Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,097
Umekuwa katika mahusiano naye kwa muda mrefu hivyo bila shaka unamjua vilivyo! Pengine mpo ndani ya ndoa kabisa au mahusiano tu ambayo mnaishi pamoja kwa ukaribu sana.
Sasa kwa kawaida lazima kuna machale yanakucheza pale unapoona kama humsomi flani hivi. Usipuuze.. Fuatilia tu utabaini ukweli..
Kuna mambo ambayo mwanzo yalikuwa hayapo ila yameanza kujitokeza.. Unahisi kabisa hapa lazima kuna mtu anamchanganya ila ushahidi huna unaishia kuugulia tu.. Kuna mambo unayaona na yanakutia shaka ila bado unashindwa kujua kama ni kweli au hisia zako tu.
Sasa mimi naamini kuna mambo ukiyaona yanaingiliana na haya hapa chini basi ni salama zaidi kusema goma limechacha!
Ukaribu
Mtu wako akianza kupunguza ukaribu au kuongeza ukaribu sana na wewe usifurahie, ni dalili mbaya hiyo. Kwa sababu kama anachepuka, aidha atakuwa hana time kabisa na wewe au atakuwa na mzuka zaidi na wewe hasa kwenye 'kupigana miti'.
Mfano kwenye sex hapo utamkuta analeta style mpya ambazo hukuwahi kuziona.. Kajifunzia wapi? Tuchukulie ni kwenye runinga au story za vijiweni au siyo!?
Simu
Ushazoea kuwa huru na simu yake lakini siku hizi inakuwa kama inahifadhi nyara za serikali. Hugusi! Pengine kipindi cha nyuma alikuwa huru kupokea simu mbele yako ila siku hizi ikiita tu anaenda room nyingine au anatoka nje kabisa.. Na kuchati kunapitiliza! Hii nayo ni sababu ya wazi sana.
Kupendeza
Siku hizi jamaa ako au mkeo anajali sana mitupio. Kama ilikuwa anaoga ile kawaida tu na kuvaa kawaida aah siku hizi anachange. Habanduki kwenye kioo... Kama ni kidume kila mara ataenda saloon kujiweka fresh nywele, ndevu. Nguo lazima ahakikishe katoklezea ndio anatoka..
Kama alikuwa anaongelea vibaya gym utakuta ghafla ameanza kupenda kwenda kujiweka fiti kiume... Tena na ratiba maalum.. Gari kila mara linapelekwa kuupigwa sopu sopu na kwa wale wa gettho/apartment basi inakuwa safiiii muda wote tofuti na zamani..
Kazini
Ushazoea kumsikia akilalamikia masuala ya kazi kwamba zinamboa na anatamani kumaliza arudi home kupumzika, lakini siku hizi ndio panamnogea hatari.. Atakuambia kuna team yake mpya siku hizi inachangamsha sana.. Kazi zimekuwa nyingi blah blah..
Ngoja tu niishie hapo lakini kwa kweli ukiona dalili za aina hiyo (najua zipo nyingi) ujue hapo tena mambo sio mazuri sana..
Jitahidi kurudisha penzi kwenye reli!