Unabii wa Tundu Lissu unaosubiriwa kuitikisa Tanzania

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,738
15,211
Makamu mwenyekiti wa Chadema Tundu Lisu ameshauriwa kama mtu mzima aombe msamaha kwa watanzania kwani mtu mzima akivuliwa nguo huchutama na siyo kukimbia uchi.

Ni miaka sita sasa tangu Tundu Lisu aitabirie Tanzania mabaya ikiwemo kushitakiwa MIGA , ndege kukamatwa, uchumi kufilisika, kunyimwa misaada mbalimbali.

Mpaka sasa hakuna hata kitu kimoja kilichotabiriwa na Lisu kilichotimia maaana yake aliwadanaganya watanzania, yani licha ya kusoma kwa kodi za watanzania yeye anakuja kufanya kazi ya kuwadanganya watanzania

Kinyume na utabiri wa Lisu ,Tanzania ya sasa imeingia uchumi wa kati, hatujashitakiwa MIGA na viwanda vya kuchenjua dhahabu vimejengwa Mwanza.

Mapato ya madini yamepanda kutoka billioni 100 hadi billion 500, ndege hazikamatwi na watanzania ni wamoja zaidi kinyume na utabiri wake.

Baada ya kuona aibu Tundu Lisu na Lema badala ya kuwaomba msamaha watanzania wao wamekimbilia Ulaya kwenda kulishwa bure na wazungu.

Lema na Lisu rudini nyumbani muwaombe msamaha watanzania muanze kuishi kwa jasho lenu kwa kufanya kazi na siyo kulelewa.
 
Mwanasiasa mwenye msimamo hapa tanzania ni MBOWE TU mpaka Sasa hakuna mwngne , mbowe KWA alivoharibiwa mali, fitna alizofanyiwa, na ahadi alizopewa akisaliti chama angekuwa mwngne angeshawapga chin watu wake.

Over
 
Kuna kampuni nyingi sana zimeishitaki Tanzania kuhusu kuvunja mikataba nimesoma sehemu mbalimbali moja inaitwa Indiana polisi ya USA cjajua waliishia wapi !!!
Nina uhakika watatushitaki achana na mzungu hakurupuki akiibuka utapigwa tuu
 
2024 sasa 😂
 
Makamu mwenyekiti wa Chadema Tundu Lisu ameshauriwa kama mtu mzima aombe msamaha kwa watanzania kwani mtu mzima akivuliwa nguo huchutama na siyo kukimbia uchi.

Ni miaka sita sasa tangu Tundu Lisu aitabirie Tanzania mabaya ikiwemo kushitakiwa MIGA , ndege kukamatwa, uchumi kufilisika, kunyimwa misaada mbalimbali.

Mpaka sasa hakuna hata kitu kimoja kilichotabiriwa na Lisu kilichotimia maaana yake aliwadanaganya watanzania, yani licha ya kusoma kwa kodi za watanzania yeye anakuja kufanya kazi ya kuwadanganya watanzania

Kinyume na utabiri wa Lisu ,Tanzania ya sasa imeingia uchumi wa kati, hatujashitakiwa MIGA na viwanda vya kuchenjua dhahabu vimejengwa Mwanza.

Mapato ya madini yamepanda kutoka billioni 100 hadi billion 500, ndege hazikamatwi na watanzania ni wamoja zaidi kinyume na utabiri wake.

Baada ya kuona aibu Tundu Lisu na Lema badala ya kuwaomba msamaha watanzania wao wamekimbilia Ulaya kwenda kulishwa bure na wazungu.

Lema na Lisu rudini nyumbani muwaombe msamaha watanzania muanze kuishi kwa jasho lenu kwa kufanya kazi na siyo kulelewa.
Mtoa mada utakuwa unaishi shimoni na uko peke yako. Yote hayo yameshatimia.
 
Makampuni wameshitakinna wamelipwa mfano ni Indianapolis mineral resources wamelipwa bil 231 za kitanzania hakika jiwe alikuwa wanhovyo
 
Back
Top Bottom