Unafiki: Wenye Kusema vs. Wenye Kutenda

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
911
Reaction score
792
Watu wasio na maadili ndio wamesimama mstari wa mbele kuwakumbusha waadilifu umuhimu wa kulinda maadili. Wenye dhambi ndio wamesimama mimbarini kuwahubiria wacha Mungu umuhimu wa watu kuacha dhambi. Wenye michepuko ndio wanaogombania majukwaa kuendesha semina za uaminifu katika ndoa.

Wasio na biashara zinazoeleweka ndio wanaoendesha ‘podcast’ kutufundisha namna ya kuendesha biashara. Wahalifu ndio wanaosimamia kampeni za kuhamasisha watu wema kuheshimu sheria. Wanaovuruga amani ndio hao hao wanaopishana majukwani kutoa wito kwa watu wema kulinda amani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…