una umri gani!!!?

john hotsam da1

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2012
Posts
396
Reaction score
79
habari za muda huu wakubwa kwa wadogo.leo hii in mara yangu ya kwanza kuanzisha topic hapa jukwaani tangu nimejiunga na jf,huwa napita hapa kiangalia yanayojiri kila siku na kukaa kimya ila leo nimeamua kutoa ya moyoni.
Katika jukwaa hili kuna sentensi moja ambayo ndani ya kila anayeomba ushauri hapa utaikuta.

UNA UMRI GANI!!??

mara nyingi swahi hilo huulizwa members wasio na majina hapa jukwaani,yaani members wasiojulikana sana hapa mmu.

utakuta member mwenye tittle-jf seneor expert member- anauliza swali kama hilo,je huo u-expert uko wapi.......binafsi naona hilo sio neno la busara kwa sababu zifuatazo..........

1.ninaweza sema nina miaka 30 kumbe 17 na hutojua kama ni uongo

2.umri wa mtu ni taarifa binafsi siyo matangazo kila mtu ajue(ni bora kuuliza rika)

3.mara nyingi wanaouliza miaka huwa hawatoi mchango wowote hata kama umri utatajwa(pitia topis utaamini)

4.hata kama mimi ni mtu mwenye miaka 45 ukitoa ushauri wako kwenye topic yangu,kila mtu hadi mtoto atausoma.

5.......

(n-2).....

(n-1).....

n

najua wapo watakao litazama jambo hili negatively na positively basi ukitaka ku - comment,comment kistaarabu

ahsante kwa kusoma
 
Naona umejisalimisha mwenyewe POLISI, una-UMRI gani? ili tujue tukuweke selo ya watoto au wakubwa.
 
mi nafikiri huwa mtu anaulizwa umri ili kupewa ushauri unaolingana na thinking capacity yake,mtu akidanganya umri kwetu sio tabu hilo ni juu yake mtu wa 20's hawezi kupewa ushauri sawa na mtu wa 50's.
 
mi nafikiri huwa mtu anaulizwa umri ili kupewa ushauri unaolingana na thinking capacity yake,mtu akidanganya umri kwetu sio tabu hilo ni juu yake mtu wa 20's hawezi kupewa ushauri sawa na mtu wa 50's.

Hapo umenena mdada.
 
Hapo umenena mdada.

ndo hivyo mkuu waweza kumpa mtu ushauri wa mtu wa 43yrs kumbe ni mtoto yuko form two,wakati mwingine mada zinapelekwa jukwaa la wakubwa kuepusha shari na mgongano wa maadili,suala la kuulizwa umri kwangu sio tatizo kabisa.
 
umeolewa?pengine unataka kufukuza golden chance,mwambie tu,
 
Maranyingi mnaulizwa umri kutokana na vitu mnavyo andika, utajikuta mwanaume inajisifu handsome or sijui dushele langu kubwa sijui nkatongozwa na mademu sasa tunauliza umri kwa kukushanga na wala hatutaki kujua age yako. Kama ishawahi kukutokea pole sana uwe unaandika kiutu uzima. Sawa dogo
by the way how old are u?
 
You don't have to answer that you know. Ni ngumu sana kuzuia au kupangia watu wabehave vipi.
 
Elimu yako pia huwa wanauliza hawa mbwiga

siyo hivyo unakuta mtu kapost kitu cha kijinga au coment isiyo na ustaarabu na katika kuulizwa umri siyo kwamba anataka kujua umri halisi bali kutaka kumrudisha mtu kwenye mstari na kumuonyesha kuwa ulichofanya siyo na hakilingani na umri wa mtu mwenye kuchambua baya na zuri siyo lazima mtu akuambie direct ila uwezo wako wa kulichambua ndo mwongozo
 

sawasawa
 

Nawe pia,ahsante kwa kuandika,samahan lkn UNA UMRI GANI??
 
Kwa Maswali yote ambayo yanayokuwa kama ya Kipima joto cha I.T.V huwa najibu Umri unausika ktk swali lako hivyo ukikua utapata jibu hivyo na wewe ukikua utajua kwanini ulianzisha haka kathread kako, maana kama ungejua wakati gani haya majibu hutoka basi usingejadili hili suala.
 
We mwenyewe una umri gani kwanza kabla hatujaendelea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…