Unahisi ni kwanini kuna mfumuko mkubwa wa shahada ya kwanza?

bomouwa

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
1,149
798
Habari wanajamvi?

Katika miaka ya 70,80 na mwanzoni mwa 90 watanzania wachache saaana walibahatika kupata fursa za kielimu katika nyanja chache chache lakini muhimu.

Kupanua wigo wa uelewa katika mfumo wa elimu rasmi ni jambo jema sana,ingawa sina takwimu (ninakubali kusahihishwa),katika miaka nilioitaja hapo juu, ngazi a kuanzia stashahada zilikua chache sana,shahada ya kwanza halikadhalika na ukienda mbele kwangazi ya shahada ya uzamili na uzamivu ndo chaaaaaaaache balaaa.
Sasa mimi najiuliza!kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 2000 kumekua na mfumuko wa shahada ya kwanza kupita maelezo na kufikia 2007 kumekua na muendelezo wa shahada za uzamili nyingii mnoo lakini katika miaka ya 2012-sasa PhD zimepatikana nyingi kwa vijana.
Najiuliza
1.Kupatikana kwa shahada hizi ni kwamba mwamko wa elimu Tanzania umekua?
2.Fursa za elimu zimekua pana?
3.Shahada za elimu ya juu Tanzania ni bei rahisi?
4.Hawa wataalamu wanaopata shahada hizi je wako competent?
5.Inawezekana mfumo mzima wa usimamizi katika elimu ya juu umepwaya?
Karibuni tujadili,maana naona kijana anamasters anamiaka 25 lakini ni hewaa kabisa au ana Bsc lakini unamuinterview yaani unajiuliza kawezaje kugraduate..
Ieleweke sinashida na kupata PhD katika umri mdogo lakini kwanini miaka ya zamani ilikua ngumu tofauti na sasa?
Nawasilisha
 
vitabu vyenyewe wanavyosoma ni vya nyambali nyangwine halafu utegemee akili hapo.
 
Mifumo ya elimu imexhange, population imeongezeka, maadili kupungua hivyo rushwa za dydyu au pesa zimetawala
 
Ni kukidhi matwaka tu lkn hakuna shule inayosomwa indetails kwa ajili kufunza zaidi ni kupata cheti ktk means yoyote.
 
Ubora wa elimu umeshuka miaka ya 1985 mtu kupata division one form 4 and 6 was not an east task.
Sasa hivi mitaala imerahisishwa, kuna internet kwenye simu mtoto anaweza kubrowse internet akasoma nusu ya syllabus bila kitabu.
Mitihani ya siku hizi ni rahisi sana
 
Nadhani vyuo vimekuwa vingi ukilinganisha na zamani.Kipindi cha nyuma vyuo vikuu vilikuwa viwili tu kama sikosei,siku hizi vyuo viko vingi kama utitiri hadi mfano hapa Arusha kuna Kenyatta University,Arusha University,Mt Meru University,IAA,OUT............... bado kuna matawi ya vyuo.Miaka ya 80s mkaazi wa Arusha ukitaka kupiga degree ilikulazimisha kwenda Dar au Morogoro.Hali hii pia imejitokeza katika mikoa mingine mfano Dodoma Kuna Udom,chuo cha Mipango,CBE.........
 
Number one is definitely true. Watu wengi hasa wasichana wamepata fursa na nafasi za kusoma kuliko zamani
 
Wingi wa fursa za elimu kwa ss vyuo vimekua ving sana krb kila mkoa ss kutakua na chuo kinachotoa shahada ya kwanza

Watu wengi kuwekeza ktk elimu (education as inverstment) na kuona km mkomboz wa ugumu wa maisha
 
serikali ilifungua wigo wa vyuo vikuu vingi baada ya kuona chuo kikongwe kama UDSM taaluma imeporomoka sana
 
Kwa 90% ya watanzania tunapiga shule kwa ajili ya matatizo ya kifedha.
Unaweza ukamkuta mtu anasoma Master halafu haelewi anataka awe nani.
Kwa mfano wewe umesoma uhasibu na fedha, umechukua CPA(T), halafu unarudi ukasome tena MSc.Finance, Baadaye usome tena DR.
Hivi unataka uwe nani???
Kwa sababu me nadhani ulipopata CPA(T) ilitosha kabisa wewe kukaa chini na kuangalia unataka ufike wapi??
Tanzania tunapoteza muda sana ktk elimu, I am very sorry for any inconvenience.
 
Back
Top Bottom