Unafiki matamasha ya kuombea amani nchi

Unafiki matamasha ya kuombea amani nchi

Hakuna ubaya yoyote kuombea amani. Biblia inasema misingi ikiharibika wenye haki watafanya nini? Sisi kama wenye haki tunapaswa kwenda kwa Mungu kwa njia ya toba kwa ajili ya maovu yote yalipaswa kufanyika na yanayoendelea kufanyika. Tunapaswa kumuomba Mungu aingilie kati utawala wote na mfumo wote wa nchi, pia haki itendeke kwenye uchaguzi mkuu.

Kuchangia siyo pia jambo baya, kumbuka kuna gharama kubwa za kuwalete waimbaji kutoka nje ya nchi. Kumbuka Mungu huwa anaketi katika sifa za watu wake, ni jambo jema pia kuwashirikisha waimbaji kwa ajili ya kumtukuza Mungu. Kumualika mkuu wa nchi siyo jambo baya, kumbuka taifa huwa linaweza kukuosa kibali mbele za Mungu mkuu wa nchi akienda kinyume na mapenzi ya Mungu. Pale rais anakwenda kama mkuu wa nchi na siyo mwenyekiti wa chama. Kumbuka pia ni jambo jema mbele za Mungu watu kukusanyika kwa umoja na kunyenyekea mbele zake kwa ajili ya kulilia taifa lao. Sidhani kama itakuwa vyema kumualika mgombea yoyote, ila kwasababu rais ni kiongozi wa nchi hakuna ubaya.

Biblia inasema katika 2 nyakati 7:14, watu wa Mungu wakiomba na kumlilia Mungu yeye husikia na kuiponya nchi yao. Sisi tunapaswa kulia mbele za Mungu aingilie kati ili haki itendeke. Maombi ndiye silaha yetu tu. kumbuka sisi hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili bali katika roho. Hatupaswi kutukana, wala kulalamika sana, silaha yetu ya kwanza lazima iwe ni sala na maombi. Lazima tuelewe kila kitu kinaanzia kwenye ulimwengu wa roho, tusipoomba haki haitaweza kutendeka kwenye uchaguzi mkuu, hata tupige kelele vipi. Hebu tummlie Mungu yeye aingilie kati, na kugeuza mioyo ya watendaji wote wa NEC, wasisimazi wa uchagizi, na pia mwenyeketi wa tume. Shalom!!!!
 
Ni lini matamasha ya kuombea HAKI yatafanyika hapa nchini??

chief, tamasha la kuombea uchaguzi lililofanyika jana kwenye uwanja wa Uhuru (shamba la bibi) askofu Nguvumali wa Kanisa la Moravian Tanzania (ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi) alisema bila kumung'unya maneno kuwa "PASIPO HAKI HAKUNA AMANI".

aliwataka Watanzania waombee haki kwanza ili amani itamalaki.
 
Huyu Msama na genge lake ni wachumia matumbo (kiingilio cha nini? Au sadaka? wasiokuwa na hela hawataki amani?), kujipalilia makuu kisiasa na kutafuta umaarufu wa chee. Wasitufanye watanzania sote wajinga. Tamasha lake la Pasaka mgeni rasmi Membe na sasa kabuni tamasha mgeni rasmi Rais Kikwete. Gazeti lake Dira liko mstari wa mbele kuuponda upinzani na mgombea wao uRAIS Lowasa. Ni bora awe muwazi aache kutumia mgongo wa imani za dini na mungu kuendeleza agenda zake kuwapigia debe CCM na watawala. Tunatarajia TRA wafuatilie miradi hii.
 
Haya makundi ya wakristo wanafiki wanajidhalilisha sana! Ndiyo maana siku hizi wanaitwa WASANII sawa na comedy wengine!!

Wanautumia ukristo vibaya kwa kufanya biashara haramu kwa kutumia jina la Mungu!!!
 
Matamasha ya Amani kiila siku wanaoalikwa ni CCM peke yao maana yake ni kuwa vyama vingine ndivyo vinavyovuruga amani? Kuna Mantiki gani kuamini kuwa Kikwete anataka amani kwenye uchaguzi huu? Halafu amani inaombewa wakati wa uchaguzi tu?

Tafsiri ya amani kwa hao waandaaji inatia ukakasi akilini!!
NI fund rising ya CCM
 
Taifa linajazwa hofu ya kuvunjika kwa amani kwa maslahi ya watu wachache.

Badala ya kuwachukulia hatua watu wanaohusika na kauli na vitendo ambavyo vinaweza kuwa chanzo cha kuvunjika amani tunalijaza hofu taifa zima kwa matamasha, makongamano, mihadhara, na mikutano ya kuliombea taifa amani. Tunafanya mambo ya jumlajumla kwanini wakati wahusika wanafahamika? Huu ni unafiki mkubwa.

Watu wanaofanya kampeni za kikabila majukwaani kwa kusalimia na kuongea kikabila wanafahamika, watu wanaotukana wenzao majukwaani wanafahamika, watu wanaotoa kauli za kichochezi wanafahamika, watu wanaogombea wakiwa bado ni mawazi wanafahamika, watu wanaofanya kampeni za kidini wanafahamika, na watu wanaopanga kuiba kura wanafahamika, badala ya kuwafuata wahusika moja kwa moja na kuwaonya waache mara moja vitendo hivyo nyiye unaandaa matamasha ya kwenda kuimba nyimbo za kuliombea taifa amani. Tunamdhihaki Mungu? kwani huko ambako amani zao zimevunjika hakuna Mungu? tena kule Libya, Misri, Somalia, Syria na Iraq ndo wanakosali sana kuliko sisi, na hata mitume yetu mingi imeshawahi kukanyaga kwenye ardhi za baadhi ya nchi hizo. Mnatafuta pesa au mnamaanisha kuombea nchi amani, hebu acheni unafiki wenu, tungeni nyimbo (kama mnaweza) za kuwataja woote kwa majina wale watakaohatarisha amani yetu kwa kauli na vitendo vyao.

Hata wajumbe wa NEC, msajili wa vyama, polisi, masheikh, na maaskofu wanaongelea amani ya nchi kwa ujumlajumla tu kana kwamba nao hawawasikii wala kuwaona wanaohatarisha amani yetu. Amani ikivunjika tutalia na ninyi kwa ama unafiki wenu pia, au kutochukua hatua, bora mimi nimeandika kama sehemu ya mchango wangu wa kuelekea kudumisha amani.

NI kweli ndugu, ila Jua nchi kwa sasa haina Raisi. Inajiendea tu. Kuna watu wanajifanyia wajuacho . NCHI ingekuwa na Raisi ndio wakati wake wa kukemea maovu na kauli mbaya. ILA kuna kitu kama Raisi Lakini ni mfano to kama Ceremonial figure. We don't have the realy president.

Raisi ambaye kauli za bao la mkono anazienzi unadhani hapo Tuna mkuu wa nchi.ndio Maana viongozi wengi wameshaliona hili that's why wana seek gorvenance from God.
 
Asante mleta uzi.....umeugusa moyo wangu.......

Nmependa pia huyo askofu aliyesema wazi kuombea HAKI itendeke then AMANI....Tunataka kuona Tume ya uchaguz\i ikiweka uwazi wa kutosha ktk mchakato wa uchaguzi na kutangaza matokeo.....hatutaki rais anayetangazwa baada ya siku tano na matokeo ya kura zake yakiwa hayajulikani....tulilivumilia hilo 2010....miaka kimi baadae kurudia kosa lilelile nizaidi ya uendawazimu....Mungu hawezi kufumbia macho maombi ya kinafiki hati wezi wachache wanedelee kuliimbia taifa..NO!....No!....NO!

Ni busara za tume zitatuvusha salama.....lakini pia wakikosea wao waadhibiwe wao....tusilingize taifa ktk sintofahamu kwa malengo yakundi dogo...
 
Hata mmi huwa nashangaa, unasikia watu wanaanda matamasha ya kuombea nchi amani badala ya kusisitiza haki itendeke. Ni vyema viongozi wetu wa dini wakaandaa matamasha ya kuombea haki itendeke na wale wote wanaofanya kinyume tabia hizo zikasemwa hadharani badala ya kujificha kwenye kichaka cha amani. Amani ni tunda la haki ni nini kinachowafanya washindwe kuhubiri haki? Unahubiri amani wakati unaona haki haitendeki na umekaa kimya, kisa mvunja amani unamuogopa. Wote tunataka amani ila haki ndio msingi wake basi. Ama wenzetu matamasha haya mnayowatia watu hofu yanawasaidia kukusanya hela kwa njia ya sadaka nini?

Ndugu yangu, hapo hakuna cha dini..ni siasa tu. wewe haushangai haya mambo yanaandaliwa na promota na si viongozi wa dini? Hata mgeni rasmi si askofu wala mchungaji yeyote, ni Kikwete. Humo wamo akina Rose Mhando ambaye alitangaza anataka kuachana na ukristo arudi uislamu kwa kuwa anakosa raha huko aliko (ulokoleni),...shabiki wa mauno ya H-Baba...hayo maombi yatajibiwa na Mungu yupi? Hilo ni tamasha la muziki tu na lengo kuu ni kupiga pesa tu. Mnaalika waimbaji wa nje kuja kuiombea amani au kuimba maneno 'amani'? Kama ni kuliombea taifa amani kwa nini wakusanyane waimbaji na si waombaji? waimbaji wengine yawezekana hata kuomba hawajui...
 
Taifa linajazwa hofu ya kuvunjika kwa amani kwa maslahi ya watu wachache.

Badala ya kuwachukulia hatua watu wanaohusika na kauli na vitendo ambavyo vinaweza kuwa chanzo cha kuvunjika amani tunalijaza hofu taifa zima kwa matamasha, makongamano, mihadhara, na mikutano ya kuliombea taifa amani. Tunafanya mambo ya jumlajumla kwanini wakati wahusika wanafahamika? Huu ni unafiki mkubwa.

Watu wanaofanya kampeni za kikabila majukwaani kwa kusalimia na kuongea kikabila wanafahamika, watu wanaotukana wenzao majukwaani wanafahamika, watu wanaotoa kauli za kichochezi wanafahamika, watu wanaogombea wakiwa bado ni mawazi wanafahamika, watu wanaofanya kampeni za kidini wanafahamika, na watu wanaopanga kuiba kura wanafahamika, badala ya kuwafuata wahusika moja kwa moja na kuwaonya waache mara moja vitendo hivyo nyiye unaandaa matamasha ya kwenda kuimba nyimbo za kuliombea taifa amani. Tunamdhihaki Mungu? kwani huko ambako amani zao zimevunjika hakuna Mungu? tena kule Libya, Misri, Somalia, Syria na Iraq ndo wanakosali sana kuliko sisi, na hata mitume yetu mingi imeshawahi kukanyaga kwenye ardhi za baadhi ya nchi hizo. Mnatafuta pesa au mnamaanisha kuombea nchi amani, hebu acheni unafiki wenu, tungeni nyimbo (kama mnaweza) za kuwataja woote kwa majina wale watakaohatarisha amani yetu kwa kauli na vitendo vyao.

Hata wajumbe wa NEC, msajili wa vyama, polisi, masheikh, na maaskofu wanaongelea amani ya nchi kwa ujumlajumla tu kana kwamba nao hawawasikii wala kuwaona wanaohatarisha amani yetu. Amani ikivunjika tutalia na ninyi kwa ama unafiki wenu pia, au kutochukua hatua, bora mimi nimeandika kama sehemu ya mchango wangu wa kuelekea kudumisha amani.

MUNGU anatushangaa sana jinsi tulivyo wapumbavu eti tunaomba Amani badala ya kumwita kikwete, Mkapa,Bulembo,Nape na Jeshi la polisi kuwafokea hadharani bila kuwaonea aibu wala kujali nafasi zao na hapo tukimwomba MUNGU ATASIKIA TU,na sio unafiki wa kuomba AMANI TUNAOUFANYA wakati wanaotoa kauli za kuvunja amani tunawaona.
 
Hakuna ubaya yoyote kuombea amani. Biblia inasema misingi ikiharibika wenye haki watafanya nini? Sisi kama wenye haki tunapaswa kwenda kwa Mungu kwa njia ya toba kwa ajili ya maovu yote yalipaswa kufanyika na yanayoendelea kufanyika. Tunapaswa kumuomba Mungu aingilie kati utawala wote na mfumo wote wa nchi, pia haki itendeke kwenye uchaguzi mkuu.

Kuchangia siyo pia jambo baya, kumbuka kuna gharama kubwa za kuwalete waimbaji kutoka nje ya nchi. Kumbuka Mungu huwa anaketi katika sifa za watu wake, ni jambo jema pia kuwashirikisha waimbaji kwa ajili ya kumtukuza Mungu. Kumualika mkuu wa nchi siyo jambo baya, kumbuka taifa huwa linaweza kukuosa kibali mbele za Mungu mkuu wa nchi akienda kinyume na mapenzi ya Mungu. Pale rais anakwenda kama mkuu wa nchi na siyo mwenyekiti wa chama. Kumbuka pia ni jambo jema mbele za Mungu watu kukusanyika kwa umoja na kunyenyekea mbele zake kwa ajili ya kulilia taifa lao. Sidhani kama itakuwa vyema kumualika mgombea yoyote, ila kwasababu rais ni kiongozi wa nchi hakuna ubaya.

Biblia inasema katika 2 nyakati 7:14, watu wa Mungu wakiomba na kumlilia Mungu yeye husikia na kuiponya nchi yao. Sisi tunapaswa kulia mbele za Mungu aingilie kati ili haki itendeke. Maombi ndiye silaha yetu tu. kumbuka sisi hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili bali katika roho. Hatupaswi kutukana, wala kulalamika sana, silaha yetu ya kwanza lazima iwe ni sala na maombi. Lazima tuelewe kila kitu kinaanzia kwenye ulimwengu wa roho, tusipoomba haki haitaweza kutendeka kwenye uchaguzi mkuu, hata tupige kelele vipi. Hebu tummlie Mungu yeye aingilie kati, na kugeuza mioyo ya watendaji wote wa NEC, wasisimazi wa uchagizi, na pia mwenyeketi wa tume. Shalom!!!!
Kwa nini tuombe kwa Mungu nyumba isiungue badala ya kuzima kwa mikono yetu wenyewe cheche za moto tunazoziona kwa macho yetu ya nyama kabla hazijageuka kuwa moto mkubwa? Unataka kutushawishi kwamba tunapoona dalili za moto kutaka kuunguza nyumba zetu sisi tupige magoti na kuanza kuombea moto usiwake na nyumba isiungue. Huo sio uhalisia, uhalisia ni kuzima cheche kisha kumshukuru Mungu kwa nyumba kupona na moto. Baada ya kupata ajali ya gari iliyosababishwa na mwendokasi, abiria waliojeruhiwa ndo wanasema namana gari lao lilivyokuwalikiendeshwa kwa kasi kubwa, lakini kabla ya ajali walikuwa wengine wakifurahia wanavyopita magari mengine barabarani na wengine wakiombea safari iwe salama bila kumwambia dereva punguza mwendo. Tuwataje na kuwakemea kwa nguvu kwa midogo yetu ya kibinadamu wale vyanzo vya kuvunjika kwa amani, ndipo tuje tufanye matamasha ya kumshukuru Mungu kwa kuiponya nchi yetu na vurugu.
 
Back
Top Bottom