Unafiki matamasha ya kuombea amani nchi

Unafiki matamasha ya kuombea amani nchi

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,253
Reaction score
16,171
Taifa linajazwa hofu ya kuvunjika kwa amani kwa maslahi ya watu wachache.

Badala ya kuwachukulia hatua watu wanaohusika na kauli na vitendo ambavyo vinaweza kuwa chanzo cha kuvunjika amani tunalijaza hofu taifa zima kwa matamasha, makongamano, mihadhara, na mikutano ya kuliombea taifa amani. Tunafanya mambo ya jumlajumla kwanini wakati wahusika wanafahamika? Huu ni unafiki mkubwa.

Watu wanaofanya kampeni za kikabila majukwaani kwa kusalimia na kuongea kikabila wanafahamika, watu wanaotukana wenzao majukwaani wanafahamika, watu wanaotoa kauli za kichochezi wanafahamika, watu wanaogombea wakiwa bado ni mawazi wanafahamika, watu wanaofanya kampeni za kidini wanafahamika, na watu wanaopanga kuiba kura wanafahamika, badala ya kuwafuata wahusika moja kwa moja na kuwaonya waache mara moja vitendo hivyo nyiye unaandaa matamasha ya kwenda kuimba nyimbo za kuliombea taifa amani. Tunamdhihaki Mungu? kwani huko ambako amani zao zimevunjika hakuna Mungu? tena kule Libya, Misri, Somalia, Syria na Iraq ndo wanakosali sana kuliko sisi, na hata mitume yetu mingi imeshawahi kukanyaga kwenye ardhi za baadhi ya nchi hizo. Mnatafuta pesa au mnamaanisha kuombea nchi amani, hebu acheni unafiki wenu, tungeni nyimbo (kama mnaweza) za kuwataja woote kwa majina wale watakaohatarisha amani yetu kwa kauli na vitendo vyao.

Hata wajumbe wa NEC, msajili wa vyama, polisi, masheikh, na maaskofu wanaongelea amani ya nchi kwa ujumlajumla tu kana kwamba nao hawawasikii wala kuwaona wanaohatarisha amani yetu. Amani ikivunjika tutalia na ninyi kwa ama unafiki wenu pia, au kutochukua hatua, bora mimi nimeandika kama sehemu ya mchango wangu wa kuelekea kudumisha amani.
 
Upo sahihi sana mkuu,Mimi nilishagundua tu na hao wapo kimaslahi tu...na Mungu anachukia sana UNAFIKI,ila TUTAMCHAGUA LOWASSA,na naamini atasolve hilo.
 
Msama project ndugu yao na Ruge na Kusaga the same deal huku Msama promotion kule fiesta.Huku praise power ma wapo radio kule clouds fm ndo hutumika kwenye hizi dili za kinyonyaji.
 
Ni kweli kiongozi haràfu eti kiingilio ni 5000 na 3000, sasa kama ni kuombea amani kiingilio ni cha nini na kwa nini mgeni rasmi ni mwenyekiti wa ccm?
 
Hapooo umenena kunausanii flani unafanyika ambao sio poaa kiukwelii na kuwabaminisha wanainchi kuwa their is something bigg kitatokea kumbe wale wale
 
Hata mmi huwa nashangaa, unasikia watu wanaanda matamasha ya kuombea nchi amani badala ya kusisitiza haki itendeke. Ni vyema viongozi wetu wa dini wakaandaa matamasha ya kuombea haki itendeke na wale wote wanaofanya kinyume tabia hizo zikasemwa hadharani badala ya kujificha kwenye kichaka cha amani. Amani ni tunda la haki ni nini kinachowafanya washindwe kuhubiri haki? Unahubiri amani wakati unaona haki haitendeki na umekaa kimya, kisa mvunja amani unamuogopa. Wote tunataka amani ila haki ndio msingi wake basi. Ama wenzetu matamasha haya mnayowatia watu hofu yanawasaidia kukusanya hela kwa njia ya sadaka nini?
 
hivi maana ya chagadema/UKAWA ni kupinga kilakitu?
 
mungu hadhihakiwi msing wa aman ni haki hata mungu huyo wa wana wa israel aliwadhibu israel kwa dhambi za viongoz kwa kuvamiwa na kutawaliwa take care tanzanian leaders especialy ccm
 
uko sahihi kabisa kwani watumishi wa Mungu moja ya kazi zao ni kukemea maovu na viashiria vya uvunjifu wa amani na sio kuomba kila kitu hata ambacho kinaonekana wazi mkolofi ninani hakika amani ya nchi hii ikivunjika tutalia nao
 
Ni kweli kiongozi haràfu eti kiingilio ni 5000 na 3000, sasa kama ni kuombea amani kiingilio ni cha nini na kwa nini mgeni rasmi ni mwenyekiti wa ccm?

watu wazima weny akili na viongoz wa dini hili halipaswa kupita hv likemewe vikali. natoa wito roman catholic, waluther, makanisa ya pentecoste waislamu kwa ujumla wetu tukemee jambo hilo
 
Hakuna upuuzi kama haya maigizo ya kuombea amani,hiyo ni tecnic za kupinga dili na uzinzi tu. Amani kila unaposali nyumbani kwako ni sala tosha sana.
 
Hahahaa wapinzan kirakitu nikupinga tuu

Hapa suala sio wapinzani bali ni hii hofu mnayowajengea wananchi ili muishie kula hela zao kama kiingilio. Kama ni amani mbona wanaokiuka sheria wanaonekana, wanaotaka kuacha kutenda haki wote wako wazi. Acheni kutaka kuiba hela za wananchi kwa kisingizio cha kutafuta amani bwana. Ama ndugu yetu na wewe umeandaa tamasha sasa unaona wajinga wanastuliwa nini!!
 
Amani:wanaotamka neno hili wao ndo wanatoa kauli za kichochezi,siasa chonganishi,kujiona wao ndo waTanzania pekee ,na sie tunaihitaji hiyo amani.kila mmoja atimize wajibu wake.tunataka sera,wakutoa alert ya kuvunjw kw amani ni vyombo vya usalama nchini.sio vyama vya siasa.
 
Ni kweli kiongozi haràfu eti kiingilio ni 5000 na 3000, sasa kama ni kuombea amani kiingilio ni cha nini na kwa nini mgeni rasmi ni mwenyekiti wa ccm?
Hiyo ni harambee ya kuichangia CCM pesa za kampeni na kiasi kinaingia mifukoni mwa waandaaji, malofa na wapumbavu kazi kwenu.
 
Matamasha ya Amani kiila siku wanaoalikwa ni CCM peke yao maana yake ni kuwa vyama vingine ndivyo vinavyovuruga amani? Kuna Mantiki gani kuamini kuwa Kikwete anataka amani kwenye uchaguzi huu? Halafu amani inaombewa wakati wa uchaguzi tu?

Tafsiri ya amani kwa hao waandaaji inatia ukakasi akilini!!
 
safi sana ndugu yangu kwa kuandika facts. Tatizo nchi hii kila kitu ni siasa, wanataka kumfanyia siasa hata Mungu. Ni wazi kuwa amani hupatikana pale tu haki inapotendeka, sasa kwa nini watanzania wakiwemo watumishi wa Mungu hawalioni hili? Haiitaji elimu yeyote kujua kuwa tunda la amani ni haki na amani huzaa upendo. Hivi ni kweli watanzania hatuoni kauli za uvunjivu wa amani zinazoendelea majukwaani? Kwa nini basi hatuzikemia kwa kuwataja majina waziwazi? Tatizo hapa ni nini? Mungu ametupata akili tuzitumie basi.
 
Back
Top Bottom