Unaamini maneno ya Mtoto wa asilimia 100?

Mnyiramba

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2022
Posts
1,207
Reaction score
3,300
Hiki ni kisa cha kweli kabisa kimewahi kunitokea wakati nina umri wa miaka 6!
Ilikuwa hivi nilitoka nyumbani na Rafiki yangu kwa lengo la kwenda kucheza ilikuwa sio mbali sana na nyumbani,sasa yule Mtoto mwenzangu ambaye leo hii hata simkumbuki vizuri alikuwa ni nani yeye ndio alikuwa aniniongoza tupite hivi,twende hivi hadi tukafika sehemu moja wanapaki malori,nilikuja kugundua ukubwani kuwa yalikuwa yanaitwa FIAT na yalikuwa yanaendeshwa na watu jamii ya wasomali!
Sasa tulivyofika pale dereva mmoja wa lori alivyotuona akatuita na sisi tukasogelea lori kwa uoga maana tulikuwa tunahisi kama tutaibiwa vile kwahiyo hofu ilikuwa kubwa sana!
Basi tukasogea kwa uoga pale tukasalimia shikamoo baba (akili za kitoto tena kila mtu mzima baba)
Basi yule dereva akaitikia hapo sisi tupo kwa chini yeye hajashuka hata kwenye gari yupo tu ndani ya gari!
Akaitikia tu vizuri akatoa ndizi pamoja na pesa ya noti kipindi hicho hata sijui ilikuwa na thamani gani akanipa mimi pamoja na yule Mtoto mwenzangu tukapokea!
Hapo hata hatukuaga tena mbio hadi nyumbani!
Lkn kabla hatujafika tukaulizana tukifika nyumbani tukiulizwa tumepewa na nani tutajibu Vipi!?
Yule Mtoto mwenzangu akasema tutasema tumepewa na baba mwingine!
Basi mbio hadi nyumbani tukamkuta baba amekaa pamoja na mama na wakati tunatoka baba hakuwepo!
Kwahiyo tulivyofika swali la kwanza tukaulizwa mlikuwa wapi?
Mimi nikajibu tulikuwa pale uwanjani wanapoosha magari,swali lingine hizo ndizi na pesa umepewa na nani?
Bila kusita nikasema nimepewa na baba mwingine!
Nikaona Baba hajasema chochote zaidi ya kumwangalia tu usoni kama alikuwa anatafakari kitu!
Lakini mimi kwa akili za kitoto sikuelewa chochote basi baba akaniambia kacheze lkn usiende mbali sasa hivi nitakuita nikasema sawa!
Sijui ni malumbano gani yaliendelea kati ya baba na mama muda si mrefu baba aliniita akaniambia twende ukanionyeshe huyo baba mwingine aliyekupa pesa!
Basi mimi mguu kwa mguu hadi ile sehemu tulipopewa pesa ila tulivyofika pale Tayari yale malori yalikuwa yameshaondoka kwahiyo hatuwakuta wale wasomali pale!
Basi tukarudi nyumbani siku hiyo ulizuka ugomvi mkubwa kati ya mama na baba siku hiyo kumbe chanzo ilikuwa ni mimi,eti Mtoto huwa hasemi uongo kuwa ni lazima mimi nilikuwa namuona huyo baba mwingine akiwa anakuja nyumbani wakati baba hayupo![emoji276]
Aisee utoto ni usiku wa giza!,tangia hapo baba na mama hawakuwahi kuwa na amani tena hadi walipokuja kutengana!
Na tangia hapo mzee akawa na mashaka kwamba mimi sio Mtoto wake!
N:B tusiamini maneno ya watoto kwa asilimia kubwa kwa kuamini kwamba Mtoto ni malaika huwa anasema kweli tu
 
Aaah watoto ni waongo wa kupindukia.. na watu wengi wanakosea sana kuamini kuwa watoto hawasemi uongo, tena bora watoto wa zaman, watoto wa kizazi hiki ndo majanga kabisaaaaa!!!
 
Watoto waongo kuliko kawaida asikuambie mtu yani ni hatari sana

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Jamaa alikuita tu wewe na mwenzio kisha akakupeni pesa! Seriously?
 
Attachments

  • 8184i-MV+SL.jpg
    8184i-MV+SL.jpg
    260 KB · Views: 19
Watoto hua hawasemi uwongo, wanakumbuka kile walichoona na siyo walichoambiwa kwenda kusema...
 
Ndugu yake Mwigulu 'chemba' hujamalizia stori bwana kilichosababisha kupewa elfu 1 na ndizi na bwana msomali. Au unataka tumalizie wenyewe?
 
Jamaa alikuita tu wewe na mwenzio kisha akakupeni pesa! Seriously?
Hii kitu inawezkana ujue watoto wengi wakiwa wanacheza Mara nyingi huchafuka na hua Kama machokoraa Sasa maybe dereva aliingiwa na huruma ndo akawapa japo wakale
 
Back
Top Bottom