Unafiki wa Nape, CCM kuhusu ongezeko la posho kwa wabunge huu hapa

Duh Mkuu Nape, inatosha maana hamna majibu now you can see my point mara kwa mara Kwa Mwenyekiti wa CCM taifa kwamba awe anawalazimisha Viongozi wa CCM kuja kujibu hoja hapa JF itapunguza sana majungu. SALUTE!
Maneno yako kweli kabisa lakini hadi hapo tutakapo pata ushahidi toka upande wa madai ndipo tunaweza kumsafisha.. Binafsi simuamini yeyote ndani ya CCM na sababu kubwa ni kwamba hawaendi sherehe bila ndizi mfukoni hivyo sii rahisi kumsafisha mwenye ndizi ya kwamba hakwenda kwenye sherehe kutafuta kula..

nadhani kilio cha wananchi haswa sio Wabunge tu, wala sio swala la ongezeko bali kama nakumbuka ni swala zima la sitting allowance winazoliopwa watumishi wote wakiwa wanatumikia majukumu walokabidhiwa..Mathlan Nnauye anapokwenda ktk vikao vya CCM hulipwa posho hizi? mfanyakazi mtumishi wa serikali anapokuwa katika vikao vya wizara yake hulipwa posho hizi juu ya mshahara anaopokea?...kama kweli Nnauye hajawahi kupinga posho hizi isipokuwa pale walipoongeza inamweka palepale sawa na wengine wanaunga mkono posho hii.

Malipo ya sitting allowance ndio sio halali na wananchi tunapinga malipo haya..Hapa ndio swala lilipoanzia na limekuja pata uzito zaidi pale posho hii lipoongezeka kutoka 70,000 kwenda 200,000, na Zitto na wajumbe wa Chadema walipinga hata utoaji wa posho ya Tsh 70,000 toka kikao kilichopita kabla, na kama sikosei Zitto hazipokei hata hizo Tsh 70,000.. Je yeye Nnauye hapokei sitting allowance.. Je amewahi kuzikana ama kutoa rai zifutwe! na kama anaafiki na anapokea kwa nini atazame ongezeko la posho hizo kuwa haramu lakini sii kilio cha wananchi kinachoanza na utoaji wa posho hizo iwe kwake ama kwa mtumishi yeyote ambaye anawagharimu walipa kodi kwa kazi anayolipwa mshahara. hayo mengine kusema kweli sina wala shauku nayo zaidi maana sii kilio changu.
 
Duh Mkuu Nape, inatosha maana hamna majibu now you can see my point mara kwa mara Kwa Mwenyekiti wa CCM taifa kwamba awe anawalazimisha Viongozi wa CCM kuja kujibu hoja hapa JF itapunguza sana majungu. SALUTE!
Ni sawa kwa Nape kukanusha yale ambayo si sahihi aliyotuhumiwa nayo, lakini kwa viongozi wengi wa CCM ambao wamekaa kwenye mfumo wa wizi watakuja vipi hapa kukanusha madai kama ya EPA, bahasha la Jairo, Mkataba wa Kinyoji wa jengo la UVCCM pale Morogoro road?
Kwenye hii forum wezi wote wanaishia kutembelea humu kama Guests tu basi!
 
Duuuuhhh !!!! Nilikuwa sijui kumbe huwa unapiga majungu JF. Wacha wananchi wadadavue mambo. Napita tu.

siasa mchezo mchafu sana wa kuchezea akili za watu, yani kuwafanya wengine wajinga. Hakuna kitu cha maana hapo anachokiongea nape, anawanyooshea wengine vidole anajisahau yeye
wote ninyi wanasiasa tu mnatetea matumbo yenu huku sie watoto wa wakulima tunaosha vyombo ughaibuni kujisomesha. Ni mungu anaejua jinsi mnavyotunyanyasa walalahoi,ila ipo siku shilingi ikaangukia upande wa pili, shame on you all tz politicians
 
@Nape nimependa majibu yako lakini kuna hili moja na wewe unaweza kuwa mfano wa kuondoa hiyo kansa iliyopo

YAH: VX

nakuomba wewe kama kijana ambaye tunahisi unaingiza mawazo mapya ndani ya CCM jaribu kuwa
  • mbuifu-
  • Onyesha unajali na unaguswa na matatizo ya wananchi.Punguza matumizi
  • Onyesha unaweza kujibana bila kuathiri utendaji wako wa kazi
  • kuwa mfano kwa wazee wetuwaliea VX wa kutoufanya kazi kwa mazoea. badilisha hilo gari . Action speak louder than words.
Ukiuliza How. Huu ndio ushauri wangu

  • Muandikie mwenyeiti wako JK mwambie badala ya VX upewe VITARA iau gai ndogo kwa matumizi ya dar.
    • kwa safari za dar upunguze matumizi ya mafuta na kuokoa mafuta . Kwa sasa may be VX lako linawekewa lita zaidi ya 140 wa wiki. Ukiokoa hata expediture ya lita 50 kwa wiki utakuwa ni mfan mzuri si tu kwa CCM bali hata kwa serikali..... wataona aibu.
    • Uchafuzi wa mazingira unaenda sambana na magari kama VX. Kamak ijana utakuwa mfano wa kuwanyesha "wazee" kuwa utendaji kazi wa mtu na cheo hakiadhiriki kwa kuwa ndani ya VITARA na huku akipunguza caborn footprint.
Saving ya pesa utazokuwa umefanya kwa utumia vitara utakuwa ujumbe tosha kwa watedaji wengine wanaofanya kazi chini ya CCM na kutumia VX just from Masaki to Posta. Hvi jamani ndo imeandikwa kwenye katiba maafisa wa ngazi ya juu wasitumie gari zaidi ya VX from masaki Posta.

Wizara ya Sayansi au ya mazingira iitakiwa kuwa imeisha agiza magari ya umeme japo mchache kwa majaribio dar . Inshanagza hata mnaojiita vijana na mlio karibu na wazee wetu hamuwaambi haya. Mpaka siku wajapan wakiamua kutupa msaada mwaka 2016 ndio tujue kuna gari za umeme zziszotmia mafuta. Hizi gari sasa hivi kuna nyingine zina uwezo w kwenda hata KM 40.

Hivi na nyie vijana wenzetu hamuyai haya au wazee wagumu kuelewa.

Ukivua gamba a VX kwa safari za dar utawashtua wengi baada ya mwaka wape hesabu umeokoa shilingi ngapi? Au sababu umepewa huna gts z kuomba VITARA.

Otherwise nakutakia mapambano mema
 
Bravo Nape!! Majibu yako ya kwanza yalitosha kabisa na mpaka hapa hakuna aliyeleta ushahidi ulio omba. Huna haja ya kuendelea kujibu pumba za watu ambao hawataki kusoma na kujua uhalisia wa jambo.
 
Mheshimiwa Nape, umeeleweka sana na besides who are we kuingilia matumizi ya Vyama vya siasa? JF tusimamie Taifa kwanza. - William
 
Nape,
Naona siku hizi kasi yako dhidi ya CDM imepungua sana, ndio tuseme umeishiwa na nondo za kisiasa?
 
Jew CDM wameanza kuwa makini sana toka Mh. Nape ashike ngazi, siku hizi ni hoja kwa hoja, sio zile enzi za kina Tambwe na that is all Wananchi we could ask kutoka Vyama vyetu vikuu vya siasa for the good of our Nation at large! - William
 
Jew CDM wameanza kuwa makini sana toka Mh. Nape ashike ngazi, siku hizi ni hoja kwa hoja, sio zile enzi za kina Tambwe na that is all Wananchi we could ask kutoka Vyama vyetu vikuu vya siasa for the good of our Nation at large! - William

Hivi Tambwe amewahi kuwa CDM? Anyway, sio issue sana hiyo. Tatizo kuu la Nape ni kudhani anapambana na ufisadi ndani ya CCM! Hivi kwa logic ya kawaida tu, Mafisadi wanaweza kupambana na Ufisadi? One more point, CCM inaendelea kupumua katika uwanja wa siasa kwa sababu ya ufisadi wake, sasa cha ajabu Nape anapoteza muda kutudanganya kwamba anapambana na mtaji (ufisadi) wa CCM!
Alipoona ameshindwa amekigeukia CDM na kudai eti Dr wa ukweli ni fisadi! Baada ya kuona wananchi wamempuuza hana tena hoja! Poor Nape!
 
Jew CDM wameanza kuwa makini sana toka Mh. Nape ashike ngazi, siku hizi ni hoja kwa hoja, sio zile enzi za kina Tambwe na that is all Wananchi we could ask kutoka Vyama vyetu vikuu vya siasa for the good of our Nation at large! - William

Kumradhi, kwani Tambwe alikuwa Chadema?
 
Bravo Nape!! Majibu yako ya kwanza yalitosha kabisa na mpaka hapa hakuna aliyeleta ushahidi ulio omba. Huna haja ya kuendelea kujibu pumba za watu ambao hawataki kusoma na kujua uhalisia wa jambo.



 

nape, kila ukija humu ni pumba tuu, hivi unaposema mtu aende hospitali akaangalie nani kalipa unajielewa akilini? okay umelipa wewe but what is the source of that money? dont fool your fellow innocent Tanzanians
 
Naungana sana na ndugu yangu AZIMIO LA ARUSA.Kuinusuru nchi hii ni kubadilisha kabisa mfumo wa posho,Vile vile kuboresha sana uajibikaji,Watanzania sasaivi hatupo katika mfumo wa kujenga nchi yetu bali kubomoa nchi,Uwajibikaji upo nyuma na ubadhilifu unachukua kasi yaajabu,sasa tunakwenda wapi? Hatupo serious kabsa na ujenzi wa taifa na ndo maana shilingi yetu inazidi kuporomoka thamani yake,Shime viongozi wetu tujaribu kuliangalia sana swala hii kuweza kunusuru nchi yetu.
 
hujajibu hoja ww nape..unachofanya ni kulalama tu ili uonewe huruma...jibu hoja kisomi kwa kutumia ubongo na si kwa kutumia hayo MASABURI YAKO....
 

Duh hapa naona na Dr.Slaa anaingia kwenye hili, kwani hizo sifa ulizompa Nape ndizo pia sifa za Dr.Slaa na kuzidi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…