Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 8,274
- 25,322
Wapinzani wakiandamana nchini DRC Congo.PICHA: MTANDAO
UMOJA wa Mataifa (UN) umetoa wito wa kuachiwa mara moja kwa watu 30, wa chama kikuu cha upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kutoka mahabusu.
Wanachama wa vyama vikuu viwili vya upinzani vya Union for Democracy (UD) na wenzao wa Social Progress (SP), walikamatwa siku ya Jumapili katika mji wa Lubumbashi, ulioko Kusini Mashariki mwa nchi hiyo, baada ya polisi kuvunja mkutano waliokuwa wakiufanya.
Utawala wa Rais, Joseph Kabila, umepiga marufuku mkutano wa aina yoyote wa kisiasa, pamoja na maandamano ya upinzani, baada ya muda wake wa kuongoza kama Rais kisheria, kumalizika takribani mwaka mmoja uliopita.
Na Rais Kabila ameendelea kuwa madarakani hata baada ya muhula wake huo kumalizika.
Tume ya uchaguzi nchini humo, imesema kuwa, haitakuwa rahisi kuandaa uchaguzi mkuu wa Urais, kabla ya mwezi Aprili mwaka ujao wa 2019.
Chama kingine cha upinzani cha Union for the Congolese Nation (UCN), kimesema kwamba, kitajiondoa katika serikali ya umoja wa kitaifa kutokana na hatua ya kucheleweshwa kwa uchaguzi mkuu.
Maandamano ya mara kwa mara ya upinzani nchini humo yamekabiliwa vikali na utawala wa Rais Kabila.
BBC