Unafanya nini cha tofauti?

jns

Member
Sep 5, 2019
11
5
Habari ya wakati huu, poleni na hongereni pia na harakati za kila siku na nawatakia heri na pongezi za msimu huu wa sikukuu

Uzi huu uko inspired na nyuzi mbali mbali kutoka hapa jf, lakini zaidi ni kazi ya kaka yangu Walec inayokwenda kwa jina 'ulianzaje kuishi gheto', Binafsi napenda sana mazingira ya ninapoishi yawe mazuri kwa maana ya usafi, mpangilio na muonekano kwa ujumla, na hapa ndipo lengo kuu la kuanzisha uzi huu linapokuja

Kuna taratibu nyingi au vitu vingi sana ambavyo ni vidogo lakini vinaongeza sana thamani ya majumbani au maghetoni kwetu, mfano mimi kupitia wadau mbalimbali nimejifunza baadhi ya vitu kama utaratibu wa kutembea na viatu vya ndani niwapo gheto kwangu na zaidi kuwa na pair kwa ajili ya mgeni yeyote ambaye anapata wakati wa kuja kunisalimu, sambamba na hilo pia nimejifunza kuhusu utaratibu wa kuwa na tissue ziwepo mezani kwa ajili ya matumizi ya kawaida lakini pia kuna taratibu kama za kuweka picha au saa ukutani, Na pia kuna wale wanaopenda kuzungushia urembo wa vitaa kwenye tv au stand za viatu au kitanda na naona inapendezesha sana

Hayo ni baadhi ya mambo ambayo huenda yamezoeleka kufanyika majumbani na sio maghetoni au ambayo ni kama sio ya ulazima lakini yanaongeza sana muonekano na thamani ya tunapoishi, share nasi taratibu gani unayo au nini unacho gheto au nyumbani kwako ambacho huenda ni kidogo au kikubwa lakini kinaongeza muonekano au thamani ya gheto au nyumbani kwako ili nasi tuweze kujifunza

Nimeona ni vema pia kuwajumuisha wale wa majumbani kwasababu naamini yapo mengi ya kujifunza ambayo huenda yakawa na matumizi maghetoni au hata kama ni maalumu kwa majumbani tu basi kwa sisi wa maghetoni yakawa na msaada hapo mbeleni
images.jpeg
 
Naona wakubwa wamegoma kushusha nondo zao, tupeni maujanja wakubwa tuboreshe maeneo yetu
 
Naona wakubwa wamegoma kushusha nondo zao, tupeni maujanja wakubwa tuboreshe maeneo yetu
Humu JF asilimia kubwa wanaishi kwa shemeji zao, yaani walikoolewa dada zao . Na hizi likizo wako busy kunyang'anyana remote na wapwa zao vijunior
 
Humu JF asilimia kubwa wanaishi kwa shemeji zao, yaani walikoolewa dada zao . Na hizi likizo wako busy kunyang'anyana remote na wapwa zao vijunior
Aah! Mbona kama jiwe umelitupa gizani hivi😁, sa si watakuja kukudisi kuwa we ambaye huishi kwa shemeji mbona hushushi nondo waprove wrong kabisa sasa teremsha madini hayo
 
Sahihi kabisa,na asubuhi hakikisha Gari yake inaoshwa kabla ya hajaenda kazini na uwe unawachekesha chekesha watoto wake kila Mara.
Na hakuna kitu kinakosha kama watoto wake kukukubali hapo una uhakika wa ugali
 
Nimesoma lakini sielewi
Tushirikishe ni utaratibu upi unao au pengine kitu kipi unacho mahali unapoishi ambao au ambacho kinaongeza muonekano mzuri hata marafiki wakija wanakuwa wowed na kutamani kuiga pia
 
Back
Top Bottom