Una uhakika gani kuwa "sasa hivi" Haupo ndotoni?

Mtoto Wabibi

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
451
294
Binadamu mara nyingi akikutana na jambo( kitu) la ajabu la kushangaza au kuhuzunisha sana kuna swali huwa anajiuliza hata mimi binafsi nimejikuta kama mara mbili hvi ikinitokea.

Swali: Hivi naota au?(akijiuliza yani nipo ndotoni au ndio real happen).
maswali naomba mnijibu:

1: Unawezaje kutofautisha kati ya ndoto na uhalisia?
zingatia: jambo unalofanya/linalotokea ndotoni halina tofauti na linalotokea katika hali halisi.
mfano: unaweza ota unapigwa na unalia na feelings zile zile utazipata ukiwa endapo utanapigwa live(sio ndotoni)

2: Una uhakika gani kuwa sasa hauoti ndoto hapo ulipo unaposoma hii thread?
maana hata ndotoni unaweza ukawa JF unasoma na kuandika thread.

3: Una uhakika gani kama jibu lako hilo ulilotoa ni sahihi na sio umetoa ndotoni sasa.
Ukitaka ufurahie maisha siku zote katika maisha yako, uwe unachukulia kila jambo ni ndoto ambayo unaweza kuiota utakavyo wewe. Stress zote za maisha zitakwisha na utakuwa huru.

Nakutakia undeleze hii ndoto yako njema unayoota unasoma thread yangu kumbe kiuhalisia hausomi.
 
Nihakikishie kwanza kwamba wewe haukua unaota wakati unaandika huu uzi.
Lazima uwe kwenye usingizi ndio utaweza kuota, Jibu moja la swali lako, SIJALALA.

lakini je ukiwa unaota huwa unajijua kuwa umelala? au hadi ndoto ikatize(iishe) ndio unakurupuka et kumbe ni ndoto
 
lakini je ukiwa unaota huwa unajijua kuwa umelala? au hadi ndoto ikatize(iishe) ndio unakurupuka et kumbe ni ndoto

Nihakikishie kwanza kwamba wewe haukua unaota ulipokua unaandika huu uzi, nimeshakujibu kwamba SIJALALA.
 
unawezaje kuota kama hujalala mkuu? kama hujitambui kuwa ulikuwa umelala au la utakuw kwenye hasara kubwa!
hivi pale unapoingia usingizini huwa unajitambua? au unajikuta tu umesinzia tu yani ghafla.
Niambie kitu cha mwisho jana kufikiri kabla hujalala na je ulianzaje kupoteza ufahamu wako hadi unasinzia.
kinachofanyika wewe unauandaa mwili tu katika mazingira ya kusinzia( kupoteza ufahamu) kama kujilaza n.k
Usingizi ukikubana haijalishi upo wapi utasinzia tu( utapoteza ufahamu) hata uwe umelala kwenye maji.
 
Basi kama hujitambui wala hujui ni nini mara ya mwisho kufikiri kabla hujasinzia na ndio hivyo huwezi kutofautisha ndoto na uhalisia.hivyo feelings zitakutesa sana ndotoni kama katika uhalisi.ndio maana huwezi kujizuia kuota
 
Binadamu mara nyingi akikutana na jambo( kitu) la ajabu la kushangaza au kuhuzunisha sana kuna swali huwa anajiuliza hata mimi binafsi nimejikuta kama mara mbili hvi ikinitokea.
swali: hivi naota au?(akijiuliza yani nipo ndotoni au ndio real happen).
maswali naomba mnijibu:
1: unawezaje kutofautisha kati ya ndoto na uhalisia?
zingatia: jambo unalofanya/linalotokea ndotoni halina tofauti na linalotokea katika hali halisi.
mfano: unaweza ota unapigwa na unalia na feelings zile zile utazipata ukiwa endapo utanapigwa live(sio ndotoni)
2: una uhakika gani kuwa sasa hauoti ndoto hapo ulipo unaposoma hii thread?
maana hata ndotoni unaweza ukawa JF unasoma na kuandika thread.
3: una uhakika gani kama jibu lako hilo ulilotoa ni sahihi na sio umetoa ndotoni sasa.
Ukitaka ufurahie maisha siku zote katika maisha .yako ,uwe unachukulia kila jambo ni ndoto ambayo unaweza kuiota utakavyo wewe.Stress zote za maisha zitakwisha na utakuwa huru.
Nakutakia undeleze hii ndoto yako njema unayoota unasoma thread yangu kumbe kiuhalisia hausomi.
Thread yako naiua kwa kusema kua utapata feelings zote lakini hutasikia physical pain kwenye ndoto hata siku moja.
Kwahyo hii sio ndoto sababu nimejifinya nikasikia maumivu makali ambayo kwenye ndoto hakuna.
 
Ndoto haina muendelezo wenye mpangilio wa matukio yanayoeleweka..
Huwezi kuota masaa zaidi ya(3) jambo mboja lenye muendelezo huohuo.
 
Ndoto haina muendelezo wenye mpangilio wa matukio yanayoeleweka..
Huwezi kuota masaa zaidi ya(3) jambo mboja lenye muendelezo huohuo.
sawa but you share the same feelings in both.
Uliwahi kuwa kwenye ndoto na ukatambua kuwa unaota? Thus why ikiwa ndoto ni nzuri baada ya kukurupuka utatamani uiendeleze lakin impossible. ndoto ni maisha ya rohoni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom