MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Kambi ya upinzani Tanzania haijifunzi kila baada ya Uchaguzi Mkuu kutokana na makosa yao!
The opposition has been the architects of their own downfall. Kansa inayowasumbua wapinzani ni ubinafsi na unafiki.
Kuanzia mwaka 1995, kambi ya upinzani imekuwa ikitengana au kupigana vijembe ndani ya bunge. Hata kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni imekuwa ni suala gumu kutokana na ubinafsi au unafiki.
Tulishuhudia kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, CUF waliamua kuungana na UDP pekee kilichokuwa na wabunge watatu tu ili kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni na kuvitenga vyama vya NCCR Mageuzi (kilichokuwa na wabunge 24) na CHADEMA (kilichokuwa na wabunge 4).
Mwaka 2000-2005, tulishuhudia CUF wakila matapishi yao kwa kuwaalika wabunge wa vyama vingine kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni kwa sababu ya kubanwa na kanuni na sio matakwa yao. Kwa maana nyingine, kambi rasmi ya upinzani haikuwa na dhamira ya kweli katika umoja bungeni.
Mwaka 2010 ilikuwa ni zamu ya CHADEMA baada ya kupata wabunge wengi. Kamati Kuu ya CHADEMA iliagiza/kuelekeza kuwa Freeman Mbowe aunde Kambi Rasmi ya upinzani bungeni bila kuvishirikisha vyama vingine vya upinzani kwa sababu kanuni zinawaruhusu. CHADEMA waliamua kuunda serikali kivuli bila kuvishirikisha vyama vingine vya upinzani.
Makosa ya CHADEMA ya kutokushirikisha vyama vingine yalikuja kuonekana baada ya miaka minne baada ya kuanzishwa kwa Bunge Maalum la Katiba huku wakichagizwa/kusukumwa na kuwepo mtafaruku mkubwa wa kiuongozi ndani ya CHADEMA ambao ulipelekea Zitto na kundi lake kufukuzwa ndani ya CHADEMA.
Makosa yao walijaribu kuyarekebisha kwa kuvialika vyama vingine viwili(CUF na NCCR-Mageuzi) ili kuunda Serikali Kivuli huku wakivitenga vyama vya TLP na UDP.
Makosa yaleyale ambayo chanzo chake ni ubinafsi na unafiki yamejitokeza katika Uchaguzi Mkuu 2015. Wabunge wa upinzani wamefanya kila linalowezekana ili kuhujumiana katika nafasi mbali mbali za Kamati za Kudumu za Bunge.
Baadhi ya wabunge walifanya kila linalowezekana kwa Spika ili kuhakikisha Zitto hapangwi katika kamati(LAAC na PAC) ambayo walidhani itampatia umaarufu ndani na nje ya bunge.
Spika akautumia ubinafsi na unafiki wa wabunge wa upinzani kukamilisha ajenda zake ambazo ziko ndani ya Kanuni za Bunge. Badala ya kutompanga Zitto pekee katika kamati ya LAAC au PAC, akaamua kutowapanga wabunge wote katika Kamati ambazo walikuwa wanazitumikia katika Bunge la 10.
Maamuzi ya Spika yaliwafanya wakose wote, kitu ambacho hawakutegemea wale ambao walikuwa wanachochea na kutaka Zitto asipangwe katika Kamati ya PAC au LAAC.
Msiba wa kisiasa ukawafika wote na kwa umoja wa kinafiki wameanza tena kulalamika kuhusu mpangilio wa Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge. Too late!
Waingereza wanasema, Where there is trouble, that is the place for a rupee!