Unafuta Vyuo Vikuu kwa kuutafuta Ubora upi?

Unafuta Vyuo Vikuu kwa kuutafuta Ubora upi?

MAKA Jr

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2016
Posts
267
Reaction score
209
Serikali inaendelea na kuuzunguka mbuyu. Yaani inazidi kuzunguka tatizo badala ya kulitatua. Na sababu kubwa ni kwamba inazunguka kwa sababu yenyewe ndiyo ilivisajili, lakini leo inavifuta.

Wizara ya Elimu inayopaswa kuwa madhubuti inachezewa tena kama hivi. Unafuta vyuo kwa sababu havitoi elimu inayofaa, je wewe unatoa elimu bora?

Mimi ninachoona hapa ni kuzunguka mbuyu tu. Hakuna kitakachofanyika bali ni kuzunguka kama ndege aliye kwenye 'cage'.

Toeni Elimu bora ili mtoe vitu bora!
 
Nilikuwa nina imani sana juu ya utendaji wa mama ndalichako kabla hajaingia kwenye siasa,huyu mama amebadilika sana tokea aingie kwenye siasa
 
Tukia dawa ikuingie wewe wacha Magufuli ainyooshe hii nchi....au utakua mmiliki wa chuo kikuu cha TEKU
 
Na hatujasahau kuwa mwakavjana tu wametoka kujisifu serikali ya chama tawala kuwa wamepiga hatua kielimu kutoka kuwa na chuo kikuu kimoja wakati wa uhuru hadi kufikia vyuo vikuu zaidi ya sitini...leo vipi tena havifai wkt mlivitumia kujisifu?......hawa jamaa ni wasahaulifu sana
 
Mi naona wafute tu coz kuna vPhD vya ovyo ovyo huku mitaani mtu ana PhD but ukimwambia aongeze kingereza utakimbia

Ili kuondoa aibu hii zibaki diploma tu PhD zinatuaibisha tunaishia ze zee ukiweza sana I love you

Naona umeamua kurusha mawe magogoni
 
Mi naona wafute tu coz kuna vPhD vya ovyo ovyo huku mitaani mtu ana PhD but ukimwambia aongeze kingereza utakimbia

Ili kuondoa aibu hii zibaki diploma tu PhD zinatuaibisha tunaishia ze zee ukiweza sana I love you

Umeamua kumsema Magufuli....mungu anakuona
 
Sio ubora wa wapi unaotafutwa ..mie mwenyewe naona kama upuuzi mtupu ...
 
Nilikuwa nina imani sana juu ya utendaji wa mama ndalichako kabla hajaingia kwenye siasa,huyu mama amebadilika sana tokea aingie kwenye siasa
Mimi naona ipo shida mahali hapa Afrika. Mimi hadi leo akili inanigomea kabisa. Hakuna mtu ambaye ana legacy kubwa kama Prof wetu wa kule Muleba. UN anaheshiwa mno nenda Kibera Nairobi.
Napata shida hasa nini kinasababisha. Naamini mifumo yetu haiko sawa.
 
Tumeshindwa kujenga misingi ya Taifa na sasa tunajikanyaga. Kila kitu kimewekwa kizimamoto tu. Ndio maana kujikanyaga huku hakuishi na yamekuwa ni maisha yetu.
 
Mama ndalichako naomba ufute vyuo ambavyo havina sifa maana vinazalisha watu ambao haeleweki kabisa.

Pia ni bora tukawa na vyuo vichache ambavyo vikitoa product za kweli walioiva vilivyo na wenye maadili mazuri na siyo kutoa wasomi wezi.
 
Mimi naona ipo shida mahali hapa Afrika. Mimi hadi leo akili inanigomea kabisa. Hakuna mtu ambaye ana legacy kubwa kama Prof wetu wa kule Muleba. UN anaheshiwa mno nenda Kibera Nairobi.
Napata shida hasa nini kinasababisha. Naamini mifumo yetu haiko sawa.
Tatizo ni CCM
 
Back
Top Bottom