Una maoni yapi kuhusu haya aliyo yasema mtumishi?

papag

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
1,137
1,608
Asilimia kubwa ya wanawake waliopo kwenye ndoa wana Hofu..

Jana nilizungumza kuhusu changamoto zinazo mkabili mwanaume asiye na pesa,..

Leo nataka niongee kidogo kuhusu hofu inayoendelea miongoni mwa asilimia kubwa ya wanawake ambao tayari wako kwenye ndoa..

Ulimwengu wa sasa ni ulimwengu wa utandawazi ( globalisation) utandawazi umepelekea mapenzi yamekuwa wazi tofauti na huko nyuma, kuna ma motivation speaker wengi sana wanaongea kuhusu mahusiano, lakini pia mitandaoni mapenzi yako wazi ni tofauti kabisa na huko nyuma..

Na kiuhalisia mwanamke huwezi kumzuia mume wako kuangalia haya mambo mtandaoni, japo wanawake wengi ingekuwa amri yao wangethibiti waume zao wasiangalie wala kufuatilia mambo ya mapenzi mtandaoni zaidi ya kuangalia simba na yanga... ,lakini hawana huo uwezo wa kuwazuia labda mwanaume mwenyewe akiwa mkomavu wa akili na kiroho anajidhibiti mwenyewe,maana ni ukweli usiopingika asilimia kubwa ya wanaume wanaoangalia sana vitu vya kimapenzi mtandaoni hawana hamu tena na wake zao na hata wakiwa kitandani ni ngumu kuridhika na sex ya wake zao kwa kuwa kile wanachokiona mtandaoni wake zao hawawezi kukifanya maana vile vitu vingine pia vina uvuvio wa kipepo..kwa hiyo kila wakati anahisi kama kuna mahali mke wake hamfikishi..

Hii hali inapelekea wanawake kuwa na hofu ya kuibiwa waume zao, kwa sababu hawana uwezo wa kushindana na wa mitandaoni, maana wa mtandaoni hufanya biashara lakini mke ana majukumu mazito ya kuhudumia familia yaani mume watoto na watu wa nyumbani mwake, sasa kamwe huyu mama hawezi kukimbizana navyo kama wale wa mitandaoni, basi anabaki kujitahidi sana kutaka amfurahishe mume kwa hofu ya watu wa mitandaoni, jambo ambalo wanawake wasipoliangalia wapo hatarini kuvuka mipaka kwenye tendo lao la ndoa na hivyo kumkosea Mungu, lengo likiwa ni kumtuliza mume na kumfurahisha ..

Ushauri

Mwanamke imarisha mahusiano yako na Mungu usalama wa ndoa yako uko hapo
Sina maana usiwajibike, wajibika kulingana na mapenzi ya Mungu, Mungu atamdhibiti mume wako... kamwe usiifuatishe namna ya ulimwengu eti tu umfurahishe mume hapana, baki kwenye mstari wa Mungu..

Mwanaume usidanganyike na vitu vya mtandaoni, yale ni maigizo kwa kiasi kikubwa
Hakuna bora kuliko mkeo wako ..jifunze kumhofu Mungu kama mungu mdogo kwenye familia ili familia yako ijae utukufu kwa wa Mungu..

Pastor Leah..
 
Well spoken Pastor
 
Back
Top Bottom