Unahisi ushawahi kuhenya juu ya mapenzi?

Unahisi ushawahi kuhenya juu ya mapenzi?

The Hunter

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2010
Posts
1,048
Reaction score
307
Ukimsoma Jacob kwenye Mwanzo 29:27
Utagundua wewe hujawaji teseka juu ya penzi
Msela alimzimikia binamu yake Rachel, akapewa masharti apige mzigo wa kuchunga mbuzi kwa miaka 7 ili ampate,
Hakushirikisha akili yake kufahamu huwezi oa mdogo kabla dada ake hajaolewa so kilichotokea akapigiwa cheusi chekundu akamwoa Leah bila kujua,
Alipostuka siku ya pili yake, kwamba kalambishwa garasa, ikabidi uncle ake amkumbushe mila na Desturi, jamaa akaambiwa apige mzigo tena miaka saba mingine, so jumla 14 years.
Najua wengi wenu mmetokea magorofani, so hamjua adha ya kuchunga mbuzi.
Asikwambie mtu hiyo, kazi ya kuchunga mbuzi full kichefuchefu.
Unaweza kuwa Filbert Bayi bila kupenda.
Jua lako vumbi lako. Mapenzi ni uvumilivu na subira, unae mpenda na kumtendea mema leo anaweza asione lakini ipo siku atakukumbuka na kukupa credits unazo stahili, usisite kuteseka hata kuumiza mtima wako kwa yule umpendae kwa dhati.
 
Adha ya kuchunga mbuzi ni noma bora uchunge ng'ombe 1000 ila sio mbuzi 20!! Mbuzi wasumbufu wanapenda kukimbia tu yaani mbuzi anaweza kukufanya uwe kichaa!! Anyway nimefurahi kusoma andiko katika lugha ya vijana!!
 
Ndugu, Una maanisha nini kwa hubiri lako ?
 
Hahahahaa chezea mbuzi wew,kwahiyo unamaanisha hata kama umegundua mpenzi wako anatoka nje uvumilie tu eti kwakuwa atakuja kujua umuhimu wako baadaye wkt tayar ushauvaa!
 
mahubiri ya skuhzi!! Duh! Unaitwa nabii nan tena? Hahahahaha
 
. . .mi nimewahi!
Niligeuzwa punda nikatenda mema kuzidi uwezo wangu.
 
Daaah kuchunga mbuzi ni balaa nakumbuka hiyo kazi iliifanya nijue vichaka vyote na mashamba yote kijijini kwetu maana mbuzi wana ka pepo fulani hivi ka kukimbilia kula mazao ya shambani sasa ukijisahau kidogo tu wote hawapo yaani Mbuzi ni Nomaaaa.
 
umenikumbusha adha ya kuchunga ng'ombe niliyokua naipata kipindi flani nyumbani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom