"Watoto wangu njooni,
Njooni niwaambie,
Maisha ya sasa,
Yamebadilika,
Tofauti na zamani.
Wakati wa ujana wangu,
Mimi Baba yenu,
Shati dukani,
Shilingi sita unapata,
Lakini sasa hivi,
Shilingi sita,
Hata soda haupati.
Kwa hiyo wanangu,
Muishi kuendana,
Na wakati.
Kwa hiyo wanangu,
Muishi kuendana,
Na wakati.