Unahitaji Logo? Ingia hapa

Izzi

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
553
1,107
Watu, salamu kutoka Azma Africa. Uzi huu ni mahsusi kwa yeyote anaehitaji Logo na anaamini tunaweza kufanya nae kazi. Zifuatazo ni hatua ambazo kwa kawaida huwa tunazifuata mpaka kukamilisha zoezi la kutengeneza Logo ya mteja, karibu.

Hatua ya kwanza: Utatupa maelezo ya namna unavyotaka/unavyopenda/unavofikiri logo yako iwe.
Hatua ya pili: Tutakubaliana bei kulingana na kazi ilivyo, kisha utafanya malipo - aidha nusu ya bei (Ni lazima) au malipo yote.
Hatua ya tatu: Tutatengeneza na kukutumia concepts 3 ili uzipitie na kuchagua moja kati ya hizo, au unaweza kupendekeza muunganiko wa concept 2, au ukaona kuna kitu kinakuvutia kwenye concept moja unataka kihamie kwenye concept nyingine n.k.
Hatua ya nne: Ukishachagua concept mojawapo, tutafanya marekebisho yote yatayotakiwa na utakayopendekeza. Hatua hii itahusisha mawasiliano endelevu - 'back n' forth'. Hapa pia tutajadili vitu kadhaa ikiwemo aina ya maandishi, rangi, n.k.
Hatua ya tano: Ukiridhika na muonekano wa mwisho wa Logo, tunaandaa package yenye;

☆ Logo variations zote zinazotakiwa (Mara nyingi ni nne: Vertical, Horizontal, Brandmark & Wordmark)​
☆ Color variation zote kadiri inavyofaa (Mara nyingi ni nne: Full, Inverse, Black & White)​
☆ File Formats zinazotakiwa i.e Vector na Image.​
Vector inajumuisha; Ai, SVG, EPS, na Editable PDF. Image ni; PNG, na JPEG.​
☆ Logo package guide (Maelekezo ya namna ya kutumia vilivyomo katika package)​

Hatua ya sita: Kama ulilipia nusu, unamalizia malipo kisha tunakutumia package yako kwa njia ya email. Pia tunaipakia kwenye G-Drive ambapo tutashare link na wewe na package hiyo tutaitunza kwenye G-Drive kwa kipindi cha Mwezi mmoja kabla hatujaifuta.

MUHIMU:
☆ Tunafanya kazi mbalimbali za Digital Designing (Zile ambazo zinaweza kuwa delivered digitally; Maana yake ni kuwa Hatuprint). Kwahiyo kama unatafuta kitu kingine tofauti na logo, tafadhali wewe jisikie huru kutuuliza, na sisi tutafurahi kukupa majibu.
☆ Tunafanya kazi za commision pia i.e kama una mteja ambae amekupa kazi na ungependa tushirikiane kuifanya.

SAMPLE:
☆ Baadhi ya mifano ya kazi zetu tutaziweka hapa.
☆ Baadhi ya kazi zetu zinapatikana kwenye tovuti yetu: www.azmaafrica.com
☆ Unaweza kuona baadhi ya kazi kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii: Instagram, Twitter, Facebook
☆ Ndani ya miezi miwili ijayo tutafungua na kuweka baadhi ya kazi zetu katika tovuti mahsusi mbili: Dribbble na Behance.

MAWASILIANO
Tunapatikana kirahisi sana kwa namna tofauti tofauti;
☆ Whats up?: Bonyeza Hapa
☆ Ofisi: Jengo namba 1(Ofisi za PADECO)
Barabara ya B. Mbeyela,​
Mtaa wa Idundilanga/Chaugingi,​
Njombe Mjini.​
☆ Barua pepe: Bonyeza hapa
☆ Tovuti: www.azmaafrica.com


MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA.

GHARAMA YA LOGO NI SHILINGI NGAPI?
Inaanzia TSh 50,000/=, inaongezeka kulingana na project details kutoka kwa mteja.

NAWEZA KULIPIA KWA NJIA GANI?
Njia tatu: LIPA NAMBA (Ya M-Pesa), M-Pesa, au Benki (NBC).

MALIPO NI KABLA AU BAADA YA KAZI?
Unatakiwa ulipe angalau 50% ya malipo yote kabla kazi ya kusanifu logo yako haijaanza. Lakini mara nyingi tunapenda mteja alipe malipo yote kwanza (Itakupunguzia adha ya makato kwa kufanya malipo mara mbili)

NAWEZA KULIPIA BAADA YA KUZIONA CONCEPTS?
Concept ni sehemu muhimu sana ya mchakato wa kutengeneza logo, hivyo hatutumi concepts kabla ya malipo.

INACHUKUA MUDA GANI KUTENGENEZA LOGO?
Kila kazi ina upekee wake, hivyo hata muda unatofautiana. Lakini kwa uzoefu wetu, mara nyingi (Kwa Logo ambazo hazina mambo mengi) ni ndani ya masaa 24. Kuiweka package mpaka inakamilika inachukua muda pia, na wakati mwingine inatokea kuwa tumepata oda nyingi kwa wakati mmoja. Kwahiyo, inaweza kuchukua hata wiki 2; Kwa mfano kuna Logo za taasisi nyeti ambazo zinahitaji utafiti kwanza kabla ya kuanza kazi ya usanifu, au wakati mwingine mteja yuko slow kutoa mrejesho, au mrejesho unahitaji marekebisho mengi, n.k. - hapo muda utaongezeka accordingly.

Muhimu ni kuwa huwa tunahakikisha tunawasiliana na mteja ipasavyo ili afahamu ni nini kinaendelea.

VIPI KAMA MKINITUMIA CONCEPTS NA NISIZIPENDE?
Waneni husema "Mawazo hasi huleta matokeo hasi". Kwahiyo tafadhali, ondoa hofu juu ya huo uwezekano. Mpaka sasa imetokea mara moja tu ambapo mteja alishindwa kuchagua concept - alizitaka zote 🥴(phew!) hivyo tukashindwa kufika nae muafaka. Kwahiyo, inaweza kutokea pia usizipende concepts zetu; uwe na uhakika tutaboresha mpaka uridhike kwa 100% na tukishindwa tutarudisha pesa yako.

KAZI YANGU MNAIANZA LINI?
Mambo mawili yakitimia; Tukipata maelezo (brief) yako juu ya namna gani unataka logo iwe, na tukiuona muamala 🤑.

NINA LOGO LAKINI NATAKA KUIBORESHE, MNAWEZA?
Tafadhali itume tuione. Kuna mawili; inawezekana kweli inahitaji maboresho au haihitaji maboresho (Kuna logo hazitakiwi kuguswa). Waneni husema "Usitengeneze ambacho hakijaharibika - utaharibu.". Kwahiyo, wewe itume Logo yako kwenda; hello@azmaafrica.com au kwa WhatsApp; +255 756 650 650 na sisi tutakupa mrejesho mapema kadiri itakavyowezekana.

KWANINI MNATUMA LOGO KWA EMAIL TU?
Package ina vitu vingi, na kwa faida ya mteja huwa tunatuma package ikiwa 'zipped' na kama individual files + Link ya folder yake ya kwenye G-Drive. Sisi tunadhani ni vizuri zaidi hivi vitu vikatumwa kwa email. Lakini, hatukatai kumtumia mteja kwa njia zingine pia ilimradi mteja anafahamu faida na hasara za kutumia njia zingine.

MNATUMIA PROGRAM GANI KUDIZAINI LOGO?
Tunatumia Adobe Illustrator tu!

NAHITAJI KUJIFUNZA, MNAWEZA KUNISAIDIA?
Bado hatujamaliza kutengeneza mifumo mizuri ya kufundisha - kwa maana kwamba tupo tunaitengeneza ili tuanze kufundisha. Na tukiwa tayari kufundisha elimu itatolewa kwa njia ya mtandao; ambapo baadhi ya videos zitawekwa kwenye Channel hii ya Azma Africa. Lakini, ikiwa unaishi Njombe na maeneo ya jirani, usisite kuwasiliana nasi tunaweza kukusaidia physically.

--------------------------------

Una swali jingine? Usisite kutuswalika. Una maoni, lawama, ushauri, kejeli, dukuduku, jakamoyo 😝 you know, anything, ambacho ungependa kukiwasilisha kwetu? Mawasiliano yetu hayo hapo juu; karibu sana.

Sisi... tunashukuru 🙏

🤩MACHO KWENYE SKRINI:🤩

SAMPLE #1: Hii ilikuwa ni kazi ya "Commission" (Mawasiliano yalikuwa yanapitia kwa 'middle man'); Mteja yupo jijini Dar es Salaam, ni kampuni ya kuuza nafaka. Hakuwa na idea ya namna logo yake inavyoweza kuwa, kwahiyo alituachia sisi jukumu la kubuni logo "nzuri" kwaajili ya kampuni yake.

Na haya ndizo concepts tulizompa; na kama ilivyo kawaida, mbili aliipenda zaidi moja ambayo aliikubali kama lilivyo pasipo marekebisho yoyote.

*Mbili zilizobaki tunazitafutia wateja 😎

IBN Logo by Azma.png


SAMPLE #2: Hili shindano hata sijui liliishaje, maana tulishiriki lakini hatujui mshindi alikuwa ni nani (Hawakumtangaza). Ndio, ni Vunja Bei. Tuli-submit concept 3 kama kawaida, na hii ni mojawapo. Unaonaje, tungechukua kitita au tuachane na kazi ya kudizaini tufanye mishe zingine?😎

VB Logo by Azma.png



SAMPLE #3: Na ya Jasiri muongoza njia nayo tukashiriki. Hata sijui mshindi alikuwa ni nani, cha msingi ni kwamba sisi Azmanians huwa tunasikiliza sana ule wimbo wa Mrisho Mpoto Ft. THT: Nenda Salama Ruge,... literally.

RM Logo by Azma.png



SAMPLE #4: Logo kwaajili ya kikundi cha vijana wanaotengeneza bidhaa(Vyakula) ambazo ni "Organic".

Bayo Logo by Azma.png



SAMPLE #5: Njombe Innovation Academy (NIA)
NIA Logo by Azma.png


SAMPLE #6: Shindano la TAA, hatujui mshindi ni nani lakini tuliitumia haki yetu ya kushiriki ;)

TAA Logo by Azma.png



SAMPLE #7: Kwa pamoja zinaitwa "Na kadhalika".

Assorted Logo by Azma.png
 
Nahitaji kujifunza vingine kupitia wewe nipo mafunzoni nikimaliza ntakuja tuelekezane mawili matatu
 
tzhosts katika pitapita nimeona uzi wako kuhusu Hosting n.k, nikashawishika kwenda kuona tovuti yako. Hongera kwa kazi nzuri, na bei zinavutia. Lakini kama GFX Designer, no offense, sikuvutiwa na Logo; so, nikatengeneza concept moja ya haraka haraka ambayo nahisi itakufaa; unasemaje? ;)

TZH Logo Proposal by Azma.png
 
tzhosts katika pitapita nimeona uzi wako kuhusu Hosting n.k, nikashawishika kwenda kuona tovuti yako. Hongera kwa kazi nzuri, na bei zinavutia. Lakini kama GFX Designer, no offense, sikuvutiwa na Logo; so, nikatengeneza concept moja ya haraka haraka ambayo nahisi itakufaa; unasemaje? ;)

View attachment 2472546
Nashukuru mkuu.Nikifikia kufanya rebrand nitakucheck mkuu.
 
Back
Top Bottom