Maramla
JF-Expert Member
- Jan 8, 2014
- 588
- 648
Na Munis Swai, ARUSHA.
Kuna jambo tunapoelekea Noeli ya Xmas na Mwaka mpya 2020 lazima turudi nyuma tujitakase. Hivi ninapoandika hapa tayari kwa Tanzania kuitwa wanaharakati ni doa kubwa, kwa nini?
Kwanza, kuna wanaharakati uchwara wameivamia hii tasnia yenye malengo mema ya kufanya advocacy kwenye mambo ya maendeleo na haki za watu.
Ghafla limeibuka kundi la kina Maria Sarungi, Karume na wengine aidha ni wanasiasa per se au ni watu waliotamani vyeo fulani wakiwa na wagombea wao 2015 lakini wakashindwa na wamegeuka kupinga kila kitu cha Serikali kwa hasira zao binafsi au wengine hata sio watu wenye uaminifu na nchi hii kwa kuwa wana asili ya kwingineko. Nao eti ni wanaharakati!
Anaibuka mtu kama Fatma Karume, ana hasira zake kwenye masuala ya madini ambako wateja wake waliokuwa akiwasaidia kuifaidi nchi wamesambaratishwa kwa maslahi ya Tanzania kaibuka ghafla naye kawa mwanaharakati na tunamsikiliza!
Maria Sarungi ni Team January Makamba na alikuwa kwenye team yake daima na alishachagua hadi cheo. Naye leo mwanaharakati!
Kwa hiyo siku hizi harakati zimekuwa ni mtu yeyote mwenye hasira na mtu fulani Serikalini anaanzisha movement ya kuponda kila kitu hata pale Serikali inapofanya mema ya wananchi.
Hii ni aibu sana kwetu tuliojenga hoja za kuboresha nchi hii na sasa tunaona mabadiliko tuliyoyapigania yanafanyiwa kazi ingawa bado yapo maeneo ya kufanyiwa kazi zaidi ambayo bado.
Pili, kama nilivyosema hapo juu, katika eneo la haki tujue kuna haki na wajibu. Sisi wanaharakati wa zamani tumelitofautisha sana hili.
Tumekuwa tukitoa elimu kwa jamii kwamba unahaki zako lakini pia unawajibu wa kutii sheria na mamlaka ya nchi.
Siku hizi ni tofauti, yani wanaharakati ni kuwajaza watu akili mbovu kuwa wanaonewa tu hata pale ambapo wao wenyewe ndio wenye makosa.
Juzi amekamatwa mtu anaitwa Mwanaharakati Toti Magoti, mpaka sasa tunaambiwa anahojiwa huenda kuna makosa makubwa akiwa polisi.
Wanaharakati tumeibuka na kudai kaonewa. Hatujui aliresist vipi kukamatwa, hatujui kama alipewa wito akakaidi, hatujui ana makosa gani ila tunataka tu aachiwe. Moja ya hoja zisizo na msingi sana katika masuala ya advocacy.
Lakini cha ajabu zaidi, wakati sisi zamani tulikuwa tunapigania jamii hivyo tunafuatilia matukio nchi nzima na kuona yale yanayopaswa kufanyiwa advocacy, wanaharakati wa Dar wao wanamtandao wao; akiwa mwandishi wa habari tena wa Dar na akawa mtu wa mrengo wao wa kutukana na kupinga kila kitu au mtu wa LHRC au TLS ndio utasikia kelele.
Kuna waandishi walipigwa katika mkutano wa CUF kimya, kuna vijana wa asasi za kijamii au wananchi wa kawaida wanakamatwa kwa makosa mbalimbali na wengine wanaonewa mpaka Rais ajue aingilie kati jamaa hawa kimya. Ni kama wanaorodha ya watu wao wa kazi zao!
Huu sio unaharakati (activism au advocacy) ni njaa, majungu, fitna, na kufanyia kazi matumbo yetu badala ya maslahi mapana ya jamii.
Uanaharakati ni uchambuzi wa mambo yawe ya kisera, kisheria, kitaasisi au kiutendaji na unakuja na uchambuzi mbadala na kutoa mapendekezo sio kukurupukia kila jambo, kupinga kila jambo na kubagua mambo ya kuyapinga au sura ya mtu wa kumtetea. Huu ni unafiki.
Mwandishi amefanya kazi katika asasi mbalimbali nchini ikiwemo Kivulini, Kituo cha Amani na Maendeleo (CPD) na sasa ni Afisa Ushauri wa Maendeleo Vijijini.
Sent from my iPhone using JamiiForums