Unafiki wa wanasiasa na salaam kwenye mikutano

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,422
7,211
Hii kitu ya wanasiasa wa CCM kuwasalimia wananchi kwenye mikutano eti 'Salaam Aleikum: Bwaba asifiwe' ni unafiki mkubwa wa viongozi wa CCM.
Kwanza haipendezi na zaidi ni kinyume cha katiba inayokataza kuchanganya dini na siasa. Tukimsifia mungu ni vema tu kwani sote tunaungana kuhusu uwepo wake.
Kwa wakristo Bwana ni Yesu, na Salaam Aleikum ni salaam aliyoitumia Mtume Muhamad..... kwa wafuasi wake. Sasa hapo niambie baniani na mwenye dini ya kienyeji wanaingia wapi? Kwanza ni mzaha mkubwa.
Muislam wa kweli haamini kama yesu ni Bwana (Mungu), na mkristo wa kweli anakereka kwa salaam ya Salaam Aleikum anaona ni uislaam.
Namsifu JK, hatumii salaam hizi za kinafiki na hii inaonyesha asivyo mtu mnafiki;Pongezi sana ndugu yetu. Safu ya viongozi wengi wa CCM hawana msimamo ila wanafiki bendera kufuata upepo washibe.
Kwa kua lazima mwanasiasa asalimie kadamnasi kuliko kuiga usichokijua waambie watu: 'Amani iwe nanyi' nao wakujibu 'Iwe nawe pia'. Nadhani hiyo ndio salaam ya mtume Muhamad na Yesu kwa wafuasi wao, lakini tusiipe sura ya udini kwa kutumia Kiarabu au Kiebrania- ie Shalom.
 
Waambie hao.Na huko Radio Tanzania oh samahani, TBC ndio zao hizo.Waache udini.Mwl.Nyerere tunakukumbuka kweli!
 
Back
Top Bottom