Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,611
Shirika la Umoja wa Mataifa lenye dhamana ya kuwahudumia wakimbizi, UNHCR limesema idadi ya wakimbizi wanaokimbia vita nchini Ukraine imepindukia watu 368,000.
Katika taarifa yake aliyoitoa kupitia mtandao wa Twitter, kamishina mkuu wa shirika hilo amesema idadi imekuwa ikibadilika kila wakati.
Shirika hilo limesema kwa makadirio ya Jumamosi zaidi ya watu 150,000 wamekimbilia Poland, na mataifa mengine ikiwemo Hungary na Romania.
Poland imesema hadi leo hii zaidi ya wakimbizi 156,000 wameingia katika mipaka ya taifa hilo.
Ndani nchini Ukraine hali imeendelea kuwa tete ambapo majeshi ya Ukraine na Urisi yanaelezwa kukabiliana vikali katika mitaa ya mji wa pili kwa ukubwa wa Ukraine wa Kharkiv wenye jumala ya watu milioni 1.5.
Pia soma:
- Raia wa Ukraine watoroka nchi yao kukimbilia usalama