Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 5,527
- 7,121
Yesu alipokuwa akiwaeleza wanafunzi wake dalili za kuja kwake, na za mwisho wa dunia, alitamka maneno haya ya kinabii: “Na kwa sababu ya kuongezeka kwa maasi, upendo wa wengi utapoa.” (Mathayo 24:12). Huu ni unabii unaoeleza hali ya kijamii na ya kiroho itakavyokuwa duniani kabla ya kuja kwa Bwana Yesu Kristo.
Unabii huo tayari umetimia. Hebu tuuchambue kwa kifupi unabii huo.
1. Maasi kuongezeka – Kuna ushahidi gani kuwa maasi au maovu yameongezeka nyakati hizi? Leo tunaishi katika kizazi ambacho uasi au maovu dhidi ya Mungu na maadili mema, umepindukia. Labda utasema, "Ah, hata zamani watu walitenda maovu." Lakini ukweli ni kwamba maasi yameongezeka kwa sababu nyakati hizi kuna nchi zimehalalisha maovu na kuyapa kinga kisheria. Zamani, uzinzi, ushoga, na mimba za utotoni vilikuwa aibu na vilipigwa vita. Leo, uovu huo unatungiwa sheria za kuulinda?! Duh!
Haya, angalia tena jinsi maovu yanavyosambaa kwa kasi kwa njia ya mitandao. Sasa hivi, mtoto wa miaka 3 anaweza kupata maudhui machafu kwa simu bila hata mzazi kujua. Hali hii haikuwepo zamani.
Leo hii watu wanajivunia dhambi badala ya kutubu. Siku hizi watu wanajitangaza mitandaoni kwa kufanya mambo yasiyo ya haki—wanajiona mashujaa wa uovu.
Ukatili na uhalifu umeongezeka kwa kiwango cha kutisha. Miaka ya zamani, milango ya nyumba iliachwa wazi bila hofu. Leo, hata watu wakiwa ndani, wanafunga milango kwa makufuli matatu! Ripoti za uhalifu wa kikatili, mauaji ya kifamilia, ubakaji wa watoto wachanga, na hata ibada za kishetani—vimejaa kila kona ya dunia.
2. Upendo wa wengi kupoa
Siku hizi, upendo wa kweli wa kibinadamu na ule wa kumcha Mungu umepoa mno: Sio jambo la ajabu leo hii kuona wanandoa wanapeana talaka wiki moja baada ya kuoana kwa sherehe kubwa!
Zamani, majirani walikuwa kama familia. Leo, mtu anaweza kuugua hadi kufa chumbani kwake bila jirani kujua.
Watu hawasaidiani tena kwa moyo wa upendo.
"Kila mtu apambane na hali yake" ni usemi ulioanza hivi majuzi tu. Zamani, mtu alipokuwa na njaa, kijiji kilimhudumia. Leo, mtu akilia barabarani, wengi hupita bila kujali. Na wengine wanampiga picha za video badala ya kumsaidia. Gari likipata ajali, watu wanadiriki kusechi mifuko ya majeruhi ili wapate pesa badala ya kuokoa maisha ya majeruhi!
Tazama manabii wa uongo wanavyohubiri ili kupata pesa za kujaza matumbo yaotu. Mtu ana shida, anaumwa, lakini bado anakamuliwa hata kile kidogo alicho nacho kwa kuambiwa anunue eti chumvi na mafuta ya upako. Ni nini hiyo kama sio upendo kupoa?