unahitaji wazo la biashara ? soma hapa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

unahitaji wazo la biashara ? soma hapa.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Red Giant, Mar 15, 2012.

 1. Red Giant

  Red Giant JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 9,511
  Likes Received: 6,014
  Trophy Points: 280
  wadau napenda kuliona hili jukwaa la watu wanaopeana mbinu za kutatua matatizo na sio walalamishi, hivyo basi kama unawazo jipya la biashara liweke hapa au modify waliyoweka wengine.
  Naanza mimi: ningekuwa na mtaji au kwa watu wenye mtaji naona kujenga vyoo kwenye barabara kuu sehemu ambazo watu huwa wanachimba dawa unaweza kuwa mradi mzuri, ni kwamba kila abiria kwenye gari analipia kama tsh mia mbili hivi kwa magari ya abiria na watu binafsi. Nahisi ni biashara ya uhakika sababu watu hawapendi kujisaidia wazi kama wanyama pia ni aibu wageni kutoka nje kuondoka na picha eti watanzania wanajisaidia hovyo. mwana jamii irekebishe hii au to wazo lako jipya hasa lisilo hitaji mtaji mkubwa.
   
 2. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu RG, yaan hili bado ni wazo! Au umeshaanza kulifanyia kazi? Hapo kwenye red sio tatizo sana, kwani mtaji mkubwa zaidi ni kichwa chako. Kwan utahitaji kiasi gani kuongea na serikali ya kijiji ili wa kupatie eneo kwenye hayo maeneo watu wanayochimba dawa?

  Kumbuka unaweza ukaanza kujenga choo kwa rasilimali zinazopatikana pale pale. Kikubwa zaidi ni usafi. Kitu kingine cha msingi, ni by laws (ambazo ni lazima zitungwe na serikali ya kijiji) ili kuwadhibiti watu watakaokuwa wanachafua mazingira baada ya uwepo wa hizo huduma za choo.

  Ukitaka utekelezaji uwe mzuri na rahisi, ifanye iwe SOCIAL ENTERPRISE, na ushirikiane na kijiji husika. Kwa kufanya hivi ardi utapata bure (kama machango wa kijiji). Ukiweza kutengeneza proposal nzuri, unaweza ukapata wadhamini, kwani mradi huu ni suala mtambuka na taasisi nyingi zina interest huko kwenye mambo ya sanitation

  All the best
   
 3. Red Giant

  Red Giant JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 9,511
  Likes Received: 6,014
  Trophy Points: 280
  hilo bado ni wazo sijatake even a single step, halafu kuifanya social interprise ni wazo ambalo nililifikiria pia, maeneo yale watu huwa wanauza na snacks kwa hiyo mnakuwa mnawezeshana kwa kuboresha mazingira ya biashara, hivi NEMC hawawezi kuhusika hapo?
   
 4. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  NEMC hawawezi kuwa kikwazo kwenye mradi mdogo kama huu. Go for it, mkuu
  Anza kwa kuainisha maeneo husika watu wanayopenda kuchimba dawa kienyeji? Kisha fanya utafiti kuhusu suala la umiliki na uangalie ni eneo lipi litakuwa muafaka kwako kwa kuanzia
   
 5. H

  Haika JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mie napenda sana kuwa na biashara yangu.
  Tatizo nahisi kuwa nakuwa na vibes za negativity wakati wote.
  naona vikwazo kuliko opportinities.
  Mfano tu kwa mradi huu hapa naona kama itakuwa capital kubwa sana kusafiri hadi sehemu utakayoweka ofisi mara kwa mara kuisimamia. Ukijua kuwa Tanzania hii, biashara bila kuisimamia mwenyewe, ni kumuanzishia huyo mfanyakazi.
  Naombeni msaada nitoke huku gizani
   
 6. Red Giant

  Red Giant JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 9,511
  Likes Received: 6,014
  Trophy Points: 280
  ukiona mawazo hasi yanakuja anza kufikiria njia anazoweza kuepuka au kusolve hizo challenges usiache vikwazo ndio viwe mwisho wako. mfano kuhusu kusafiri unaweza kupanga labda mara moja kwa mwezi labda iwe imejensi halafu biashara yenyewe sidhani kama inataka uangalizi mwingi, kama unaogopa kuibiwa mwanzoni unafanya research ujue kwa siku unaweza kuingiza tsh ngapi halafu unamwambia mfanyakazi upate daily report ya mapato na matumizi hapo huwezi ibiwa.
  jamani wenye mawazo huko lets share!
   
 7. L

  LAT JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu

  wazo zuri, siku hizi kuna style nyingi za ku-manage biashara ambapo lazima uwe na controlling tools za uhakika,

  ningekushauri ufanye built and outsource operations, jenga vyoo, weka standards zako za usafi na ada ya matumizi, tafuta mtu au kikundi cha watu mbalimbali, wape waendeshe hivyo vyoo kwa kuwapangia hesabu ya siku baada ya kuwa umeshaestablish kiasi cha mapato kwa siku kwa kufanya pilot study ya collections, hata wafanya usafi outsource, pesa yako iingie kwenye m-pesa kila siku, kama utakuwa na vituo katika njia za kaskazini, kati na kusini unaweza ukafanikiwa vizuri

  assume njia ya kaskazini ina mabasi zaidi ya 40 yanayofanya safari kila siku

  assume watakao tumia huduma hiyo ni 70% ya basi lenye abiria 60 - 42 passengers per day

  42 x TZS 300 per person = 12,600

  12,600 x 40 buses = 504,000

  ukiwa na vituo 5 vyenye choo njia zote kubwa - 504,000 x 5 = 2,520,000 per day

  weka mabasi madogo na magari madogo mengine katika vituo hivyo vyote yaingize 300,000 per day

  total = TZS 2,820,000

  chukua 40% ya kipato chote = TZS 1,128,000 per day

  oooppppps, too good to be true

  hebu na wadau wengine watoe mawazo yao

  have a good day
   
 8. kwelwa

  kwelwa Member

  #8
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kinachoonekana kwako ni kuthubutu.ebu thubutu kuingia,usiogope
   
 9. Red Giant

  Red Giant JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 9,511
  Likes Received: 6,014
  Trophy Points: 280
   
 10. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu, kuwa na biashara, haimaanishi ni lazima uisimamie mwenyewe (yaan uwe owner manager). Pitia huo ushauri wa LAT hapo juu uongeze uelewa kwenye masuala ya outsourcing. Au labda jiulize halmashauri nyingi zinaendesha vipi vitegauchumi vyake? (Swali hili "Mbona kiasi cha mapato wanachokubaliana na hao waendeshaji kwa mwezi ni kidogo?" linahitaji mjadala mwingine)

  Na hapo kwenye RED, usijishangae sana kwani haupo peke yako, huu ni ugonjwa mkubwa kwenye sehemu pana ya Jamii zetu. I bet it has something to do with Emotional Intelligence (chanzo chake ni nini? huu ni mjadala mwingine) lakin tiba yake ya kwanza (kwa mujibu wa mimi) ni kutafuta ukombozi wa kifikra kwa kujisomea vitabu (inspirational novels) tofauti tofauti (lakin hasa vinavyohusiana na mambo ya ujasiriamali na biashara)

  Unaweza ukaanza na hiki ingawa hakihusiani na ujasiriamali, "HOW TO CONQUER NEGATIVE EMOTIONS" by Roy Masters
   
 11. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #11
  Mar 15, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu, namna ulivyo break down hii kitu, mpaka inavutia, (lakini ungemalizia na ceteris peribus ingekaa vizuri zaidi). Sasa kazi ipo kwa RG. Inaonekana hata payback period ya huu mradi haiwezi kuwa ni zaidi ya miaka miwili

  1,128,000 x 30
  = ?
  Ooh my God, are we talking about 33,840,000/= Tsh? (40% of Monthly income)
  Wako wapi wataalamu wa ujenzi, waje watupe BOQ?
   
 12. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Umeniibia wazo langu wewe,nimewaza hchi kitu miaka lakini huwa nasema watajenga 2 siku moja especially kutoka moshi kwenda dar,
   
 13. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Haa haa haa, unapaswa kujisifia kwa kutambua OPPORTUNITY (kwan kwa wengine ni kazi sana). Halafu kufanana mawazo si tatizo, tatizo liko hapo kwenye namna ya kuyaweka haya mawazo kwenye vitendo (UNIQUENESS). By the way mbona wewe hukulitekeleza hili kwa kipindi chote hicho? Au changamoto ndio ile ile anayosema RG? (Capital)

  Hivi Mamzalendo kwenye hii Barabara (Dar- Arusha), ni sehemu gani watu wanapochimba Dawa kienyeji? Mbona Pale Msata (kwenye mizani) nimeona hii huduma? Halafu barabara hii inahoteli nyingi sana njiani, hivyo ni rahisi kupata hizi huduma (mfano Highway Hotel)
   
 14. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  my friend suala ni capital lakini pia hiyo ardhi,nilianza kuwaza jambo hili kuna siku nilimeza dawa jamani nilitamani kuwamaliza wa2 wa kmanjaro bus ni siku hyo oh hatusimami hadi highway,majina sitaweza kujua kwa usahihi mpendwa ila kwa kweli ukitoka moshi hadi highway halafu highway dar haifai,hotel zipo lakini hawasimami mkuu,labda vikijengwa hivi vitu itakuwa sio ombi tena kusimama na viwe katika umbali maalumu,
   
 15. Red Giant

  Red Giant JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 9,511
  Likes Received: 6,014
  Trophy Points: 280
  ma mzalendo ukiona inafaa changamkia faster kaongee na wadau,siku tukitaka kujiingiza tunakukukuta umejaa full tutatafuta kitu kingine na hili linchi tutakuwa tunalisogeza mdogomdogo. vipi haukuwa na wazo lingine?
   
 16. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #16
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hujaibiwa wazo lako,business ideas ni zile zile ambazo huwa tunaweza kila siku gap ipo kwenye implementation hapo huwa tunatofautiana.
   
 17. G

  GenX Member

  #17
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wazo zuri sana RG. Nafikiri inabidi ulifanyie kazi hata kama huna mtaji kwa sasa hivi. Unaweza kuanza kuandika Master Plan ya business nzima wakati huu. Survey maeneo ambayo unaweza weka biashara katika route tofauti, jinsi ambavyo biashara itaendesheshwa, n.k. Kuhusu wafanyakazi, unaweza ukatafuta mtu mwenye kiwanja karibu na barabara mkakubaliana profit sharing kwa yeye kukupa kiwanja ujenge halafu yeye awe msimamizi.

  Still there's so many way this can be done. Keep up!
   
 18. s

  sawabho JF-Expert Member

  #18
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Wazo zuri, weka katika vitendo niliona Namibia njia ya Windhoek - Wavis Bay, halikuhusisha huduma ya Msalani tu, bali hata uchafu mwingine.
   
 19. i

  iMind JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,908
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Chalenji ya biashara hii ni maji. Ili kumaintain usafi na ubora, lazima kuwe na maji ya kutosha. Solution yaweza kuwa kuchimba kisima kirefu, kuweka pump, tank na generators.
   
Loading...