Unafiki wa Polepole na ukweli kuhusu MCC

njundelekajo

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
310
227
UAMUZI WA M.C.C NA UNAFIKI WETU

Nguzo Noel .R.

Kamusi ya kiswahili imetoa maana ya neno "UNAFIKI" kama hali ya kujifanya kua ni rafiki au kutokua mkweli.

Unafiki ni utovu wa ukweli katika muendelezo wa kibanadamu hasa kwa lengo la kujipatia sifa.Mnafiki anatenda wema kwa Nje lakini nia yake ya ndani ni tofauti.Lengo la unafiki ni kupendeza watu Wengine ili kupata faida toka kwao.

Dini zote za kweli hupinga UNAFIKI.Biblia takafu pamoja na Quran zote pamoja zinapinga UNAFIKI.

"Vivyo hivyo nanyi kwa nje mwaonekana watu wema na wenye Haki,bali ndani mmejaa unafiki na maasi"(Matt 23:28)

Wanafiki wengi wanachokisema si wanachokiamini (Al-Baraqash 2/8)

Mtu mnafiki anategemea mapato yake katika kuongea na kutenda katika mfumo kuridhisha kila upande wenye matatizo.HUWEZI KUHALALISHA UBAKWAJI WA DEMOKRASIA YA ZANZIBAR KWA HOJA YA KUACHANA NA MISAADA YA MABEPARI NA USIWE MNAFIKI.

Mwishoni mwa mwezi wa 3 mwaka huu 2016 Shirika la kimarekani linashughulika changamoto za millennia (M.C.C.)liliiondoa Tanzania kwenye orodha ya nchi zenye sifa ya kupewa misaada na shirika hilo.Vigezo vinavyotumika kuipa misaada nchi husika ni pamoja na utawala mzuri na wa Haki,Uhuru katika shughuli za uchumi na uwekezaji katika rasilimalia watu.

Wapo watu kwa sababu ya unafiki wanataka ionekane KUONDOLEWA KWENYE SHIRIKA HILO NI JAMBO LA KAWAIDA .

Nchi Yetu ilikidhi rasm vigezo vinavyotolewa na M.C.C 2005.Vigezo vya msingi ni utawala, Uhuru WA kiuchumi pamoja na uwekezaji kwenye Rasilimali watu.

Ni kweli kwamba nchi zilizoendelea kutengeneza mahusiano ya kinyonyaji na nchi za kiafrika.Je hivi vigezo vya vilivyotuondoa M.C.C. vinatunyonya kwa namna gani?
Hivi utawala mzuri na WA Haki NI jambo baya? ,Uhuru katika shughuli za uchumi ni uhuni?,Uwekezaji katika rasilimali watu ni upuuzi?

Wapo watu kwa sababu ya unafiki wanalazimisha iaminike TUMEJIANDAA KUJITEGEMEA.

Unafiki unawafanya wengine wadanganye HAKUNA UHUSIANO KATI YA M.C.C. NA SERIKALI YA MAREKANI!! unafiki unafanya Waziri analalamika juu ya uamuzi huu makada wanasema hakuna tatizo.

1.TUMEJIANDAA KUJITEGEMEA?

Ni unafiki wetu umetufanya tuamini nchi kujitegemea NI jambo la kulala na kuamka tu.Serikali tunayoamini ipo tayari kufanya nchi kujitegemea ina miezi 6 tu tangu iingie madarakani.

Wakati tunafikiri tupo tayari kujitegemea serikali haijamaliza hata kupanga safu zake za uongozi (nyinyi mnaita kutumbua majipu).

Tuna uwezo wa kujitegemea lakini sio sasa.Tujitegemee sasa KWA maandilizi yapi?Mpaka sasa walimu waliojariwa 2012 hawajapandishwa madaraja yao,Viwanda hatuna,kilimo chetu kitaabani,elimu Yetu I "hohehahe"

Adhabu ya unafiki ni upofu.Upofu unatufanya tusione umuhimu WA M.C.C kwa kipindi hiki cha kujiandaa na huko KUJITEGEMEA

Kwa mujibu WA taarifa ya wizara ya fedha iloyosomwa tareh 14/Nov/2014 wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya m.c.c. 2 jumla ya dola za kimarekani million 698 zilitumika kufadhili miradi mbalimbali ikiwemo kilometa 450 za barabara,kilometa 300 za mtandao wa nyaya za umeme, miradi mbalimbali ya maji ya maji Daresaalma, Kidunda,Unguja nk hata jeuri ya serikali kuufanya mgao wa umeme kua historia ukipata nguvu kutokana na M.C.C

Kama bado hatuna mtandao WA uhakika wa barabara hatupo tayari kujitegemea,kama bado kuna Wenzetu hawana uhakika WA kupata maji safi bado hatukujiandaa kujitegemea,kama bado mfumo wetu wa elimu unazalisha wasomi legelege waliokosa ubunifu hatupo tayari kujitegemea,kama bado tuna bajeti inayoyotegemea pombe NA sigara kama vyanzo vya uhakika bado hatukujiandaa kujitegemea Unafiki wetu unatulazimisha tuseme TUMEJIANDAA kujitegemea.

HAKUNA UHUSIANO KATI YA M.C.C NA SERIKALI YA MAREKANI?

Kwa Afrika ili uwe kipenzi cha watawala ni kukubali kufikiri kama wao...

Watu wanajaribu kulazimisha "mahaba" kwa kudanganya. Wapo watu wanajaribi kuitenganisha M.C.C na taifa la marekani kwa sababu tu imeandikwa kwenye makaratasi M.C.C. NI SHIRIKA HURU.

Hatua ya tano ya M.C.C. ili nchi ipate misaada hiyo ni M.C.C kutoa taarifa kwa serikali ya marekani ya kuingia mkataba na nchi husika.Sasa kama hakuna uhusiano wowote kwa nini M.C.C. inalazimika kutoa taarifa?

Kama mtendaji mkuu WA M.C.C. anateuliwa na rais wa marekeni na kuthibitishwa na senate ya nchi hiyo unatenganishaje M.C.C. na taifa zima la MAREKANI?(Dana J hyde C.E.O WA M.C.C. alithibitishwa tar 20/5/2014) na sanate hiyo.

Kwakua tumeamua kua wanafiki tunasema UHUSIANO WETU NA MAREKANI UTABAKI KUA IMARA kwakua M.C.C. ni chombo huru.

Wanayosema haya hawasemi kwa bahati mbaya .Wanaujua ukweli ,wanasema kuthibitsha kauli ya Alik Shahadah.."In much of Africa the theory is if you eat enough crumbs from the master's plate you will eventually get foo"

Wengine wanakubali kujisaliti ili waukwae ukuu WA wilaya,Wengine wameamua kuzisaliti haki za wanzibari ili waukwae ukurugenzi.Hamuwaoni kwenye vyombo vya habari Wengine "wakijichetua" kwa kulia,kubeba mabox ya dawa?

Ingekua haya yanasemwa kwakua sisi ni waoga ingeleta matumaini kwakua uwoga ni hali tu inayotokea na kuondoka haraka.Ila kwakua ni wanafiki na unafiki ni tabia sio hali.Tabia ni kama ngozi .

Tulioamua kutokua wanafiki tutaendelea kusimama katika kweli hata ikionekana tuna pinga kila kitu. Soren Kierkegaard alipata kusema "there are two ways to fooled ,one is to believe what is not true,the other is to refuse to believe what is true."

Uwongo ni kuamini TUMEJIANDAA KUJITEGEMEA. UKWELI NI KWAMBA HAKI YA WAZANBARI INAANZA KABLA YA UNYONYAJI WA WAMAREKANI.

Don't believe on abstract terms from our leaders, We must learn on something more concrete to measure a leader. Picha za kwenye vyombo vya habari zisitufanye kuamini visivyowekana.

Nguzo Noel .R.
 
12376665_1602211640104372_6334296553671129513_n.jpg

Adui mkubwa wa Taifa hili ni CCM!
Eti heri Watanzania tule nyasi lakini hilo dude libaki madarakani!​
 
Nilishangaa Polepole kuitenga MCC na serikali ya Marekani, wakati pesa za MCC ni za Walipa kodi wa Marekani!

MCC ilianzishwa na kisheria kwa muswada wake kupitishwa na Senate ya Marekani, halafu eti leo hii useme eti kusitishwa kwa nisaada ya MCC serikali ya marekani haihusiki, this is ridiculous.

Tunaposema MCC ni independent, maana yake ni chombo huru kwa maana kuwa hakiingiliwi na wanasiasa lakini kipo accountable kwa serikali ya Marekani, kina oversee namna gani pesa za Walipa kodi wa kimarekani zinatumika, pale wanapopartner na nchi wanazotaka kuzisaidia
 
polepole awadanganye wajinga wenzake wasie jua usiku na mchana haiwezekan ufukuzwe kwenu alafu ujigambe swala la kujimudu kwenye kujitegemea kwni muda ote ulikuwa wap na kwnn kma ulikuwa unataka kujitegemea hukuondoka kwa matakwa yko mpaka ufukuzwe ndo Tz ya leo imetolewa inasema imejiandaa duh
 
Polepole anajitoa ufahamu kwa tamaa ya madaraka, anataka kupata wadhifa kwa style ya makonda. Anajua sana asemacho si sahihi ila njaa yakutaka madaraka inamfanya awe changudoa wa siasa.
 
Umenitoa tongotongo huyu mpolempole anapenda kuongopa tena kwa makusudi kweli ni 'MNAFIKI 100%'
 
Dalili za mvua ni mawingu
taratibu somo linaanza kueleweka kivitendo, porojo za kudanganyana kitoto hazina nafasi, wazungu wameamua kutuminya kiuchumi

Kifo cha nyani miti yote huteleza kila kona kugumu, kabla hatujaumia sana CCM ikubali matokeo mapema vikwazo vitaendelea mpaka tunuke vumbi.
 
Watanzania bhana, maelezo ya Polepole hayakunitosheleza, nikaona heading yako nikasema ewaaa huyu sasa yaelekea Ana concrete facts kuhusu hii kitu MCC, kumbe Na wewe taarabu tu, hata hoja za Polepole hujajibu unaleta assumptions zako. Jamani Kila MTU anaweza kuassume, tunataka wenye facts sio jinsi unavyofikiria
 
facts zipi unazozitaka? Kwani mcc ni benki? Umeambiwa ni taasisi ya umma wa wamarekani na funds wanazozitoa ni fedha za wananchi wa marekani. Hiyo siyo fact? Au wewe ni polepole unataka kutafuta ya kukupeleka tbc ukatudanganye tena? Kubalini tu kuwa mmekurupuka na kuharibu kwa kukosa weledi na diplomacy. Think loudly muache kutuingiza kwenye migogoro ya kiuchumi kwani madhara yake si ya kitoto kama mnavyotaka kutuaminisha. Rejea ya zimbabwe na U.K ndiyo mjipange.
Hivi hii ni mbinu ya kutufanya maskini ili mtutawale kirahisi badala ya kutuongoza ninyi ccm baada ya kushindwa kuungwa mkono?
 
Kwa hiyo unatakaje, ukinyimwa msaada unatakaje, ni lazima tuwajengee wananchi kujiamini siyo tukae kulialia, haya NENDENI UKAWA mkailete hiyo misaada basi.
 
Nilishangaa Polepole kuitenga MCC na serikali ya Marekani, wakati pesa za MCC ni za Walipa kodi wa Marekani!

MCC ilianzishwa na kisheria kwa muswada wake kupitishwa na Senate ya Marekani, halafu eti leo hii useme eti kusitishwa kwa nisaada ya MCC serikali ya marekani haihusiki, this is ridiculous.

Tunaposema MCC ni independent, maana yake ni chombo huru kwa maana kuwa hakiingiliwi na wanasiasa lakini kipo accountable kwa serikali ya Marekani, kina oversee namna gani pesa za Walipa kodi wa kimarekani zinatumika, pale wanapopartner na nchi wanazotaka kuzisaidia
Bahati moja aliyopata polepole nikupata coverage kwenye media lakini kichwani hamna kitu kwa hiyo mlitegema kuwa ajue kuwa CEO wa mcc anateuliwa na obama kwa akili ipi aliyonayo mm ndio nishamzalau ni msaka tonge na hajui chochote
 
Polepole anajitoa ufahamu kwa tamaa ya madaraka, anataka kupata wadhifa kwa style ya makonda. Anajua sana asemacho si sahihi ila njaa yakutaka madaraka inamfanya awe changudoa wa siasa.

Polepole ni bonge la chizi anayejifanya muungwana ili angalao aambulie hsta u-DC kama huyo mnafiki mwenzakeî Makonda! Sitashangaa kama huyu jamaa Polepole atakuwepo kwen orodha ya ma-DC wapya watakaoteuliwa na na JPM!
 
facts zipi unazozitaka? Kwani mcc ni benki? Umeambiwa ni taasisi ya umma wa wamarekani na funds wanazozitoa ni fedha za wananchi wa marekani. Hiyo siyo fact? Au wewe ni polepole unataka kutafuta ya kukupeleka tbc ukatudanganye tena? Kubalini tu kuwa mmekurupuka na kuharibu kwa kukosa weledi na diplomacy. Think loudly muache kutuingiza kwenye migogoro ya kiuchumi kwani madhara yake si ya kitoto kama mnavyotaka kutuaminisha. Rejea ya zimbabwe na U.K ndiyo mjipange.
Hivi hii ni mbinu ya kutufanya maskini ili mtutawale kirahisi badala ya kutuongoza ninyi ccm baada ya kushindwa kuungwa mkono?
Hatari sana.
 
Back
Top Bottom