawasaidia au anawajibu wakiomba sio ticket kuwa anawakubali. Huyo Kornelio uliyemtolea mfano kama Mungu angekuwa anakubaliana na upagani wake asingemtuma Petro aende akamuongoze juu ya njia iliyo sahihi.

Mungu kukuacha unapotenda dhambi haimaanishi kuwa amekubaliana na wewe ila anakuacha ili yumkini kuna siku utakubali kugeuzwa moyo wako kumfuata yeye.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom