UN yakubali kushindwa mgogoro wa Ukraine baada ya kiev kushambuliwa

Labani og

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
15,770
24,200
Vita vya Ukraine: Makombora yapiga Kyiv, Umoja wa Mataifa wakiri kushindwa

Makombora yamepiga Kyiv wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini humo, ambapo alikosoa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Antonio Guterres amesema baraza hilo limeshindwa kuzuia au kumaliza vita nchini Ukraine.

Hiki kilikuwa "chanzo cha kukatishwa tamaa sana, kufadhaika na hasira," alisema.

"Niseme wazi kabisa: [ilishindwa] kufanya kila kitu katika uwezo wake kuzuia na kumaliza vita hivi," aliongeza.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 15 limepewa jukumu maalum la kuhakikisha amani na usalama wa kimataifa.

Lakini imekabiliwa na ukosoaji, ikiwa ni pamoja na serikali ya Ukraine, kwa kushindwa kuchukua hatua tangu uvamizi huo uanze mwezi Februari.

Urusi ni miongoni mwa wanachama watano wa kudumu wa baraza hilo na imepiga kura ya turufu zaidi ya azimio moja kuhusu mzozo huo.

Bwana Guterres alikuwa akizungumza Alhamisi jioni katika mkutano wa waandishi wa habari pamoja na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ambaye hapo awali amelikosoa Baraza la Usalama.

"Niko hapa kukuambia Bw Rais, na kwa watu wa Ukraine, hatutakata tamaa," alisema.

Lakini Bw Guterres pia alitetea shirika lake, akikiri kwamba wakati Baraza la Usalama "limepooza" Umoja wa Mataifa ulikuwa unachukua hatua nyingine.

"Umoja wa Mataifa lina wafanyakazi 1,400 nchini Ukraine ambao wanafanya kazi ili kutoa msaada, chakula, pesa taslimu na aina zingine za usaidizi," aliiambia BBC.

Katika kikao cha Alhamisi, Rais Zelensky alisema Bw Guterres alikuwa na nafasi ya kushuhudia kwanza "uhalifu wote wa kivita" uliofanywa na Urusi nchini Ukraine.

Kiongozi huyo wa Ukraine alielezea tena vitendo vya Urusi nchini mwake kuwa ni "mauaji ya halaiki".

Wakati wa ziara ya mkuu wa Umoja wa Mataifa, milipuko miwili ilipiga wilaya ya kati ya Shevchenko huko Kyiv, na watu watatu kupelekwa hospitalini wakiwa na majeraha, kulingana na meya wa jiji hilo.

Bw Guterres pia alitembelea maeneo kadhaa ambapo Ukraine inaishutumu Urusi kwa kufanya uhalifu wa kivita. Moscow inakanusha mashtaka.

Katika mji wa Borodyanka, kaskazini-magharibi mwa Kyiv, Bw Guterres alizungumza na waandishi wa habari mbele ya majengo ambayo yalikuwa yameharibiwa na mashambulizi na makombora.

Alisema tovuti hiyo ilimfanya kufikiria jinsi itakavyokuwa kwa familia yake mwenyewe, akiviita vita vya Ukraine "upuuzi katika Karne ya 21."

Na Bw Guterres alitoa ombi la dhati kuokoa maelfu ya watu katika mji wa kusini mwa Ukraine wa Mariupol, ambao umeharibiwa kabisa na majuma kadhaa ya mashambulizi makali ya Urusi.

"Mariupol ni mgogoro ndani ya mgogoro," alisema. "Maelfu ya raia wanahitaji usaidizi wa kuokoa maisha, wengi ni wazee na wanahitaji huduma ya matibabu. Wanahitaji njia ya kutoka ''

Urusi hadi sasa imekanusha maombi ya mara kwa mara ya Kyiv ya kuruhusu watetezi wa mwisho wa Ukraine na raia waliokwama katika eneo la viwanda la Azovstal kuondolewa.

Lakini Bwana Guterres baadaye aliiambia BBC kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin alikubali "kimsingi" kuruhusu raia kuhama mji huo.

Majaribio ya hapo awali ya kuwahamisha yamekwama na maafisa wa eneo hilo wamelaumu uvamizi wa Urusi.

Source: BBC news
 
The United Nations has outlived its usefulness and its continued existence is a great disservice to those nations which are considered to be militarily disadvantaged like Ukraine.

Umoja wa mataifa haina maana ni bure kabisa na ile kura ya turufu haifai kabisa kuwepo.
 
Nmeona Kama Kuna dalili ya kuiletea mageuzi kura ya veto
 
Umoja wa mataifa umebaki picha huyo Secretary General anabaki kutetea tumbo lake tuu hana jipya. Utaiambia nini marekani ambae ndio contributor mkubwa kwenye umoja huo? Ndio maana UN yupo kimya marekani anapotangaza kupeleka fedha na silaha Ukraine kwasababu hana cha kumfanya. USA ndio mmiliki halali wa UN
 
Babu wa watu akasema nitorosheni jamani putin asije niangamizia huku nina wajukuu!
20220430_052101.jpg
 
Sasaivi wanalalamika? Yaaani hawa wale kichapo mpaka wajute, Je umoja wa mataifa ulifanya jitihada gani Iraq, Libya au Afghan? Je umoja wa maitafa wamechukua hatua gani kwa marekani kupeleka silaha Ukraine imesema hata neno moja?? Kuna masuala Putin aliyauliza kwa hawa vilaza kabla ya vita wamewacha midomo wazi hawana majibu
 
Nmeona Kama Kuna dalili ya kuiletea mageuzi kura ya veto
Nchi ya kwanza itakayopinga ni US nawengine wote wenye VETO hawatakubali
Hapa ndio hua twasema kua UN inatakiwa ivunjwe nitaasisi yakwanza yahovyo kabisa
Hii OP italeta mabadiliko hii UN haitakiwi kuepo kabisaa
Pia kama itawepo inatakiwa isiwe na jengo la kudumu katika nchi fulani inatakiwa uwe uwanachama wa kiduru kwakila member wa UM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona pro US wa Kuanzia Kilindi hadi mwandiga bila kusahau Namanyele hadi Tunduma mpaka Nanjilinji wanapita humu kwa kunyata ili wasijulikane kana wanapita kwa jinsi wanavyonyooshwa na Putin na hapa wanamsubiri babu anaepungia upepo na kusalimia hewa atoe neno ili wapone
 
Sasaivi wanalalamika? Yaaani hawa wale kichapo mpaka wajute, Je umoja wa mataifa ulifanya jitihada gani Iraq, Libya au Afghan? Je umoja wa maitafa wamechukua hatua gani kwa marekani kupeleka silaha Ukraine imesema hata neno moja?? Kuna masuala Putin aliyauliza kwa hawa vilaza kabla ya vita wamewacha midomo wazi hawana majibu
Miaka 25 Urusi analia na Ukraine,,,Leo hii UN analalama alikua wapi?
 
Vita vya Ukraine: Makombora yapiga Kyiv, Umoja wa Mataifa wakiri kushindwa

Makombora yamepiga Kyiv wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini humo, ambapo alikosoa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Antonio Guterres amesema baraza hilo limeshindwa kuzuia au kumaliza vita nchini Ukraine.

Hiki kilikuwa "chanzo cha kukatishwa tamaa sana, kufadhaika na hasira," alisema.

"Niseme wazi kabisa: [ilishindwa] kufanya kila kitu katika uwezo wake kuzuia na kumaliza vita hivi," aliongeza.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 15 limepewa jukumu maalum la kuhakikisha amani na usalama wa kimataifa.

Lakini imekabiliwa na ukosoaji, ikiwa ni pamoja na serikali ya Ukraine, kwa kushindwa kuchukua hatua tangu uvamizi huo uanze mwezi Februari.

Urusi ni miongoni mwa wanachama watano wa kudumu wa baraza hilo na imepiga kura ya turufu zaidi ya azimio moja kuhusu mzozo huo.

Bwana Guterres alikuwa akizungumza Alhamisi jioni katika mkutano wa waandishi wa habari pamoja na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ambaye hapo awali amelikosoa Baraza la Usalama.

"Niko hapa kukuambia Bw Rais, na kwa watu wa Ukraine, hatutakata tamaa," alisema.

Lakini Bw Guterres pia alitetea shirika lake, akikiri kwamba wakati Baraza la Usalama "limepooza" Umoja wa Mataifa ulikuwa unachukua hatua nyingine.

"Umoja wa Mataifa lina wafanyakazi 1,400 nchini Ukraine ambao wanafanya kazi ili kutoa msaada, chakula, pesa taslimu na aina zingine za usaidizi," aliiambia BBC.

Katika kikao cha Alhamisi, Rais Zelensky alisema Bw Guterres alikuwa na nafasi ya kushuhudia kwanza "uhalifu wote wa kivita" uliofanywa na Urusi nchini Ukraine.

Kiongozi huyo wa Ukraine alielezea tena vitendo vya Urusi nchini mwake kuwa ni "mauaji ya halaiki".

Wakati wa ziara ya mkuu wa Umoja wa Mataifa, milipuko miwili ilipiga wilaya ya kati ya Shevchenko huko Kyiv, na watu watatu kupelekwa hospitalini wakiwa na majeraha, kulingana na meya wa jiji hilo.

Bw Guterres pia alitembelea maeneo kadhaa ambapo Ukraine inaishutumu Urusi kwa kufanya uhalifu wa kivita. Moscow inakanusha mashtaka.

Katika mji wa Borodyanka, kaskazini-magharibi mwa Kyiv, Bw Guterres alizungumza na waandishi wa habari mbele ya majengo ambayo yalikuwa yameharibiwa na mashambulizi na makombora.

Alisema tovuti hiyo ilimfanya kufikiria jinsi itakavyokuwa kwa familia yake mwenyewe, akiviita vita vya Ukraine "upuuzi katika Karne ya 21."

Na Bw Guterres alitoa ombi la dhati kuokoa maelfu ya watu katika mji wa kusini mwa Ukraine wa Mariupol, ambao umeharibiwa kabisa na majuma kadhaa ya mashambulizi makali ya Urusi.

"Mariupol ni mgogoro ndani ya mgogoro," alisema. "Maelfu ya raia wanahitaji usaidizi wa kuokoa maisha, wengi ni wazee na wanahitaji huduma ya matibabu. Wanahitaji njia ya kutoka ''

Urusi hadi sasa imekanusha maombi ya mara kwa mara ya Kyiv ya kuruhusu watetezi wa mwisho wa Ukraine na raia waliokwama katika eneo la viwanda la Azovstal kuondolewa.

Lakini Bwana Guterres baadaye aliiambia BBC kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin alikubali "kimsingi" kuruhusu raia kuhama mji huo.

Majaribiowanza ku ya hapo awali ya kuwahamisha yamekwama na maafisa wa eneo hilo wamelaumu uvamizi wa Urusi.

Source: BBC news
mauaji ya halaiki ameyafanya marekani na nato syria libya iraq afaghanistani,
kama kupelekwa kwenye mahakama ya uhalifu wa kivita wa kwanza kupelekwa awe bill clinton, Bush na Obama,
 
Umoja wa mataifa umebaki picha huyo Secretary General anabaki kutetea tumbo lake tuu hana jipya. Utaiambia nini marekani ambae ndio contributor mkubwa kwenye umoja huo? Ndio maana UN yupo kimya marekani anapotangaza kupeleka fedha na silaha Ukraine kwasababu hana cha kumfanya. USA ndio mmiliki halali wa UN
Nikweli mkuu......
 
Sasaivi wanalalamika? Yaaani hawa wale kichapo mpaka wajute, Je umoja wa mataifa ulifanya jitihada gani Iraq, Libya au Afghan? Je umoja wa maitafa wamechukua hatua gani kwa marekani kupeleka silaha Ukraine imesema hata neno moja?? Kuna masuala Putin aliyauliza kwa hawa vilaza kabla ya vita wamewacha midomo wazi hawana majibu
The world must be balanced....ndicho anachokifanya mwamba Putin
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom