Unafiki wa TCU

Aisee! umetumia vigezo gani kujua mimi ni kijana halafu natafuta vigezo? Kama nchi yetu itaendelea kuwa na elimu ya namna hii taifa hili halitaendelea kamwe. Wasomi wa kariba yako ambao wanatangulia kutangaza kuwa wapo kwenye comfort zone kwa kuwa wapo tayari kwenye ajira. Did you take any critical thinking course in your bachelor program? Sina maana ya kukukashifu isipokuwa unanishangaza how you rush to the conclusion! Wonderful
 
kweli ulichoxema kupandisha viwango chuoni ni kuonea wengne isitoshe hiyo pia wamepandisha viwango/alama kwenye mtian wa form six 2016 kwani 55 ni D. huu ni ubabe kabisaa
 
Kama huna sifa ya kwenda chuo kikuu we kaa benchi mjomba, wala usijipenyezee hoja zako ambazo hakiza nafasi kwa sasa! Kama upo shule kaza msuli utilize vigezo na kama ni muhanga angalia alternative nyingine, na sio kuelekeza watu vya kusoma
Sikumaanisha vibaya kukushauri vitabu vya saikolojia isipokuwa nimeona jambo lipo ndani yako ni psychological problem. Unaonesha ni mtu ambaye unashindwa kutawala hisia, unatoa hitimisho bila kufikiria kwa kina. Unaandika kama vile unaniona na kunifahamu vizuri. Hapo ndipo napata tabu kidogo juu yako. Ile comment yangu uliyoingilia kati ungejaribu kuifuatilia ilikuwa ni majadiliano na mtu fulani ambapo mwisho tumeafikiana katika hoja zetu.

Sasa nyinyi wasomi wa viwango vya juu nashangaa sana inapotokea mkakosa hata ile basic knowledge ya kujibizana kwa hoja ndipo tunapoanza kuona kuna tatizo kwenye mfumo wa elimu yetu, na si viwango tu. Wewe unamtazamo wa kila anayechangia suala la vigezo basi form six, huoni hilo ni tatizo? Jaribu kutafuta threads zangu nyingi tu humu nimeongelea mfumo wa elimu, yawezekana ukatoa mchango mzuri wa mawazo endapo utapunguza hisia.

Ndalichako kafanya research nyingi tu kuhusiana na elimu. Na matatizo ya elimu yetu anayajua. Kuna research moja kafanya akishirikiana na Mama mmoja hivi inaongelea Uchaguzi wa masomo kwa wanafunzi wa sekondari ni jambo la mapenzi/ uwezo au kuna sababu zinalolazimsha uchaguzi huo. Kuna facts nyingi wamezitoa. Nilitarajia angeanza na hizo changamoto ambazo tayari amekwishazifanyia utafiti.
 
una mawazo ya kujenga mkuu
 
BORA MKUU UMENISAIDIE KILA MTU ANA HAKI KUPATA ELIMU NA DIGIRI TUNAKO ENDA NI LEVEL YA KAWAIDA SANA
 
Mkuu hata mimi binafsi nimeshindwa kuwaelewa TCU. Hili swala la kubana sana kiukweli sio "fair" wakati shule zao za serikali zenyewe ovyo, hakuna mitaala ya kueleweka, n.k... Hata huku chuo kikuu penyewe wanaposema wanawaleta wanafunzi "competent" pia utoaji wa elimu kiujumla bado ni mbaya. "Tanzania ni Tanzania tu, kuanzia chekechea hadi chuo kikuu" elimu bado mbovu hivyo inahitaji mabadiliko kwa asilimia kubwa ila sio mabadiliko ya kuumiza watu kijinga...
Kama wanataka watu "competent" basi waanze marekebisho kwanzia shule za awali, NA WAELEWE KUA HII ITACHUKUA MUDA
 
Mkuu unaandika vizuri sana, una facts na maelezo yaliyoenda shule
 
Mtu kama wewe kuwa na ajira ni aibu kwa taifa.... Hata akili ya kawaida kwenye kuandika comment unakosa!
 
Mkuu, ndiko wanakotupeleka.

Wanataka wachache wafaidi elimu, ila wengi wasiona uwezo wabaki watawaliwa tu yaani vi.laza.
Ili jambo ni la mpito tu.
Naamin watalifikiria upya, kwan Tanzania ni nchi inayoendelea bado haijafikia maendeleo ya nchi kama marekan.
Na nchi kama hii inatakiwa iwe na wasomi weng il ipate kuendelea lakn c kwa kuwapa elim hii wachache.
 
Ili jambo ni la mpito tu.
Naamin watalifikiria upya, kwan Tanzania ni nchi inayoendelea bado haijafikia maendeleo ya nchi kama marekan.
Na nchi kama hii inatakiwa iwe na wasomi weng il ipate kuendelea lakn c kwa kuwapa elim hii wachache.


Ingekuwa hivyo wala isingekuwa shida kutambua hilo.

Kipaumbele cha elimu kwa sasa ni nini?Madawati? Kurekebisha madaraja ya ufaulu? Kupunguza idadi ya watakiwao kujiunga Chuo Kikuu...?
 
Ingekuwa hivyo wala isingekuwa shida kutambua hilo.

Kipaumbele cha elimu kwa sasa ni nini?Madawati? Kurekebisha madaraja ya ufaulu? Kupunguza idadi ya watakiwao kujiunga Chuo Kikuu...?
Elimu yetu bado haijafka huko wanapotaka kuiwahisha.
 
Elimu yetu bado haijafka huko wanapotaka kuiwahisha.


Uko sahihi.

Tatizo maamuzi ya kisiasa na kulipizana visasi. Serikali ni ile ile ya CCM.

Kwa mfano Waziri Mkuu alikuwa mmojawapo wa mawaziri (Naibu Waziri Elimu) akishughulikia elimu.

Leo hii naye anayaponda maamuzi yake yale aliyoyaamua yeye mwenyewe.
 
BORA MKUU UMENISAIDIE KILA MTU ANA HAKI KUPATA ELIMU NA DIGIRI TUNAKO ENDA NI LEVEL YA KAWAIDA SANA
Ilikuwa iwe hivyo lakini wamekuja wale wanaoamini makaratasi na nadharia, wamewanyima Watanzania haki ya elimu. Wangewapata nafasi watu wasome kadiri ya wanavyohitaji. Wanajificha chini ya mwanvuli wa kuepuka graduates wasiokuwa na sifa, hivi chuo kukuu hakuna mitihani? Kwanini kuna discontinuity? Ni bora wangeweka GPA ya 2.7 ili uendelee na mwaka kuliko kuwabana watu wasiingie vyuo.
 
Naomba niseme kitu,kiukweli elimu yetu ulikuwa imeoza kwa kuwa wanafunzi walikuwa hawasomi,Instagram na fb kila dakika ndo ulikuwa kaz yetu then mtu huyo anasoma kwa kurelaz kwa kuwa unajua ataingia tu degree then mtu huyo huyo anakuja kupewa kaz na ndugu yake angalia GPA yake mbovu,mtu ana pass ya 2.7 then anapata kaz mapema kuliko mwenye GPA ya 3.5 na kuendelea,heshima Mtaani na makazini haipo,ukiwa na diploma au degree kila mtu anayo,fedha za serikali kupotea kusikoeleweka,TCU wanapeleka wanafunzi vilaza then wanapewa mikopo alafu mbele ni hasara kwa taifa,udom wanafunzi 7000 vilaza,lakini tujiulize walipelekwa na nani kule,nani aliwapeleka

Solution kwa serikali walichofanya
1.njia za mkato,kwenda chuo hazipo,ukipita form5 na 6 au ukipita cheti na diploma mbele kuna daraja la kuvuka
2.kurudisha hadhi ya elimu,mwenye degree na diploma tutawajua kirahisi na heshima itakuwepo kwanzaia makazini,Mtaani na kila sehemu
3.fursa lukuki za ajira,baada ya mkaka mi3 watakaotoka vyuoni asubuhi unaptiliza kazini na sio kusubili mjomba au shangaz akuunganishie
4.chet cha diploma kitaheshimika na wahusika kujiajiri au kupewa kazi
5.tutapunguza vusingizio na ugumu Wa maisha,ile tabia ya kusema sijaendelea kwa kuwa baba au mlezi hana fedha itapotea,sasa hvi tutaomba cheti chako kwanza na ndo tutajua Shida fedha au ni ww kilaza
6.kila mtu atafanya kazi vizuri,wakusoma atasoma kweli,maana kazi ni nyepesi tu kudahili wasiojua

INSHORT:hata uwaambie Leo wanafunzi kuwa GPA ni 3.5 watakaopata ni wachache nimesoma ifm mkaka 5 huyo GPA haiji tu kama tunavotamka,mtu unakaa chini na kutuliza akili,lkini mwanafunzi Wa sasa hvi mwambie aamke saa11 asubuhi hataki,anaamka saa4 then tukipewa 3.5 tu nalalamika!!!!kila mtu achape kazi
 
Yangekukuta ww usingesema haya yote.
Unasema coz yamemkuta mwenzako.
Mda mwengine pima kitu ndio uropoke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…