unafikiri nifanyeje?

unafikiri nifanyeje?

mafia boy

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2013
Posts
268
Reaction score
82
mimi nina msichana wangu ambae tupo kwa mda mrefu sana,katika miaka mingi tulio ishi tumejikuta tunapendana zaidi na kujiona tunaweza kuishi pamoja kama mke na mume,hivyo
tunajipanga ili tuwe pamoja kama mke na mume hapo baadae,kiukweli mimi nipo nae mbali kwa sasa yeye yupo dar nami nipo zenji kimasomo(chuo)na natarajia mwaka huu kumaliza masomo,na mungu akijaalia panapo uhai na uzima tutaenda kumchagua rais mpya tukiwa tumefuatana kama mke na mume.
kitu ambacho kinachoniumiza kichwa ni kwamba binti alipata wazo la kuenda VETA kupata ujuzi wa fani fulani,ila mie hakunishirikisha,akaenda kafanya mambo yake kamaliza alipopata na fasi ndio aliponiambia kwamba anataka kuenda VETA nikamuambia ni swala zuri sana,ila unataka kuchukua fani gani?akanijib nataka kuenda kuchukua fani ya hoteli,daaaa,mzee kichwa kiliniuma kusikia hotel,kwanza nilikua mbishi kidogo kumkubalia,maana mi najua mambo ya mahotelin,lakini kwakua binti ashapata nafasi akaniambia amelipiwa tuu na yeye anapelekwa tuu akasome,kishingo upande nikamuambia poa,kwakua tunaaminiana,
akanza chuo na alikua anaendelea vizuri,mpaka mwisho ulivyofika kamaliza akaenda field na akarudi kumalizia mitihani ya mwisho,hatimaye akapata cheti.
katika kuhangaika hapa na pale kutafuta kazi huwezi amin hata hajaniambia wala kunishirikisha pia,nilikua najua kama leo anaenda kufanya usahiri wakati nampigia sim mda mrefu hajapokea then akinitafuta ndio ananiambia kwamba alikua anafsnya usahiri,kwa bahati nzuri sasa amepata pa kujishikiza,tatizo liliopo anafanya kazi tabata yeye anakaa kigogo,anaingia saa 9 jioni anatoka saa 6 usiku au saba usiku,so mawasiliano kwa sasa yamepungua sana kwa kisingizio yupo kazini sim wanazima anatoka saa saba mie nishajipuunzisha,na asubuhi au mchana mimi nipo na mambo yangu ya chuo,siwezi kumcheki yeye,na kikubwa zaid mi hii kazi siikubali sana kwa mtoto wakike,then haswa kwa hizi shift za usiku,sasa hapo sijajua nifanye nini,
naombeni mawazo yenu wakuuuu

 
embu jaribu kukaa nae kwanza umweleze jinsi unavyofikiri kuhusu hayo maisha then umsikie atasemaje.
 
Kwani wewe swala lako hasa ninini? Hiyo kazi huipendi au unahisi utasalitiwa au shida ni kutopata tena muda mwingi wa kuwasiliana naye?
 
inaonyesha unapenda sana kulalamika......


Binti kajitahidi kapata kijiajira chake kama huipendi badala ya kulalama mtafutie mbadala.....

La sivyo endana na hali halisi...........

Mwisho.
Alokwambia kila mfanyakazi hotelini ataishia uzinzini nani? Wangapi wanafanya kazi maofisi tena posta(nimeandika posta kuonyesha msisitizo ) lakini wanajiuza coner bar?

Kinachotakiwa ni malengo na kujitambua plus msimamo wa binti
 
So far you two aint tied anyhow...ndio kwanza mpo kwenye stage ya awali....peaneni nafasi ya kila mmoja kufikia ndoto zake kabla ya ndoa.
Mawasiliano si lazima yawe kila siku, kuna weekends unaweza ukawa na utaratibu huo...pia hapo Zenji ni kitu kama 40,000 kwenda Dar na kurudi huko.
 
kazi ya hoteli ni kazi kama nyingine,kinachotakiwa ni binti kujiheshim na kuheshimu mahusiano yenu,ila kwa uzoefu wangu kazi ya hotel asipokua na msimamo basi,tarajia kusalitiwa,stopisha habari za ndoa mcheki kwanza kama atabadilika ujue huna mke!
 
Mtafutie kazi huko huko zenji si kuna mahotel kibao!!

fidel80 hata akimtaftia huko zenji kama binti ni kifagio atamdhalilisha tu,coz shift ya usiku yy atakua kalala, binti yupo kazini!ampimie kama binti atabadilika ajikatae taratibu!
 
kwa hiyo unataka aache kazi halafu iweje? swala ni kumsisitiza awe mwaminifu tu
 
fidel80 hata akimtaftia huko zenji kama binti ni kifagio atamdhalilisha tu,coz shift ya usiku yy atakua kalala, binti yupo kazini!ampimie kama binti atabadilika ajikatae taratibu!

awe anamsubiri getini pale kabla hajatoka mahotel makubwa hayaruhusu mhudumu kulala na mteja
 
ukipenda amini, unzinzi ni popote hasa pale ambapo hutegemei, akipata kazi mbadala ataacha usimkataze sasa
 
awe anamsubiri getini pale kabla hajatoka mahotel makubwa hayaruhusu mhudumu kulala na mteja

wateja hua hawana shida na wahudumu coz wengi wanaokuja hotel ni pea,mameneja wetu ni wakware,meneja atamrubuni,na mihela yake,kaka etu yy ndio yupo chuo,kama binti hana msimamo ni ngumu kukwepa vishawishi!
 
wateja hua hawana shida na wahudumu coz wengi wanaokuja hotel ni pea,mameneja wetu ni wakware,meneja atamrubuni,na mihela yake,kaka etu yy ndio yupo chuo,kama binti hana msimamo ni ngumu kukwepa vishawishi!

navyo elewa hapo kutokana na uzeefu wangu mabinti wakitoka vyuo wakabahatika kazi na huwa wanadakwa na bazazi ili kuwatumia kingono zaidi na wakisha dakwa wanawasahai hao wachumba zao walio wekeana ahadi
 
Mawasiliano yanapopungua hiyo ni moja ya dalili zinazopelekea mahusiano kuvunjika! kwa hatua mliyofikia mawasiliano ya mara kwa mara ni muhimu sana hasa kama mnapendana kwa dhati....cha muhimu ni kukaa nae vizuri kuongea jambo hilo kwa kina! kama mnaelewana na mnajua mnachokifanya, i hope mambo yataenda vizuri
 
navyo elewa hapo kutokana na uzeefu wangu mabinti wakitoka vyuo wakabahatika kazi na huwa wanadakwa na bazazi ili kuwatumia kingono zaidi na wakisha dakwa wanawasahai hao wachumba zao walio wekeana ahadi

yah!ndio hvyo my dear,kinachotakiwa ni binti awe na msimamo bas!
 
yah!ndio hvyo my dear,kinachotakiwa ni binti awe na msimamo bas!

:becky: hapo kazi binti akipata kazi anafikiria kupanga upande wa nyumba, kumiliki mkoko, kununua kiwanja vyote hivyo anavitaka kwa muda mfupi na siraha yake kubwa ni kujipendekeza kwa boss amvulie nepi/kyupi hapo usalama kwisha kazi
 
nashukuru kwa michango yenu,pia ningependa kusema hivi sijamaanisha wote wanaofanya kazi hotelini ni watu wa ajab,usaliti hauletwi na kazi ni tabia ya mtu ila nina uhakika tabia inabadilika kutokana na mazingira pia,wale wanaosema kazi ya hoteli ni kazi kama kazi nyengine nakubaliana na wao ila wajue mazingira ya hoteli mimi nayajua vizuri kwani wakati wa likizo hua nafanya kujipatia vijisenti vya nauri kwa semester inayofuata,jamani mahotelini heshima yake ni ndogo sana kwa wale wafanyakazi wenyewe,hawaheshimiani kama huyu mke wa mtu wala mume wa mtu,kila mtu akipata mshahara anataka kumn'goa mtu,haswa kwa hawa wasichana ambao ndio wanaingia kazini wao akili zao ni kutoka tuu na unafikiri mtu anaakili ya kupanga nyumba,kua na maisha mazuri faster unafikiri nini kinachofuata?
pia wale wanaonibishia hebu angalia umbali kutoka tabata na kigogo tena usiku wa saa 6 na saa 7,je haiwezi kua kishawishi tosha?tatizo kubwa hakunishauri mwanzo hata mie napenda afanye kazi ila angenishauri mwanzo sidhani kama ningemshauri aende kufanya hotel kwa sababu ya haya
ajira zake hazina uhakika hata usain ajira ya miaka saba unaweza ukafukuzwa mda wowote,
hofu yangu kwake hua hapendi kushauriana je unafikiri tutafika kla mtu akiwa na maamuzi yake?
 
Back
Top Bottom