Unafiki wa Marekani kwenye mapambano dhidi ya ugaidi

Unafiki wa Marekani kwenye mapambano dhidi ya ugaidi

Ushimen

Platinum Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
44,298
Reaction score
111,439
Ingawa Marekani inapenda kujidai kama kiongozi wa muungano wa kupambana na ugaidi, lakini uhusiano kati yake na makundi mengi ya msimamo mkali pamoja na watu wenye msimamo huo ni wenye utata na hata unatiliwa mashaka.

Kati ya makundi mengi ya kigaidi duniani ambayo yamekuwa yakipata uungaji mkono kutoka serikali ya Marekani, kundi la Al Qaeda ni mfano mzuri wa kuonesha kwamba sera za mambo ya nje za Marekani zinatungwa kwa msingi wa kuangalia tu maslahi madogo ya muda mfupi.

Tukiangalia historia, tutaona kuwa kati ya mwaka 1979 na mwaka 1989, ili kupambana na uvamizi wa Urusi dhidi ya Afghanistan, idara za ujasusi za Marekani ziliwahi kuunga mkono makundi mengi ya kiislamu yenye msimamo mkali nchini Afghanistan na katika nchi nyingine za kiislamu.

Na baadaye, mfanyabiashara mmoja wa kiarabu aliibuka kuwa mfuasi mkubwa wa Idara ya Ujasusi ya Marekani CIA katika vita hiyo ambayo uhalisia wake ni kati ya Marekani ya Urusi, na jina la mfanyabiashara huyo ni Osama Bin Laden.

Kundi la Al Qaeda, ambalo wafuasi wake wengi walipewa mafunzo na serikali ya Marekani limekuwa kundi kubwa na hatari zaidi la kigaidi duniani. Mikono ya kundi hilo imefika kwenye nchi karibu zote za kiislamu zilizotumbukia vitani.

Tukiangalia kundi la Islamic State ambalo mienendo yake ni yenye msimamo mkali zaidi hata kwenye macho ya wapiganaji wa kawaida wa Al Qaeda, tutaona kuwa wafuasi wengi wakubwa wa IS walipewa mafunzo na CIA na makao makuu ya vikosi maalum vya Marekani katika kambi moja ya kisiri nchini Jordan mwaka 2012, taarifa ambayo imetolewa na maofisa wa Jordan.

Zaidi ya hayo, alama za idara za ujasusi za Marekani zimefikia hata nje ya dunia ya kiislamu.

Mnamo miaka ya 1990, vikosi maalum vya Marekani vilishirikiana na kundi la Los Pepes nchini Colombia kumwua mfanyabiashara mkubwa wa dawa za kulevya nchini humo Pablo Escobar. Baadaye baadhi ya viongozi wa kundi la Los Pepes walianzisha kundi linaloitwa vikosi vya umoja wa kujilinda vya Colombia ambalo linajulikana zaidi kama AUC. AUC ilihusika na mauaji mengi ya halaiki na mauaji dhidi ya wanasiasa nchini humo.

Mnamo miaka ya 60 ya karne iliyopita, CIA pia ilitoa mafunzo na hifadhi kwa magaidi wawili waliojaribu kumwua kiongozi wa Cuba Fidel Castro na kupindua serikali yake.

Wakati Marekani inapoinua kwa mara nyingine tena bendera ya kupambana na ugaidi, inatakiwa kuachana na ubinafsi wake na tabia yake ya kuangalia tu maslahi ya muda mfupi.



Chanzo:
CRI online
 
magaidi namba moja duniani ni wamarekani wakifuatiwa na wafaransa bado nakumbuka tukio la wachezaji wa togo walioshambuliwa na magaidi ambao walithibitisha wenye makao makuu yao yakiwa ufaransa k=lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa
 
Habari za ugaidi na magaidi dunia huwa naona zimekaa kipropaganda zaidi kuliko uhalisia. Kumbuka shetani Bush Jr alivyouaminisha umma kuwa Iraq ina silaha za chemical kumbe ni uwongo kweupe nia yake aivuruge nchi ili apate kuchukua mafuta pia angalia leo libya imepangalanyika sio Taifa tena ni vikundi vikundi.

Marekani akishaiingilia nchi kivita hiyo nchi huwa haitulii ni vita mwanzo mwisho.

Mzee Makosa
Iringa
 
Magaidi ni watu wa Imani ya wazunguka mawe A.K.A wafia dini
America wanafanya kazi nzuri kupambana na hii Imani ya watu
Wenye ulemavu wa akili tuipe pongezi USA
 
America hutoa mafunzo na silaha kwa nchi
Mbalimbali ikiwemo Israel na nchi nyingi za kiarabu lakini
Cha ajabu waraabu hutumia hizo siraha na mavunzo kumalizana wenyewe pamoja na kuua watu wasio na atia.Niujinga Pia kutaka watu tuamini kwamba Wazungu wanaakili zaidi ya Waraabu ,hadi kufikia atua ya kuwachonganisha kizembe namna hii
 
enhanced-buzz-wide-29924-1362537741-3.jpg
ALEJANDRO PAGNI / Getty Images
 
Kwanini watumie dini ya kiislam au kuna udhaifu kwenye kitabu chenu
 
Marekani mara zote hulinda maslahi yake zaidi, Na nijuavyo mimi kila nchi inapoona maslahi yake yanakuwa hatarini au kutishiwa na mtu yeyote lazima hatua stahiki huchukuliwa ili kulinda maslahi hayo,Nitatoa mifano hai iliyopo hapa Kwanza huko Yemen kwenye vita vinavyoendelea huko Iran inawasaidia kundi la wa Houth kwa hali na mali, Naamini hasa Iran ina maslahi yake huko Yemen na istoshe kuna watu ambao wana Imani moja nao.

Saudi-arabia nao wameingia yemen kuwapiga wa HOUTH sababu nao wana maslahi huko Yemen na isitoshe wanajua kuwa kama IRAN itakuwa na mvuto huko Yemen basi utawala wa Saudia unaona utakuwa hatarini hivyo imeamua kuingia vitani ili kulinda maslahi yake huko.Syria nayo wakati wa utawala wa ASSAD(Baba)walijiingiza Lebanon maana waliona wana maslahi yao huko na kuanza kulisaidia kundi la HIZBOULLAH na mpaka leo hii wanalisaidia kundi hilo kwa hali na mali,Hizboullah nao hawawezi kumwacha ASSAD atoke maana nao wana maslahi yao huko Syria maana wanapata silaha mbali-mbali kutoka IRAN kupitia syria.

Hata Urusi nayo ni lazima iwakumbatie waarabu maana wana maslahi kule wanauza silaha kule wanapata mafuta huko hivyo ni lazima tu kwa wale ambao wako upande wa pili wataita kitendo hicho ni UGAIDI, Hata hapa kwetu Tanzania kama kuna maslahi yetu ni lazima tutawasaidia ndugu na marafiki zetu,Tuliwasaidia Msumbiji,Afrika kusini,Zibambwe,Namibia,Ushelisheli na mpaka huko cape-verde na sehemu nyingi tu nchi yetu ilitia mikono yake najua waliokuwa upande wa pili walituita walivyopenda iwe UGAIDI au KIHEREHERE na majina mengi tu lakini kwetu sisi MASLAHI yetu yamelindwa.

Kenya nao ilibidi waingie vitani huko Somalia ili kulinda maslahi yao (Ingawaje waliingizwa choo cha kike)lakini kwa watu wanaowaunga mkono wanapewa jina zuri lakini kwa ambao wako kinyume na wanaitwa WAVAMIZI. Uganda nao waliwaunga mkono RPF mpaka wakaipindua serikali ya Habyalimana Rwanda nayo iliwaunga mkono M-23 ili kuwafukuzia mbali waasi wanaotuhumiwa kuendesha mauaji ya ki-mbali huko Rwanda vile vile nayo ilikuwa na maslahi huko Congo, Sudani nayo ilibidi tu iingie kwa mlango wa nyuma huko South-Sudan ili tu kulinda maslahi yake huko,Ethiopia nayo kuna kipindi ilibidi iingie Somalia kijeshi ili kulinda maslahi yake huko.

Marekani nayo vivyo hivyo kama ina maslahi sehemu na wewe ukaleta za kuleta ni lazima watashughulika na wewe kwa kila hali,na Daima kwenye mambo ya siasa hakuna rafiki wa kudumu bali yupo kama maslahi ya nchi husika yanalindwa.
 
Magaidi ni watu wa Imani ya wazunguka mawe A.K.A wafia dini
America wanafanya kazi nzuri kupambana na hii Imani ya watu
Wenye ulemavu wa akili tuipe pongezi USA

...Jifunze Utamaduni Wakufuatilia Chimbuko La Mambo Usiwe Mpokeaji Wamwisho!Mtoa Mada Kaelezea Vizuri Ila Wewe Ndo Walewale Waliomezeshwa,unatia Aibu Ndugu!
 
Back
Top Bottom