Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,288
Unafki mwingine bwana...
Limtu tuko nalo hapa hapa mtaani
kwetu. Kipindi kile kafa Mzee
Mwakilembe ilikuwa kimya kimya,
lahaula fil-aiti, tukakutana kwenye
kuaga maiti, kipindi fulani akatutoka kijana mwenzetu Tito, nikamgumia msibani wakati nampa sinia la ubwabwa (nilikuwa mwandazi), haya kipindi kile akafariki jirani yangu Sophia... namtext ananiambia atachelewa kuzika anaenda Magomeni kuna kibeseni shoga yao amejifungua.
Picha halijaisha hapo, akafariki alwatan Mzee Shaaban Irembe, kimya kimya tulionana kwenye kisomo msikiti mkubwa... Alivyodondoka Tina si nikajua atanipa taarifa kwa kuwa wamesoma wote, ebwana tulionana Mwembejini tukigombania usafiri wa
kurudi.
Leo kafa Sharo Milionea (hata sijui kama walishaonana na huyu kiumbe) usiku nimelala ananipigia simu, sauti anaisikia kabisa ya usingizi, afu aniuliza "Eti Sharo amefariki kweli?", jamani usiku
huu mie tajuaje? Halafu misiba yote
Mikocheni hukuguswa mpaka hii ya mastaa?
Kipindi kile cha Marehemu Kanumba ulifanya hivi hivi, nikakukaushia... Ona sasa umeniharibia usingizi wangu, na
utaulipa nakuambia!